Rais tunaomba uingilie kati kuhamishwa kimizengwe kwa Mkuu wa Idara ya ukaguzi wa ndani Manispaa ya Ilala

Coster2

Senior Member
Apr 28, 2019
155
250
Katika Manispaa ambazo zilikumbwa na ubadhilifu mkubwa wa pesa za umma na kukosekana kwa systematic audit Manispaa ya Ilala iliongoza kwa kipinding kwa zaidi ya miaka kumi.

Hiii ilitokana na kuwa na mkaguzi wa ndani ambaye hakuweza kuifanya kazi yake kwa weledi. Lakini mnamo mwaka jana 2020 mwezi March aliyekua mkaguzi wa ndani toka Manispaa ya Ubungo, ndugu Bikmbo Mujuni alihamishiwa manispaa ya Ilala na baada ya miezi michache tuliweza kuona alivyoibua madudu mengi katika idara zote kuanzia idara ya fedha, afya na zinginezo, tulishuhudia riport zikitoka kwa wakati, ubadhilifu wa fedha za umma ukiibuliwa.

Kwa kuona hivyo ndugu Bikombo Mjuni ameletewa zengwe na idara ya utumishi pamoja na idara ya uhasibu mpaka kupelekea kupewa barua ya kuhamishiwa Morogoro vijijini, kwa sababu tu alikataa kushiriki upitishwaji wa madodoso feki, mkaguzi huyu anaondlolewa Manispaa ya Ilala kwakua tu amekuwa akipingana na njama chafu za ukwapuaji wa pesa katika vifungu mbalimbali katika manispaa ya Ilala, tunakuomba mheshimiwa rais kupitia vyombo vyako vya uchunguzi kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu sakata hili.

Ndugu Mjuni anaondolewa kimizengwe ili watu wafanye mambo yao maovu, pia mnaweza fuatilia utendaji wake wa kazi tangu akiwa manispaa ya ubungo, ni mchapakazi, mwaminifu na ni mtu ambaye kweli anaijua kazi yake. Tunaiomba sana serikali imwache mkaguzi huyu katika manispaa yetu ya Ilala walau aweze kuendelea kusawazisha mambo.
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,644
2,000
Idara ya Utumishi haiwezi kumhamisha mtumishi pasipokuwa na idhini ya DED, tena baada ya kwenda kufanya lobbying huko TAMISEMI ikizingatiwa uhamisho unaambatana na gharama zake.

By the way umuhimu wa huyo Internal Auditor utaonekana siku Halmashauri itakapopata hati Chafu FY 2020/21
 

Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
658
1,000
Hii ipo Sana ukitekeleza majukumu yako vilivyo, jipange kuhamishwa au kufukuzwa kazi kabisa.

Katika maisha yangu nimeyashuhudia Sana haya.
 

Coster2

Senior Member
Apr 28, 2019
155
250
Yani mtu anayesimamia sheria na haki anaonekana hafai, kuna kakikundi pale wameifanya kama manispaa ni mali yao
 

Kibosho Mjini

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
1,802
2,000
Yani mtu anayesimamia sheria na haki anaonekana hafai, kuna kakikundi pale wameifanya kama manispaa ni mali yao

Kwanini hutaki kwenda Morogoro?

Hayo madodoso feki yalihusu nini na yalitaka pesa kiasi gani?

Uliundiwa zengwe gani hadi uhamishiwe Morogoro?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom