Rais Trump achukizwa na tuhuma za Comey

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,599
2,000
Rais Trump pamoja na timu yake wamejibu vikali dhidi ya tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa mkurugenzi wa FBI ,kuwa rais Trump alimtaka kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na Urusi.

Hapo jana James Comey alihojiwa na Kamati ya Bunge la Seneti ya Usalama na kumtupia lawama Rais Trump kwa kuingilia uchuguzi unamhusu kujihusisha na Urusi. Wakili binafsi wa rais Trump,Marc Kaswitz amepinga vikali shutuma hizo zilizotolewa na Comey na kudai kuwa huo ni uzushi.

"Raisi hakuwahi kutoa maelekezo au mapendekezo kwa Comey kuacha kumchunguza wa mtu yeyote ".
Rais Trump pia alitoa mustakhabali wake juu ya suala hili;

"hakuna kitu chenye dhamani ambacho kinakuja kiurahisi,lakini tunajua jinsi ya kupambana vizuri zaidi mtu mwingine yeyote na hatutakata tamaa .Sisi ni washindi na tunaenda kupambana na kushinda na tutakuwa na mustakabali ambao hauelezeki kwa siku za mbeleni,na tutaenda kuwa pamoja

Comey katika ushaidi alioutoa alieleza namna ambavyo alijisikia vibaya mara baada ya rais Trump kumtaka kuachana na uchunguzi huo wa mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na juu ya urusi.
Na anaona ndio sababu ilionekana haendani na majukumu ya shirika la kijasusi la FBI

Donald Trump and his team have reacted furiously to allegations by the former head of the FBI that the president ordered him to drop an inquiry into links between his disgraced National Security Adviser and

Chanzo; BBC Swahili
 
Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,389
2,000
Tusubirie hizo rekodi zitatupa ukweli kama zipo. Sijaona jipya kwa yale yaliyosemwa wazi labda kwa hayo yaliyosemwa private. Ambaye hakujua Trump ni muongo sijui ni nani. Trump anapambana na Queen of Chaos Hillary muongo wa karne na establishment iliyojiandaa kunufaika na urais wake na hao interest zao zimeguswa. Ila naye ajipange yeye sio CEO wa Trump Organization sasa ni Rais na kuna namna ya kufanya mambo kwa kupitia watu wengine na institutions na sio kila kitu atoe kauli yeye. Dunia ina viongozi waropokaji sana na wepesi wa maamuzi na matamko.Binafsi Comey amenishangaza kukiri ku-leak taarifa na sasa naamini yapo mengi taasisi hiyo iliyatoa kupitia vyombo tofauti tofauti kipindi cha uchaguzi.
 
Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,389
2,000
Obama anajaribu kurusha miguu ya mwisho-mwisho
Yaani anaumia legacy yake kufutwa na mtu kama Trump na watu wake na Hillary kuwa watazamaji na sio wanufaikaji wakubwa. Yaani jana wameanza kujadili tena namna ya kuiondoa Obama Care basi miguu itatupwa hata kupitia Russia mradi tu Trump aonekane hafai. Wanajiharibia nchi wenyewe kwa maslahi ya wachache na kuirudisha heshima ya nchi yao itawachukua tena muda. Queen of Chaos hataki kabisa kukubali na navyomuona hata Pence akiwa Rais watamfitini tu manake hata Comey jana kaanza kumuonyesha nae VP kuwa muongo na kuwa alijua kuhusu Flynn toka mwanzo. Its a game worth watching.
 
Chenchele

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,753
2,000
Naona mwisho wa usupa power huu...getup Russia and China where are you!! Yaani kabibi ka clinton sijuw kanataka nini?
 
Kabibi kanataka POWER tu,hela kanazo ukisoma The Clinton Cash utaelewa ila sasa kanataka Power na kamefika hapo kwasababu ya connections sasa unavyojua hakuna free lunch kwahiyo zile connections nazo zinataka malipo ya matarajio. Soros na wenzie walitoa hela ili mob queen awe Rais haijawa hivyo.
Sijawahi ona biandamu anapenda power na ameitafuta zaidi ya Hillary napata hofu kuwaza nini kitatokea akiwa Rais wa Marekani.

Ukweli China na Russia navyowaona na safari zao wanajipanga kisawasawa. Wavurugane huko ndani nchi nyingine zijijenge. Hadi muisrael anafanya strategic partnership na Africa kwa kiasi kikubwa zaidi kuna jambo wameliona.
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,660
2,000
Obama anajaribu kurusha miguu ya mwisho-mwisho
Hilary ana mapungufu yake sawa na Trump. Issue hapa ni kuondoa UBEPARI unaokua kwa kasi sana. Swala la Health Care ni janga kwa medium n low class. Ubaguzi unakuwa kwa kasi sana kama enzi za utumwa. Trump ana mazuri yake na mapungufu yake. Somo zuri kwa REPUBLICANS wamuulize Bi May/UK
 
INGENJA

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
4,995
2,000
Yaani anaumia legacy yake kufutwa na mtu kama Trump na watu wake na Hillary kuwa watazamaji na sio wanufaikaji wakubwa. Yaani jana wameanza kujadili tena namna ya kuiondoa Obama Care basi miguu itatupwa hata kupitia Russia mradi tu Trump aonekane hafai. Wanajiharibia nchi wenyewe kwa maslahi ya wachache na kuirudisha heshima ya nchi yao itawachukua tena muda. Queen of Chaos hataki kabisa kukubali na navyomuona hata Pence akiwa Rais watamfitini tu manake hata Comey jana kaanza kumuonyesha nae VP kuwa muongo na kuwa alijua kuhusu Flynn toka mwanzo. Its a game worth watching.
hivi snowden hawezi kuwa zao la republican kweli??
 
Chenchele

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,753
2,000
Kabibi kanataka POWER tu,hela kanazo ukisoma The Clinton Cash utaelewa ila sasa kanataka Power na kamefika hapo kwasababu ya connections sasa unavyojua hakuna free lunch kwahiyo zile connections nazo zinataka malipo ya matarajio. Soros na wenzie walitoa hela ili mob queen awe Rais haijawa hivyo.
Sijawahi ona biandamu anapenda power na ameitafuta zaidi ya Hillary napata hofu kuwaza nini kitatokea akiwa Rais wa Marekani.

Ukweli China na Russia navyowaona na safari zao wanajipanga kisawasawa. Wavurugane huko ndani nchi nyingine zijijenge. Hadi muisrael anafanya strategic partnership na Africa kwa kiasi kikubwa zaidi kuna jambo wameliona.
Mabibi kanataka kuiangusha russia either kijeshi au kiuchumi na ndyo mana Putin hakupenda kapite sasa naona kanataka madaraka sio tu kuongoza US bali kuonesha ubabe na ushetani wao.
 
Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,389
2,000
Hilary ana mapungufu yake sawa na Trump. Issue hapa ni kuondoa UBEPARI unaokua kwa kasi sana. Swala la Health Care ni janga kwa medium n low class. Ubaguzi unakuwa kwa kasi sana kama enzi za utumwa. Trump ana mazuri yake na mapungufu yake. Somo zuri kwa REPUBLICANS wamuulize Bi May/UK

Pakawa nielimishe namna ambavyo mapungufu ya Hillary ni sawa na ya Trump? Trump mja jana na bibi wa establishment toka yuko chuo yeye anatumikia tu establishment.

Ubepari unaondolewaje jamani nauchukia mno ila namna wanavyouondoa siifahamu.

Ubaguzi unakuwa wazi sasa ila sidhani utafikia enzi za utumwa haiwezi tokea vile tena naamini
 
Michelle

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,389
2,000
Mabibi kanataka kuiangusha russia either kijeshi au kiuchumi na ndyo mana Putin hakupenda kapite sasa naona kanataka madaraka sio tu kuongoza US bali kuonesha ubabe na ushetani wao.

Kabibi kababe jamani kanapambana hata kakiwa nje ila Mrusi nadhani anakunywa Vodca tu huku akikapangia mkakati. Juzi niliona Putin akihojiwa akaniudhi kusema yeye hanaga bad days kwakuwa yeye si mwanamke. Hii vita pengine hata ilikuwa ni ya jinsia he he he yaani yeye aliona haifai kiongozi wa taifa kubwa duniani awe ke. Putin sasa yuko na BRICS yao na anaendelea kuwazunguka tu waliomwekea vikwazo vya kiuchumi. Huu mchezo hauhitaji hasira kabisa ni kuelewa nia ya adui,kuhakikisha una monitor adui na mipango yake na kufanya unaloweza na wasiokuwekea vikwazo.
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,888
2,000
Trump Akivuka Viunzi Vyotet Hivi Mpaka Amalize Miaka Yake Salama Akachinje Kondoo Amle Nyama Choma Tu Ashushie Na Jack Daniel Yaani Tangu Mwanzo Anaandamwa Kama Mpira Wa Kona
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,660
2,000
Pakawa nielimishe namna ambavyo mapungufu ya Hillary ni sawa na ya Trump? Trump mja jana na bibi wa establishment toka yuko chuo yeye anatumikia tu establishment.

Ubepari unaondolewaje jamani nauchukia mno ila namna wanavyouondoa siifahamu.

Ubaguzi unakuwa wazi sasa ila sidhani ila utafikia enzi za utumwa haiwezi tokea vile tena naamini
Michelle, sikuwa na maana mapungufu yao yanafanana isipo kila mmoja ana mapungufu. Republicans wana mapungufu so as Democrats.
UBEPARI utapungua endapo matajiri watalipa kodi stahiki kuliko sasa matajiri wanasamehewa kodi medium n low class pays more
Watu wameshikwa na kiburi wamekuwa na uthubutu wa kuwaambia watu 'You don't belong here go back to your country' Nani anawapa jeuri hii?
North America si ya wazungu bali ni ya Red Indians. Jamii ya Trump believe wao ndio wazawa halisi the rest mrudi kwenu'
Utumwa upo bado amini hilo!
 
Trump ni mjermani by nature!! Babu yake Trump mzee Drumpf alivo fika US wakamwita jina Trump akazaa mtoto John Na john akapata Huyu Orange Trump haha!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom