Rais Samia: Waziri wa Nishati aliondoa Tozo kwenye mafuta kimakosa kwa sababu Tozo ilipitishwa na bunge, Nimeirejesha!

Mama anasema Waziri wa fedha aliondoa Tsh 100 kwenye bei ya mafuta lakini akairudisha kwasababu moja ilikuwa imeshapitishwa kwenye bajeti na pili isingeleta unafuu wowote kwa walaji katika kipindi hiki cha mfumuko...
Usisahau, mara nyingi serikali imekuwa inavunja katiba (japo wana apa kwa mbwembwe kuwa watailinda) na kudai ilifanya hivyo kwa nia njema. Mara kadhaa imeshuhudiwa ongezeko la kodi au tozo baada ya budget. Hakuna Mbunge anae hoji maamuzi kama hayo, na wajinga tukisema bunge halina meno tunazomewa.
 
Mama anasema Waziri wa fedha aliondoa Tsh 100 kwenye bei ya mafuta lakini akairudisha kwasababu moja ilikuwa imeshapitishwa kwenye bajeti na pili isingeleta unafuu wowote kwa walaji katika kipindi hiki cha mfumuko.

Swali langu kwanini Waziri aliamua kuondoa hiyo tsh 100 wakati Bunge lilikuwa limeshapitisha? Je alitaka kumchonganisha Rais na Bunge? Alilidharau Bunge? Alipitiwa? Ana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria? Au ndio yale mambo ya watu watatu kukaa na kuamua kukopa au kubadilisha matumizi ya mkopo kwa niaba ya Taifa?
Labda nikuulize kitu, kwani Samia akiirudisha ndio yupo sahihi?
 
Hata yule Kigogo kule twitani hakuliona hili.

Hii sasa imekuwa nchi ya comedy.

Baada ya bunge kuwa la ovyo (la mazuzu - by prof Assad), watu wasio na dhamana yoyote wanalalamikiwa kutoikosoa au kutoisimamia serikali? Lissu, Zitto, Maria, Kigogo …? Who the heck are these?

Wapinzani waliosukumiwa nje na kufanyiwa kila aina ya dhihaka; all dissenters wanaoitwa wasaliti kila siku ndio wahoji serikali ikifanya ujinga? Bunge la CCM lifanye kazi gani? Kukinga mafao tu na kumtukuza Rais? Wamekuwa makerubi na maserafi?

Acha Watanzania waendelee kupigika na ufalme wa milele wa magenge ya CCM hadi ule uamsho mkuu utakapotimia - karne ijayo.
 
Mie simshangai Mwigulu…nashangaa Wabunge na Wanasiasa hasa wa Upinzani pamoja na vyombo vya habari vilivyopiga kimya uvunjifu huu wa sheria

Spika msomi kuliko wote waliowahi kutokea Ndugu Tulia nae alitulia…mchambuzi wa kujitegemea wa Uchumi na Bajeti Ndugu Zitto nae kimya…mwanasheria Nguli Antipas Lissu nae Kimya…Jf nako tukapiga kimya!

Hadi kina Fatma Karume na Maria Sarungi nao kimya

Tuliandika humu kuwa tutalipia gharama ya kumzodoa Ndugai…na ndio hii… watu wanakosea hadi wanagundua wenyewe wanajirekebisha sie tupo kimyaaa tu kwa kuwa tunaogopa mashambulizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu toka Njombe kwa mikwala


Zogo la Katiba mpya limeanzishwa upya ili kuficha mengi sana maana sote tuko busy kwny hili… nawakumbusha …Escrow ilipigwa wakati tupo busy na Heka heka za Rasimu ya Warioba

Tume ingeundwa kuchunguza hili maana sio kawaida kwa ukimya huu
Hao uliowataja wote hawana meno, nashangaa hata wewe hukuthubutu kushusha uzi hapa JF kulaani uvunjwaji wa katiba.
 
