Rais Trump ashangazwa na uwezo wa kucheza danadana wa mwanamke mtanzania anaye-trend mtandaoni

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,535
2,000
Uwezo wa mwanamke huyu mjuzi wa mpira na danadana za miguu na kichwa, umeushangaza ulimwengu baada ya clip hii kusambaa mtandaoni wiki hii. Uwezo wake si wa kawaida, anavyouchezea mpira, utadhani Ronaldinho au mchezaji nyota mwingine wa soka duniani mwenye stamina ya aina yake aushikapo mpira na kuuchezea.

Clip hii imefanikiwa kuyafurahisha macho ya moja ya watu wenye nguvu zaidi duniani kwa sasa, Rais wa Marekani, Donald Trump. Kama mamilioni ya watu wengine duniani walivyoiona video hii, Trump naye ameiona kupitia Twitter, mtandao anaotumia zaidi kutangaza propaganda zake.

Ameiona kupitia akaunti ya Akin Sawyer aliyeipost video hiyo Jumamosi ya February 16 na kuandika ‘talent is evenly distributed, opportunity isn’t.’ Video hiyo hadi sasa imetazamwa kwa zaidi ya mara milioni 9 kwenye mtandao huo.

Jumanne ya February 19, Trump aliiretweet post hiyo kwenye akaunti yake yenye followers milioni 58.4 na kuandika ‘Amazing.’ Tweet yake imekuwa retweeted kwa zaidi ya mara elfu 33, watu zaidi ya 119,000 wameilike na imepata comments zaidi ya elfu 9.


04E8D788-972C-413E-9CA7-67ADE133363C.jpeg


Kama hilo limekushangaza, hebu sikia hili. Mwanamke huyu anaitwa Hadhara Charles Mjeje na ni Mtanzania. Video hiyo iliyosambaa imechukuliwa Lilongwe, Malawi alikoenda tangu January mwaka huu kuonesha uwezo wake huo na kujipatia fedha za kujikimu.
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom