Rais Trump anapanga kuipiga marufuku App ya Tik Tok kutoka China ifikapo Septemba 15

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,068
10,010
Rais Donald Trump ametangaza kuwa ndani ya siku 45 zijazo atazuia mitandao ya kijamii ya TikTok na WeChat inayomilikiwa na wachina kama isipouzwa kwa wamarekani ndani ya siku 45 zijazo

Trump alipanga kuzuia mitandao hiyo Septemba 15, ikiwa mitandao hiyo haitauzwa. Aidha mitadao hiyo ilikuwa katika maongezi na kampuni ya kimarekani ya Microsoft

TikTok ina watumiaji zaidi ya milioni 100 nchini Marekani. Azma ya Rais Trump kuifunga mitandao hiyo imetokana na ugomvi wa kisiasa

Aidha Rais Trump amekuwa akilaumu mtandao huo kuiba taarifa za watumiaji wake na kupeleka kwa serikali za China. Hivyo Rais Trump anaona kwa usalama wa taarifa ni heri azuie mtandao huo au usiendelee kumilikiwa na wachina

====
Rais Trump alisema Jumatatu hatojali kama kampuni ya Microsoft inajiongeza kuichukua APP ya Tik Tok lakini ununuzi huo utatakiwa kukamilika ifikapo Septemba 15 mwaka huu

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumatatu kwamba atapiga marufuku APP maarufu ya video iitwayo Tik Tok ya China ifikapo Septemba 15, vinginevyo kampuni ya Microsoft au kampuni nyingine yeyote ile ya Marekani iinununue kama uamuzi wake.

Rais huyo kutoka chama cha Republican alisema wiki iliyopita kwamba atapiga marufuku APP hiyo ambayo inamilikiwa na kampuni ya kichina ya ByteDance kwa sababu ya wasi wasi wa usalama. Rais Trump alisema Jumatatu hatojali kama kampuni ya Microsoft inajiongeza kuichukua APP hii lakini ununuzi huo utatakiwa kukamilika ifikapo Septemba 15.

Katika taarifa Microsoft ilithibitisha kwamba mkurugenzi wake mkuu alikutana na Rais Trump na alikuwa na nia ya dhati kuinunua kampuni ifikapo tarehe ya mwisho iliyotolewa. Trump aidha alisema angependa kuona kiasi fulani cha fedha zitakazolipwa katika makubaliano hayo ya ununuzi kinaenda kwa wizara ya fedha ya Marekani.
 
Back
Top Bottom