fiksiman
JF-Expert Member
- May 17, 2008
- 402
- 107
Ni wazi kabisa vuguvugu la kisiasa linaelekea kushoto kwa Mhe. Zitto Kabwe, sitaki kujihusisha na malumbano ya nani yuko sahihi kati ya Zitto na Viongozi wake. Ukweli utaendelea kubaki kuwa Zitto ni mwanasiasa mchapakazi, mzalendo ameitendea haki siasa ya nchi hii na ikitokea uongozi wa CHADEMA wakamfuta nakuomba Ndugu Rais umpe nafasi kati ya zile 10 ulizopewa aendelee kukutumikia watanzania.
Ghilba za kisiasa zimefanikiwa kumchafua kijana huyu ambae kwa mara ya kwanza alionyesha umuhimu wa kuwa mbunge hasa kijana na kutufanya wengi wetu kufuatilia shughuli za bunge. Chadema wanaweza wasimhitaji lakini nchi hii nahakika inamhitaji sana hivyo muandalie nafasi kama uliyompa Mbatia atusaidie kuweka adabu bungeni badala ya hao wanaoomba miongozo kila kukicha. Historia itawahukumu wana chadema kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. Kama kweli amekosea basi zipo njia nyingi za kumuadabisha dhidi ya kumvua uanachama ili akose sifa ya kuwa mbunge.
Kumbukeni wanachadema Zitto amechaguliwa na wanakigoma tena katika siasa ngumu za vyama vingi hilo linatosha kuheshimu na kumchagulia adhabu mbadala. Kama mlikubali Shibuda nahakika sio ngumu kumsamehe (bila kuhusisha jaZba) kijana wenu.