Rais tupe mrejesho wa matamko yako

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,454
4,374
Kipindi cha rais Kikwete na rais Mkapa ulikuwepo utaratibu wa taarifa za kila mwezi kutoka kwa rais kueleza utendaji na msimamo wa serikali ktk mambo mbalimbali kwa maslahi ya taifa.

kupitia Taarifa hiyo, wananchi waliweza kujua uelekeo wa taifa ktk mipango, vipaumbele na utekelezaji au ufanisi wa utendaji wa serikali.

Inawezekana utaratibu huo ukaendelezwa na rais wa sasa.

Tofauti na faida za taarifa nilizo eleza hapo juu, zipo faida zingine
1. Kupunguza Matamko Tata, maana naamin taarifa itakuwa na maelezo ya kutosha yaliyopitiwa au kuhakikiwa.
2. Kupunguza tofauti za kiitikadi/kifikra na kujari maslahi ya nchi, kwa kuwa na vipaumbele na miongozo ya utendaji.
3. Kuzidisha hali ya mshkamano na umoja wa kitaifa.
4. Inaongeza uwajibikaji kwa wananchi kupata mrejesho wa mipango, matamko na utendaji wa serikali.
5. inaongeza ushirikishwaji wa wananchi kwa kutoa maoni yao baada ya kusikiliza hiyo taarifa ya rais



ni mtizamo tu.
 
wananchi wapo tayari kushiriakana na serikali mfano. usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi.

lakini wananchi hawapo tayari kuona mpasuko wa taifa na upotevu wa amani
 
Sasa unalialia nini? Hiyo ni hiari ya mtu usilazimishe

kwa faida yako.

itafika siku yatatolewa matamko tata ambayo yatagharimu nchi(mimi, ww na wengine) kwa kiasi kikubwa na kwa muda mrefu...

na hayo ndio madhara ya matamko yasiyofanyiwa uhakiki na kuangalia usahihi ktk sera, sheria na mipango ya nchi...
 
kwa faida yako.

itafika siku yatatolewa matamko tata ambayo yatagharimu nchi(mimi, ww na wengine) kwa kiasi kikubwa na kwa muda mrefu...

na hayo ndio madhara ya matamko yasiyofanyiwa uhakiki na kuangalia usahihi ktk sera, sheria na mipango ya nchi...
Hayo matamko yakugharimu nchi labda tukiwakabidhi nchi wanywa viroba yatakuja maana Viroba ni noma
 
Hayo matamko yakugharimu nchi labda tukiwakabidhi nchi wanywa viroba yatakuja maana Viroba ni noma

..watakaoficha sukari, sukari hiyo itagaiwa bure kwa raia...

... sukari itauzwa 1800/- kwa kilo...

hayo ni baadhi ya matamko yalimghari hadi mtoto mchanga lakini hadi leo hamna mkakati au mrejesho tumefikia wapi...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom