Rais Samia: Watendaji acheni urasimu msiwasumbue Wawekezaji kwa sababu wana majina ya kiswahili, Ramadhani ametutoa kimasomaso!

Rais Samia amewapongeza wamiliki wa kiwanda cha RADDY Fiber ambao ni Watanzania wazawa kwa uwekezaji mkubwa walioufanya na kuitoa Tanzania kimasomaso.

Kiwanda cha Raddy Fiber ni miongoni mwa viwanda vinne pekee barani Afrika vinavyotengeneza mikonge.

Rais Samia amewataka watendaji kuacha kuwasumbua wawekezaji wazalendo kwa kuangalia majina yao kwa mfano huyu Ramadhani Hassan wa RADDY Fiber bali muwakumbatie.

Source: Clouds tv!
Wewe mnyalukolo unavyopiga debe, ukiambiwa teuzi wanapewa kina Sikinde, tumbili na mnywa bia hodari, bila kumsahau njaakili jua
 
Ni kweli kabisa jamaa wametutoa kimasomaso. Nchi nyingine tatu za Afrika zenye viwanda kama hiki ni Misri, Algeria na Afrika Kusini. Tanzania ya Viwanda inakuja kwa kasi. Tuchape kazi kwa bidii ndugu Watanzania!!
Mikonga ndiyo nini?
 
Hapana, sikumaanisha hivyo, nilimaanisha kwamba Bwawa la Nyerere wakilimaliza litaingiza > 2 000 MW kwenye Gridi ya Taifa, na kwa kuwa Umeme wa maji ni rahisi sana kulinganisha na vyanzo vingine bei ya umeme itashuka sana na hivyo kusaidia wazalishaji kwani kama umeme ukiwa rahisi wanaweza kuzalisha bidhaa kwa bei ya chini na hivyo kuweza kushindana ndicho nilichomaanisha .
Tatizo hii nchi tunakuwa Kama tuna laana, unaweza kuta bwawa linakamilika harafu mvua hainyeshi,maji hakuna ya kutosha
 
Nahisi hayo majina ya KIswahili umeyachukulia kama vile Juma, Ramadhani, Abdul, Hamisi, n.k wakati nilivyomwelewa mimi, hata Jackson Kinyungu nalo ni jina la Kiswahili tu kwa muktadha aliokusudia!!! Na ukitaka kumwelewa, nenda wewe ambae tua-assume unaitwa Jackson Kinyungu Mbena wa Malinyi, na Abdulkadir Majid kutoka Qatar kisha angalia nani atapewa attention kati yako mwenye jina la Kizungu na Abdulkadir mwenye jina la "Kiswahili"!!
Mkuu,kunywa soda nakuja kulipa...
 
Tatizo hii nchi tunakuwa Kama tuna laana, unaweza kuta bwawa linakamilika harafu mvua hainyeshi,maji hakuna ya kutosha

Bwawa lina namna yake ya kujengwa kukabiliana na matatizo kama hayo, kumbuka Tanzania haijawahi kuwa na ukame 100% kilichopo ni uzembe tu, mvua ikichelewa mwezi au miezi ndicho tunachokiita ukame, lkn mvua huja miaka yote labda siyo kwa wakati tunaotaka au tuliotegemea lkn huja ni lazima!
 
Mfumo dume unaisumbua akili yako.
Mfumo dume ndiyo unaendesha dunia. Hakuna nchi duniani imewahikuongozwa na mwanamke ikatoboa. Haipo tangu kuumbwa dunia. Kama ipo itaje

Marekani ina miaka zaidi ya 220+ lakini haijawahi kuongozwa na mwanamke. Unadhani hakuna wanawake wenye kuweza kuongoza huko Marekani?
 
Wewe mtoto mdogo sana hujui dunia inayoisema.

Magret Thatcher aliongoza miaka mingi pale Uingereza labda ulikuwa bado upo kiunoni mwa mzee wako.

Angela Merkel kaiongoza kwa mafanikio Ujerumani tena kwa miaka zaidi ya kumi.

New Zealand waziri mkuu kaiongoza nchi vizuri sana wakati wa covid19.

Wanaume wengi wamejaa viburi na unyama usio na sababu. Wivu na uonevu ni sifa yao siku zote.
 
Hao uliowataja waliongoza nchi zao zikiwa za uchumi wa chini wa kati kama wetu?
 
Back
Top Bottom