Rais Samia: Wananchi wasichukulie kirahisi mabadiliko ya tabia ya nchi

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
Rais Samia ataka wananchi wasichukulie kirahisi mabadiliko ya tabia ya nchi

The Diplomat

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameshiriki Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliojadili athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoikumba dunia na kusisitiza umuhimu wa kutopuuzia juhudi za kukabiliana na janga hilo, nchini Marekani.

“Tuko katika kipindi ambacho wakati tunapambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi bado tunataabika na changamoto kubwa ya sasa ambayo ni Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO – 19) ambayo imeangusha sana hali ya uchumi na kufuta mafanikio yaliyokwishafikiwa katika miongo kadhaa ya kujenga jamii zetu,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza pia kuwa ingawa watu wengi wanachukulia kirahisi kupanda kwa hali ya joto kama moja ya athari za mabadiliko ya tabia nchi, bado hali ni ya kusikitisha kwa nchi kama Tanzania kwani hali hiyo husababisha ukame ambao ni athari mbaya kwa sekta zinazotegemea maliasili kama vile kilimo, uvuvi na misitu ambazo zinachangia 30% ya pato la Taifa na kuathiri takribani 60% ya wananchi.

Mkutano huo ambao ni mfululizo wa mikutano ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 26 wa athari za mabadiliko ya Tabia Nchi (COP26) utakaofanyika Glasgow, Uskochi mnamo mwezi Novemba, 2021, umejadili hatua za upatikanaji fedha kwa ajili ya kugharamia ustahimilivu na upunguzaji wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati huo huo, Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Comoro, Azali Asoumani na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Rebecca Nyandeng Garang. Viongozi hao wamezungumzia kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na mataifa hayo.

Rais Samia ameelekeza kufanyika haraka kwa mikutano ya tume za kudumu za ushirikiano baina ya mataifa hayo ili kuangalia namna ya kuboresha zaidi mahusiano.

Aidha, Rais Samia amefanya mazungumzo na Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na shirika hilo hususani katika kusaidia wakimbizi walioko nchini Tanzania.

Filippo Grandi ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kubeba mzigo mkubwa wa wakimbizi kwa takribani
miongo sita sasa ambapo pia amependekeza kuwepo na mkutano katika ngazi ya wataalam baina ya UNHCR, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Mambo ya Nje ili kuondoa changamoto katika kuwahudumia wakimbizi.

Rais Samia ameelekeza kikao hicho kufanyika mara moja ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.

#TanzaniaKimataifa
#ZiaraYaRaisUSA

IMG-20210921-WA0150.jpg
IMG-20210921-WA0149.jpg
IMG-20210921-WA0148.jpg
IMG-20210921-WA0018.jpg
 
Suala la Mabadiliko Ya Tabia nchi ni mtambuka bahati mbaya watu hawalioni kwa Uzito huo..Hasa Hapa Afrika..Wakati ambao unaweza kusikia habari za Kuogofya sana Kwamba Kuna Sehemu Kama Kilifi, Mandera na Garissa Kule Kenya Zina Miaka miwili bila tone la Mvua unatakiwa utafakari sana.
.KWANINI Mvua Haijanyesha na Kwanini Pia Ikinyesha Inakua Nyingi zaidi...

Kwa Tanzania Nadhani Ingeundwa Idara kabisa Ya Kushugulikia Haya mambo sio kuyachukua Kijumla jumla..

KULINDA SANA KWA wivu mkubwa vyanzo vya maji tulivyonavyo...Kulinda sana Misitu ya asili inayoteketea kwa kasi ya ajabu....Kupanga Namna ya kupata Nishati...Ili tuhame kwenye Wood fuel (Mkaa)

Au kama basi tunatumia mkaa uwe ambao sio kutoka kwenye miti ya asili.

HILI JANGA ni hakika litatusumbua na Afrika tutaumia zaidi maana hatuna uwezo na nyenzo za kupambana nalo...Ni Jinamizi kubwa..Fikiria Maji kukauka...Fikiria Dunia isiyo na Malisho ya mifugo...Kuna balaa kubwa.

Nilitegema Idara Maalumu iwepo ama Pale Nemc au Ofisi ya Rais Kabisa Kwa uzito wa jambo hili Idara hiyo iwe na mamlaka ya kusimamia Halmashauri zote katika eneo la kimkakati la kupambana na Mabadiliko ya Tabia nchi.

Kwenye Ziara ya Rais Hii nilitegemew Watu wa Nemc wangekuepo aidha Mkuu wa Nemc au wabobezi wengine..Sijawaona pale labda ni kwasababu maalumu.
 
