Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Mtukudzi

Senior Member
Nov 14, 2013
103
408
Katika kile unachoweza kutafsiri kama ni Kenya kuguswa na siasa mpya za Tanzania, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesistiza ustahimilivu wa kisiasa hasa kwa nchi zilizoizunguka. Amesema uchaguzi unafaa kuleta utangamano wa nchi na siyo kinyume chake.

Amedai kuwa siyo siri nchi zinazoizunguka Kenya hazina utulivu mzuri wa kisiasa kama ilivyozoeleka. Amedai kuwa kukosekana kwa utulivu kwa jirani ni hatari kwa Kenya.

Huku akipigiwa makofi na wabunge Rais Kenyatta, amesisitiza kuwa wanasiasa wazee wasiwachokoze wanasiasa vijana badala yake wawalee kwa upendo.

=======

Katika hotuba yake Bungeni, Rais Kenyatta amesema:

Nchi nyingi jirani zetu leo zinahitaji kupeana mikono. Wanahitaji siasa ambazo ushindani haugeuki uadui na vita. Wanahitaji viongozi wa kisiasa waliolenga kujumuisha vijana na waliokata tamaa, bila kuwachochea kuasi dhidi ya nchi zao na wazee wao.

Tumejifunza kama Wakenya kwamba uchaguzi pekee hauwezi kuleta amani na umoja kwa watu waliogawanyika. Kwa hilo, viongozi lazima waafikiane na kuwa madaraja ya kuwavusha watu keuelekea kwenye usalama na ustawi.

------------

Many neighboring countries today need a handshake. They need politics in which competition is not turned into enmity and war. They need political leaders focused on including the young and desperate, not inciting them to revolt against their countries and their elders.

We have learned as Kenyans that elections alone cannot bring peace and unity to a divided people. For that, leaders must reach out to each other and build bridges over turbulent waters to allow the people to cross into safety and prosperity.


Screenshot_20201112-155720_1605185891602.jpg
 
Kenya katika swala la Ukabila na siasa za kimaeneo wamekubuhu! lakini bila kupepesa macho, ndio nchi katika ukandaa wetu yenye demokrasia halisi ya uhuru wa mawazo ya watu, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru mpana katika vyombo vyao vya kutoa haki yani MAHAKAMA!
 
'Huku akipigiwa makofi na wabunge Rais Kenyatta amesema watapokea watu watakaokimbilia Kenya ili waweze kuishi kwa amani.'

'Amesisitiza kuwa wanasiasa wazee wasiwachokoze wanasiasa vijana badala yake wawalee kwa upendo.'

Soon utasikia mkuu wa PORTLAND akisema ndege za KQ ni marufuku hapa na Mahindi hakuna kuwauzia.

'Yaani Mtu unampa ndege tausi lkn bado haridhiki tu,nasema uongo ndg zangu?
 
Kenya mmekomaa kisiasa.Sisi pia inabidi tuingie mtaani ndo viongozi watapata akili.Ila siku itafika tu ambayo wananchi wengi watasema sasa yatosha kuvumilia. Wenyewe wataingia mtaani.
Victoire naona ni wazi kabisa pamoja na ushindi wa gharika, wapenzi na mashabiki ya tulioshinda hatuna furaha ya kweli!...na ni dhahiri hali itakuwa more worse baada ya miezi mitatu hadi sita!

Wengi tutaacha siasa za kishabiki, wengi tutarudi kuwa wanaTanu zaidi ya wanasisiemu!
 
Kumbe ndio maana hakuja kwenye lile igizo la kumuapisha akawaachia wasanii wengine kina Museveni.

Jamaa ana uelewa wa juu sana hasa linapokuja suala la mahusiano kati ya wanasiasa, amepevuka sana kidiplomasia, kagonga pale pale hajataka unafiki.

Kwa kauli zake anaonesha jinsi alivyo mwepesi kujirudi na kufanya mazungumzo na mahasimu wake kisiasa, sio hapa kwetu, ni uadui tu miaka yote.

Haya yanayotokea hapa kwetu atakuwa anayaona mambo ya kishamba sana, kutofutiana itikadi ndio unamuona mwenzio adui, mpaka anakimbia nchi aliyozaliwa upo kimya husemi chochote?!
 
Afwazali

~hebu ulizieni na 'posho serikali yake itakuwa inatoa?'
~na wanaoruhusiwa kukimbilia huko ni viongozi kama akina Lema au hata na raia wa kawaida.!?

*halafu baadae hatawatimua kama alivyomtimua yule Miguna wa Miguna.!?
 
Mmepewa nafasi kwenda kenya msitupigie kelele..maana alitia fitna nyingi aweke mtu anayetaka kashikwa pabaya sasa anatapatapa..wakifikia kuanza kuchinjana tutaenda kuwasuluhisha ..na kama unahasira sana kamsemee magu kwa amsterdam sawa mama..ukishindwa kaa chini fanya kazi
Yajayo yanafurahisha
 
Ruksa kwa Lema, nyalandu na wengine waende kupata hifadhi.

Kenya Inchi ya Amani, Wanasiasa wa Kenya Wanajua Siasa , sio huku Tanzania Inchi ya Kuuwana na kutiana vilema tu.
Nani kauambia Kenya ni nchi ya amani ulishawahi kufika tena na usitamke sie tunaefika mara kwa mara tunaijua fika hakufai.
 
90 Reactions
Reply
Back
Top Bottom