Rais Uhuru Kenyatta atangaza nyongeza ya mshahara wa chini

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya mshahara wa chini zaidi mfanyakazi anastahili kulipwa kwa asilimia 18
553c0f0d989f69500b3e19cc6859a851.jpg

Rais Kenyatta alitangaza hilo wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyoandaliwa katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi

Hadi shilingi 100,000 za marupurupu na malipo ya kufanya kazi saa za ziada hazitatozwa kodi kama njia ya kuwapunguzia wakenya gharama ya kupanda kwa maisha

Nao mshahara ulio chini ya shilingi 13,475 hautatozwa kodi.

Rais amewataka waajiri kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanahudumu katika mazingira salama na kuongeza kuwa Serikali itaanzisha zoezi la kukagua usalama katika maeneo ya kazi

Huku Kenya ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Rais Kenyatta amewataka wakenya kutojihusisha na ghasia akisema kuwa amani ndicho kigezo cha maendeleo ya nchi

Kenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji kiteknolojia wa konza. Amesema ujenzi wa mji huo utabuni nafasi za ajira 16,000 wakati ukijengwa na zingine zaidi ya 200,000 utakapokamilika kujengwa

Rais Kenyatta pia amewashauri wakenya kufanya kazi na mashirika yaliyothibitishwa tu wakati wanatafuta kazi nchi za ng'ambo hasa mashabiki ya kati

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini kenya Francis Atwoli ametaka kubuniwa mji zaidi kwa lengo kupunguza msongamano kwenye mji wa Nairobi na kubuni nafasi za ajira.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Kentatta yupo kwenye uchaguz ndo maana. Hata huku Tz kumbuken nyakat za uchaguzi nn hua knatokea? Kuna mwaka wa uchaguz nliwand enda kutoa hera ATM baada ya mshahara kutoka sikuamn nlcho kkuta na waliongeza kmyakmya. Nyakat za uchaguz wanasiasa hufanya hvyo.
 
Back
Top Bottom