Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,110
- 2,736
Nikiwa kada mkubwa wa CCM, napenda nikwambie wazi kwamba, unatupa wakati mgumu na wananchi. Kumbuka, Katika historia ya dunia, hakuna jeshi serikali au mtawala ambaye ameweza kuwashinda wananchi kutumia mtutu wa bunduki. Vyama vikubwa kama KANU ya Kenya, vimeangushwa na wananchi. Katika Taifa kama Tanzania, yenye raia million 45, ni vigumu kutafakari jinsi polisi wasiofika laki moja waweze kuwadhibiti raia million 45 nchi nzima. Kama wataweza, basi itakuwa ni kwa siku moja tu. Polisi nchini Tanzania hawawezi kuwadhibiti wananchi kwa siku nne mfululizo.
Dalili za sasa zinaonyesha kwamba, wananchi wamechoka. Hawaogopi bunduki tena, na hii ishara mbaya kwetu kama chama, na kwako mbaya zaidi kama rais wa miezi 8 tu
Ikitokea polisi wakadanganyika, kupiga mabomu kwa siku nzima, mabomu yao yataisha siku hiyo hiyo na kesho yake itakuwa ni machafuko. Hawa polisi watavua sare zao na kuingia mtaani ikiwa ndio njia yao ya kusalimika. Ila pia wengine hawatathubutu kuyatumia mabomu wakijua familia zao mitaani hawatakuwa salama. Hata rais mwenyewe ndani ya ikulu hawezi kuwa salama tena, kwa maana kwamba nguvu ya umma utamng’oa madarakani. Ukifika hatua ya kuagiza polisi watumie risasi za moto, bila shaka wewe Amos Makala, Paul Makonda, Mwigulu, IGP na Kamanda Siro mtakuwa wageni wa ICC
Kwa maana hiyo, Rais Magufuli inabidi uwe makini sana, uache tabia za kukurupuka na kuwategemea watu kama Tulia Ackson ambao ndio chanzo cha haya matatizo. Waajiri wako siyo CCM wala polisi, umajiriwa na wananchi. Wananchi hauwawezi. Inaonekana wamefika wamechoka, na usipoangalia, CCM inakufa mikononi mwako, pale polisi watakapowaua raia. Maana ndani ya CCM, viongozi wengi hawakutaki