Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,427
Rais Uhuru Kenyatta amekutana na rais Joe Biden wa Marekani huko White House. By the way rais Uhuru kwenye mambo ya diplomasia yupo vizuri sana. Katika miaka tisa ambayo amekuwa mamlakani, amekutana na rais wote watatu wa Marekani waliokuwa madarakani. Amekutana na rais Barack Obama ambaye alikuja Kenya kwa safari ya siku tatu. Obama alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kuja Kenya. Kisha rais Uhuru alikutana na rais Donald Trump katika white house huko Marekani. Sasa rais Uhuru amekutana na rais Joe Biden katika white house huko Marekani. Kwenye suala la diplomasia sidhani kama kuna rais yeyote hapa Africa anayemkaribia rais Uhuru Kenyatta. Congrats Mr. President Uhuru kwa kutuweka kwenye map.