Rais Trump achukizwa na kauli ya kuitwa ‘MZEE’ na Kim Jong Un, ahoji mbona yeye hamuiti 'mfupi na mnene'?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Trump.jpg

Wakati vita vya maneno vikiendelea kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un inaonekana Trump kuguswa zaidi na kauli zilizotolewa jana na serikali ya Korea Kaskazini kwa kumuita kuwa ‘mzee na mchochezi wa vita’ kitu ambacho kimemfanya aweke wazi hisia zake kuwa angefurahi siku moja kuona wanakaa meza moja na Kim.

Wizara ya mashauriano ya nchi za kigeni nchini Korea Kaskazini jana ilimuita Trump kuwa “mchochezi wa vita na mzee” na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nyuklia.

Kauli ambayo Rais Donald Trump alishindwa kujizuia kuijibu kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee wakati yeye hata siku moja haijawahi kutokea kumkebehi kuwa mfupi na mnene.

Kwanini Rais Kim Jong-un ananitukana kuwa mimi ni mzee wakati mimi hata siku moja sijawahi kumuita yeye mfupi na mnene? Sawa najaribu kila niwezalo kuwa rafiki yake najua ipo siku tutakuwa marafiki.“ameandika Rais Donald Trump.



Hata hivyo huenda Rais Trump amesahau kwani awali alinukuliwa akimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini, kwa kumuita mwendawazimu na ‘mtu wa kuunda zana za roketi’.

Hatua hiyo ya Rais Trump kujibu kauli ya Korea Kaskazini imezua gumzo nchini Marekani wengi wakimuona Trump kama Rais anayeongoza taifa hilo kubwa duniani kwa mzaha.
 
Basi miaka 75 ni kijana

Team USA watakuja kusema Trump anaomba urafiki ili ammalize vzr Kim
 
Ati hajamuita kumbe ndio anamuita katumia fasihi simulizi ktk kumuita mfupi + mnene
 
hapo trump hajachukia bali alikuwa anajibu kashfa kwa kumkashifu kim kwan ni emolo na tunyenye
 
Dah trump huwa namkubali sana yeye huwa anacheza na saikolojia tu bwana mdogo kim kwanza alistuliwa na mr rocket man leo kaja na mfupi + mnene

Trump hapo anajarbu kumtia ndim kim na kumdhohofisha kisaikolojia na kumpotezea kujiamini mbele ya kadamnasi
 
Dah trump huwa namkubali sana yeye huwa anacheza na saikolojia tu bwana mdogo kim kwanza alistuliwa na mr rocket man leo kaja na mfupi + mnene

Trump hapo anajarbu kumtia ndim kim na kumdhohofisha kisaikolojia na kumpotezea kujiamini mbele ya kadamnasi
Mmmh.
Hamna saikolojia HAPO
 
Mmmh.
Hamna saikolojia HAPO
Kwa siasa za marekani ni ngum sana rais aitwe vibaya (mzee) na akaonesha kukasirika mbele ya hadhara

Trump amepitia mengi tang kipnd cha kampen alivoitwa kibamia had leo hii

Hapo trump anacheza na saikolojia ya kim tu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa siasa za marekani ni ngum sana rais aitwe vibaya (mzee) na akaonesha kukasirika mbele ya hadhara

Trump amepitia mengi tang kipnd cha kampen alivoitwa kibamia had leo hii

Hapo trump anacheza na saikolojia ya kim tu
Kwanza MAREKAN NDIKO RAIS ANAITWA VIBAYA NA ANACHORWA VIBAYA SANA KWA sababu ya demokrasia yao,angalia ukurasa wake wa twita anavyoshambuliwa.
Pili TRUMP ni kweli MZEE,na hata aliposhinda watu waliliongelea hilo sasa hapo AMEITWAJE VIBAYA
 
Back
Top Bottom