Rais tuziangalie NGOs zote haswa za Afya

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,239
Nimefurahi kwa juhudi zako za kisoma na kutambua upuuzi wa NGOs nyingi zinazotuletea mambo ya ajabu ajabu kupitia misaada ya fedha ambazo kimsingi ni fedha zetu walizotuibia kipindi cha ukoloni na wanazoendelea kutuibia hadi leo.

NGOs nyingi zinapika data ili kuonesha mabaya katika jamii ili tu zinufaike kwa kujidai zinasaidia. Ziko NGOs zinazotuaminisha kuwa eti wanafunzi wa kike wanafeli kwa sababu ya kukosa shule wakati wakiwa kwenye hedhi.

NGOs hizi zinatuaminisha kuwa bila pedi eti watoto wetu wa kike watafeli...huu ni upuuzi na kutuondolea maadili. Leo hii ukiangalia taarifa ya habari na mtoto wako wa kike au mama yako mnaanza kuoneana aibu kwa tangazo la kipuuzi.

Ni lazima kama nchi tuje na miongozo mipya dhidi ya hii western indoctrination.

Pia tupige marufuku ya matangazo yanayosema kwa hisani ya nchi fulani...
 
Wayafutilie mbali haya mashimo ya wezi na wapiga dili, kwanza wanatifua tu amani ya nchi yetu huku wakitimiza masrahi ya mabwana zao wanaowalipa ili kutuchafu. Fungia zote tuondokane na ushenzi
 
Mkuu umefungua hii thread kutokana na tamko
La Magufuli kuhusu kusomesha wanafunzi(wa kike) wenye watoto.

Je wewe unakubaliana na tamko lake la kukandamiza watoto wa kike?
 
Wayafutilie mbali haya mashimo ya wezi na wapiga dili, kwanza wanatifua tu amani ya nchi yetu huku wakitimiza masrahi ya mabwana zao wanaowalipa ili kutuchafu. Fungia zote tuondokane na ushenzi
NGO ni mashimo ya wazungu kutafunia pesa.
 
Mkuu umefungua hii thread kutokana na tamko
La Magufuli kuhusu kusomesha wanafunzi(wa kike) wenye watoto.

Je wewe unakubaliana na tamko lake la kukandamiza watoto wa kike?
Nakubaliana na tamko la Serikali...kwa sababu hakuna sababu ya mwanafunzi kupewa mimba ...tuchague kati ya kuolewa au kusoma!
 
Ni aina ile ile tu ya kudumazwa akili na ubabaishaji ...NGOs ni mkono wa ukoloni mambo leo, ni mshipa wa damu ya ukoloni
 
Hebu niambie Serikali yako inajitosheleza kufanya shughuli za NGOs? Serikali hii inayotegemea misaada? Labda tujikite kwenye hili la watoto wa kike, niambie ni jitihada gani Serikali imefanya kuwasaidia hawa watoto ambao ni vulnerable? Serikali lini imetoa ELIMU YA AFYA YA UZAZI SALAMA KWA VIJANA?
 
Ni aina ile ile tu ya kudumazwa akili na ubabaishaji ...NGOs ni mkono wa ukoloni mambo leo, ni mshipa wa damu ya ukoloni
Vipi kuhusu misaada inayopokewa na Serikali yako? Huo ni Ukoloni Makinikia eeeh?
 
Hebu niambie Serikali yako inajitosheleza kufanya shughuli za NGOs? Serikali hii inayotegemea misaada? Labda tujikite kwenye hili la watoto wa kike, niambie ni jitihada gani Serikali imefanya kuwasaidia hawa watoto ambao ni vulnerable? Serikali lini imetoa ELIMU YA AFYA YA UZAZI SALAMA KWA VIJANA?
Jiulize anayesema hao watoto ni vulnerable ni nani at first place...yaani NGO inakwambia nchi yenu ina wapumbavu wengi ili ije na mradi wa kuondoa upumbavu...kumbe hata huo upumbavu haukuweko.
 
Nakubaliana na tamko la Serikali...kwa sababu hakuna sababu ya mwanafunzi kupewa mimba ...tuchague kati ya kuolewa au kusoma!
Na ambao ni wajawazito sasa tuwafanyaje?
Na Je waliojifungua na wamerudi shuleni tuwafanyaje?
Waliobakwa na kupata ujauzito Je ?
 
Back
Top Bottom