Rais Tshisekedi wa DRC amekataa kudungwa chanjo ya Uingereza ya AstraZeneca

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Rais Tshisekedi wa DRC amekataa kudungwa chanjo ya Uingereza ya AstraZeneca

Rais Tshisekedi wa DRC amekataa kudungwa chanjo ya Uingereza ya AstraZeneca

Utata umeibuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kubainika kuwa rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi amekataa kudungwa chanjo ya corona ya shirika la Uingereza la AstraZeneca.

Duru zinadokeza kuwa, wakati serikali inahamasisha wananchi wapate chanjo hiyo, Rais Tshisekedi haiamini chanjo hiyo aina ya AstraZeneca. Hali ya utata sasa imeibuka kwani mtazamo huo wa rais ni kinyume cha mpangp wa serikali wa kuwaaminisha wananchi wakubali chanjo hiyo wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Corona au COVID-19.

Msimamo huu wa Rais Tshisekedi, umezua maswali mengi kuhusu ni vipi, hataki kupata chanjo hiyo wakati serikali anayoiongoza, ikiwataka wananchi wapate chanjo hiyo.

Rais Farmaajo wa Somalia akipata chanjo ya corona hadharani ili kuwahamasisha wananchi wakubali chanjo hiyo

Wanasiasa na wanadiplomasia wamemkosoa Tshisekedi kwa msimamo wake huo. Mgombea wa urais mwaka 2018 Martin Fayulu amesema rais wa nchi alipaswa kuwa katika mstari wa mbele na kuonyesha mfano mzuri kwa kupokea chanjo hiyo ya AstraZeneca.

Aidha balozi mmoja wa nchi ya Kiafrika ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema Thisekedi kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipaswa kuonyesha mfano kwa kuchomwa chanjo ya AstraZeneca inayotumiwa na Waafrika wengi.

1625497019607.png
 
Bottom line ya corona ni chanjo...either pesa au effect baada ya chanjo...Mara paap.,,wanaume waliochanjwa wanajikuta tu wanaunga mkono ushoga
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom