Rais Samia weka mkazo kwenye Kilimo

Yaani post yako umeiandika kisiasa halafu unasema tuweke siasa kando?
Mkazo kwa hali hii ya ukame na mafuriko?

Kilimo haliwezi kuipaisha nchi

Screenshot_20211028-112058.png
 
Hili kwakweli halikubaliki hata kidogo.Ndio maana vijana tunakimbilia mijini na kukidharau kilimo kuona kama hakina tija mana MTU unatumia nguvu nyingi,mtaji mkubwa na unachokuja kukipata hakiendani na uhalisia wa gharama ulizozitumia.
Vijana kukimbilia mijini sio kuwa wanapenda sana Bali ni walau kutafuta unafuu wa maisha.Huwezi kuwafukuza Machinga halafu hujawawekea mpango mbadala wa kuwafanya waendelee kufanya shughuli zao.Serikali ikitaka kuwaondoa bila bughdha waboreshe Kilimo kwa ujumla wake waone kama kuna watu watabaki mjini.
Kwenye kilimo hatamataifa ya nje hawapendi kutuona tukipiga hatua hasa kwa kuwekeza nguvu kwa vijana na watu wa chini ambao ni wengi sana na ukiwekeza kwa hao kikamilifu nchi itakua na maendeleo sana. Wahisani pia wanapenda kuona tuna shida za Covid, TB, ukimwi malaria nk hapo wanatoa support faster
 
Back
Top Bottom