Suala la Mabadiliko Ya Tabia nchi ni mtambuka bahati mbaya watu hawalioni kwa Uzito huo..Hasa Hapa Afrika..Wakati ambao unaweza kusikia habari za Kuogofya sana Kwamba Kuna Sehemu Kama Kilifi, Mandera na Garissa Kule Kenya Zina Miaka miwili bila tone la Mvua unatakiwa utafakari sana.
.KWANINI Mvua Haijanyesha na Kwanini Pia Ikinyesha Inakua Nyingi zaidi.....
Wananchi wanajitahidi kuondokana na adha ya kutumia mkaa na kuhamia kwenye gesi lakini selikali nayo haiko nyuma ikiona hivyo inapandisha bei ya gesi, sasa unategemea watu wataachaje kutumia kuni na mkaa?

Nashukuru Magufuli alianzisha mpango wa nguzo za umeme ziwe za zege ili tuachane na hizi za miti, kama mafisadi walioanza kurudi kwa kasi hawataingilia hili kwa maslahi yao, hii hatua ya kuachana na nguzo za miti ni nzuri sana pia. Lakini pia hii nishati ya umeme inatakiwa iwe bei chini ili raia akitaka kutumia jiko la umeme badala ya mkaa au kuni gaharama zisiwe kubwa.

Watu siyo kwamba wanapenda kutumia mikaa na kuni hapana ila nishati mbadala ni ghali sana,
 
The Diplomat

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameshiriki Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliojadili athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoikumba dunia na kusisitiza umuhimu wa kutopuuzia juhudi za kukabiliana na janga hilo, nchini Marekani.

“Tuko katika kipindi ambacho wakati tunapambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi bado tunataabika na changamoto kubwa ya sasa ambayo ni Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO – 19) ambayo imeangusha sana hali ya uchumi na kufuta mafanikio yaliyokwishafikiwa katika miongo kadhaa ya kujenga jamii zetu,” amesema Rais Samia.

Amesisitiza pia kuwa ingawa watu wengi wanachukulia kirahisi kupanda kwa hali ya joto kama moja ya athari za mabadiliko ya tabia nchi, bado hali ni ya kusikitisha kwa nchi kama Tanzania kwani hali hiyo husababisha ukame ambao ni athari mbaya kwa sekta zinazotegemea maliasili kama vile kilimo, uvuvi na misitu ambazo zinachangia 30% ya pato la Taifa na kuathiri takribani 60% ya wananchi.

Mkutano huo ambao ni mfululizo wa mikutano ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 26 wa athari za mabadiliko ya Tabia Nchi (COP26) utakaofanyika Glasgow, Uskochi mnamo mwezi Novemba, 2021, umejadili hatua za upatikanaji fedha kwa ajili ya kugharamia ustahimilivu na upunguzaji wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati huo huo, Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Comoro, Azali Asoumani na Makamu wa Rais wa Sudan Kusini, Rebecca Nyandeng Garang. Viongozi hao wamezungumzia kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na mataifa hayo.

Rais Samia ameelekeza kufanyika haraka kwa mikutano ya tume za kudumu za ushirikiano baina ya mataifa hayo ili kuangalia namna ya kuboresha zaidi mahusiano.

Aidha, Rais Samia amefanya mazungumzo na Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ambapo viongozi hao wamezungumzia kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na shirika hilo hususani katika kusaidia wakimbizi walioko nchini Tanzania.

Filippo Grandi ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kubeba mzigo mkubwa wa wakimbizi kwa takribani
L miongo sita sasa ambapo pia amependekeza kuwepo na mkutano katika ngazi ya wataalam baina ya UNHCR, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Mambo ya Nje ili kuondoa changamoto katika kuwahudumia wakimbizi.

Rais Samia ameelekeza kikao hicho kufanyika mara moja ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.

#TanzaniaKimataifa
#ZiaraYaRaisUSA
 
Suala la Mabadiliko Ya Tabia nchi ni mtambuka bahati mbaya watu hawalioni kwa Uzito huo..Hasa Hapa Afrika..Wakati ambao unaweza kusikia habari za Kuogofya sana Kwamba Kuna Sehemu Kama Kilifi, Mandera na Garissa Kule Kenya Zina Miaka miwili bila tone la Mvua unatakiwa utafakari sana.
.KWANINI Mvua Haijanyesha na Kwanini Pia Ikinyesha Inakua Nyingi zaidi.
like yangu mkuu
 
Ni kweli bei ya nishati za umeme na gesi bado sio rafiki ili kumuwezesha kila mwananchi hasa yule alioko kijijini kuweza kuimudu...
 
Wananchi wanajitahidi kuondokana na adha ya kutumia mkaa na kuhamia kwenye gesi lakini selikali nayo haiko nyuma ikiona hivyo inapandisha bei ya gesi, sasa unategemea watu wataachaje kutumia kuni na mkaa?.....
Tatizo la nchi hii ni CCM.
 
Mwanamke kua na mapete mawili kushoto na kulia msichukulie kirahisi.
Ohooo
 
Back
Top Bottom