Mie nimchangiaji tu wa uzi…sijawahi kuanzisha uzi…sina utaratibu huo
Kuwa na utaratibu huo sio dhambi mkuu. Kabla hujawalaumu hao wadau angalau ungeonesha ulichokifanya wewe. Nchi ya kqetu sote hii tusitegemee kuvushwa na mtu, kila mmoja anayakiwa kufanya anachoweza kufanya ili kujenga.
 
Nami nimejilaumu kupitia kundi la wana JF nliposema hata sie Jf tulipiga kimya
Kuwa na utaratibu huo sio dhambi mkuu. Kabla hujawalaumu hao wadau angalau ungeonesha ulichokifanya wewe. Nchi ya kqetu sote hii tusitegemee kuvushwa na mtu, kila mmoja anayakiwa kufanya anachoweza kufanya ili kujenga.
 
Wataalam wa masuala ya uchumi tusaidieni, crisis ya mafuta imefanyiwa kwa Mbinu tofauti Kati ya Kenya na Tanzania, wakati Mhe. Samia akirejesha tozo na kushoot Bei ya mafuta Kwa shs mia Kwa Kila Lita wenzetu Kenya Mhe. Rais amesain fedha dharua kudhibiti tatizo la mafuta linaloikumba nchi Hii


Hizi ni nchi mbili ambazo zinaagiza mafuta kwenye soko Moja; Kenya Bei ipo chini na Mhe. Rais anatenga Fe kuhakikisha anaziba deficit inayojitokeza, Tanzania tunaongeza tozo kwa maelezo kwamba zilipitishwa kwenye bajeti.

Kati ya wizara ya fedha Tanzania na Kenya Nani amexhukua approach sahihi? Tujadiliane
 
Sa anawaaminia hao wahuni wake , alaf anamuona jiwe kana kwamba alikuwa Fala Sana , wait and see
 
Kenya ina hela ya kununua mafuta kwa bei ya juu na kuyauza kwa hasara ili kuwasaidia watu wao. Tanzania imefilisika baada ya miaka 60 ya sera za Ujamaa na Kujitegemea. Tunaishi kwa mikopo na misaada. Siku tukinyimwa hii nchi itavurugika.
 
Rais Samia amesema waziri wa Nishati January Makamba alifuta tozo ya tsh 100 kwenye mafuta kwa nia njema ya kupunguza bei lakini ikaonekana kuna utaratibu haukuwa sawa.

Tozo ile ilipitishwa na bunge siyo waziri hivyo kuifuta kulitakiwa kuanzie bungeni.

Rais ameirejesha tozo ya mafuta kama awali

Source: TBC.
Lady Hangaya katika ubora wake, acha aendelee kuupiga mwingi.
 
Itakuwa Zitto na January walijiamulia tu kufuta tozo kwa sababu ya kujiandaa na urais!
Kwenye Urais ondoa Neno Zitto laubda ulitaka kusema rahisi.Yaani labda Zito anajiandaa na Urahisi wa maisha sio Urais.

Unategemea nini kumwona Kijana Msomi aliyeingia kwenye siasa za upinzani halafu akawa na siasa na hulka zile zile za CCM? Hafai mana Hana tofauti na walioko CCM Kwa unafiki ,ubinafsi,kujipendekeza ,usaliti na kigeugeu
 
Watetezi wake watakuja kusema anahujumiwa ........haki ya Mungu huyu mtu akipita kwenye uchaguz 2025 ntajua watz tumelogwa

Hajapata kutokea raisi mweupe kichwan kiasi hiki
Katiba ya Tanzania ndiyo inayomfanya asiwe na uwezo ila ni Kiongozi mzuri sana.
Akiwa na katiba yenye mifumo inayojiendesha Kikatiba Hakika Watanzania watakua wamepata Rais Bora. Ila chini ya Katiba hii ya Sasa ataharibu sana kufikia 2025.
 
Back
Top Bottom