Rais Shein, kuhutubia Baraza la Wawakilishi kesho

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Wakati CUF wanatangaza kutomtambua Dr Shein kama Rais, yeye atahutubia baraza lake kama kawaida.
Siasa zetu bana, kichekesho kweli!

shein..jpg

Rais wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) Dk Ali Mohamed Shein.

Zanzibar. Rais wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) Dk Ali Mohamed Shein kesho atazindua Baraza la Wawakilishi la tisa huku akitarajia kutoa mwelekeo wa Serikali yake mpya iliyopatikana baada ya Uchaguzi wa Marudio wa Machi 20 uliotawaliwa na mgawanyiko wa kisiasa.

Tofauti na hotuba yake ya ufunguzi ya Novemba 2010, Dk Shein atahutubia baraza hilo likiwa na wabunge wa chama kimoja cha CCM baada ya vyama vya upinzani vilivyotangaza kushiriki uchaguzi wa marudio kushindwa kupata viti vya uwakilishi.

Pia, atahutubia akiwa bado hajamteua Makamu wa Kwanza wa Rais kutokana na matokeo ya uchaguzi huo kutofanikisha kupatikana chama cha upinzani chenye kura zisizopungua asilimia 10 za kufanikisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Chama kikuu cha upinzani cha CUF na vingine tisa vilisusia kushiriki uchaguzi huo baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutokana na sababu za uvunjifu wa taratibu na sheria za uchaguzi.

Hata hivyo, majina ya wagombea wa vyama hivyo yalijumuishwa kwenye karatasi za kura na kusababisha kuvuna kura kidogo ambazo hazikitosha kutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na Wawakilishi ambao miongoni mwao huteuliwa kuwa mawaziri wa SMZ.

Tayari Dk Shein alishaeleza kiufupi baada ya kuapishwa majuma mawili yaliyopita kuwa Serikali yake itakuwa shirikishi kwa kujumuisha upinzani na haitabagua katika utoaji wa huduma za jamii katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Jambo kubwa ambalo Wazanzibari wengi wanasubiri kulisikia kutoka kwa kiongozi huyo leo ni iwapo ataeleza kinagaubaga namna atakavyokabiliana na mtanzuko wa kikatiba wakati wa uundaji wa SUK.

“Ningependa Rais atueleze kwa kina atakavyounda Serikali yake kwa sababu hadi sasa yupo kimya. Hatujasikia akimteua Makamu wa Kwanza wa Rais tofauti na ilivyokuwa mwaka 2010 zaidi tu ya kuona amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais,” alisema Yusuph Ali, mkazi wa Kwa Pweza.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na sheria visiwani hapa wanaona bado ni vigumu kutabiri kikamilifu hotuba ya Dk Shein na kwamba huenda asigusie kabisa mtanzuko wa kikatiba katika uundaji wa SUK badala yake akajikita kwenye mipango ya maendeleo.

Mwanasheria Awadh Ali Said alisema Dk Shein leo anahutubia akiwa “amebeba bahasha ya changamoto ambazo hata baada ya kutaja dira ya Serikali yake zinaweza kumfanya asifanikiwe vyema kutekeleza mipango yake.”

“Rais Shein anazindua Baraza la chama chake ambalo litadolola kutokana na kukosekana upinzani. Anazindua pia akiwa na swali la kujibu la namna atakavyounda Serikali iliyokidhi matakwa ya kikatiba katika uundaji wa SUK tofauti na alivyozindua mwaka 2010,” alisema Said.

Chanzo: Mwananchi
 
Siasa za Tanzania in vichekesho , katiba imemgomea MKUU kuteua Makamo wa kwanza .Lakini CCM inauwezo wa kutumia katiba yake kumteua makamu wa kwanza
 
Shein aje na jibu kwanini kwenye sherehe za muungano zilizofutwa na watanganyika yeye kabarki uamuzi huo na kwanini mgao asipate kwenye kubariki uamuzi huo wa kufuta sherehe.
 
Mkutano wa makamo mwenyekiti wa chama na wawakilishi wa majimbo yote wa chama
 
Najaribu kuwaza.Shein anajisikiaje baada ya wahisani kututumbua?
 
Siasa za ccm wakati mwingine huwa zinafedhehesha na kuchekesha. Utaratibu uliotumika kumpata Shein kama Rais wa Zanzibar hauwezi kubarikiwa na Mungu na wapenda mageuzi.
Dr. Shein anaweza kuongoza nchi katika mazingira ambayo hata yeye atakosa amani moyoni na mwisho wa siku wanafiki ambao wanashindwa kumshauri vema laana inaweza isiwangukie.
Ewe Dr. Shein achana na siasa za upambe tulia , fikiri na tumia taaluma na busara yako kukaa na mpinzani wako wa karibu Malim Self mtafutie Zanzibar na Wanzanzibar mustakhabali mwema wa nchi yenye amani na utulivu wa mioyo yao.
 
Siasa za ccm wakati mwingine huwa zinafedhehesha na kuchekesha. Utaratibu uliotumika kumpata Shein kama Rais wa Zanzibar hauwezi kubarikiwa na Mungu na wapenda mageuzi.
Dr. Shein anaweza kuongoza nchi katika mazingira ambayo hata yeye atakosa amani moyoni na mwisho wa siku wanafiki ambao wanashindwa kumshauri vema laana inaweza isiwangukie.
Ewe Dr. Shein achana na siasa za upambe tulia , fikiri na tumia taaluma na busara yako kukaa na mpinzani wako wa karibu Malim Self mtafutie Zanzibar na Wanzanzibar mustakhabali mwema wa nchi yenye amani na utulivu wa mioyo yao.

Kwanza Ana Hofu wala haiwezi kumuondokea kwenye nafsi, kitu cha kuiba huwezi kujitanua nacho.Na Ndio maana unakuta mpk Leo Zanzibar kumejaa majeshi kila sehemu.
 
Itakua ni hutba ya kujipa moyo na kulazimisha mambo .katiba znz ilishawekwa pembeni .sasa ni maguvu tu
 
vya
Au ndo tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja?

unauliza majibu! zanzibar upinzani ulishajifia...wananchi hawataki USULTANI..... Bara CHADOMO kimekuwa umoja kamili wa mafisadi..... bora tubaki kuwa KIJANI tutasonga mbele kupita hivi vikundi vya msimu visivyokuwa na adress!
 
Back
Top Bottom