JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,457
Inadaiwa kuwa huu mchongo unawahusisha vigogo wa kwenye mamlaka za juu na ndiyo maana kuna danadana zinaendelea.
Taarifa za uhakika kutoka wa watu ambao wamekuwa sehemu ya waathirika wa mradi huo kwa ardhi yao kutaka kuuzwa kwa bei ya chini amedai kuwa wameshafanya vikao vingi lakini hakuna muafaka na hiyo ni kwa kuwa kuna michezo mingi michafu inaendelea nyuma ya pazia.
Inaelezwa kuna wakati walikaa kikao na viongozi wa juu tena baadhi yao ni watauliwa wa Rais Samia kuhusu mgogoro huo, wakapikwa mkwara kuwa hawatakiwi kurekodi kwa kifaa chochote mazungumzo hayo, iwe ni kwa simu au kamera ya kawaida.
Kuna wananchi zaidi ya 2000 katika madai hayo, kati yao wapo wachache ambao wameshapozwa na hivyo wamekubali kuuza kwa bei hiyo ya buku tatu kwa square mita, wakati wenzao wengi wanataka buku nane kwa square mita.
Baada ya kiongozi mmoja mkubwa kufika eneo hilo na kufanya kikao, wakaamua kuunda kamati ndogo ili kushughulika na suala hilo, lakini hao wachache nao wakapewa kazi ya kuwashawishi wenzao ili wakubali kwa kuwa kuna maslahi ya wakubwa.
Najua Serikali ya mama Samia ni sikivu na lazima itadili na hao vigogo wanaotaka kuwanyonya wananchi kwa maslahi yao binafsi ya wachache.