Rais Samia, wananchi tuna haki ya kujua kilichomo kwenye ripoti uliyoiunda kuchunguza pesa za BoT

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,486
51,063
Ndugu Rais,

Ukifunika ripoti hii unatupa wasiwasi sisi wananchi kuwa unalinda upigaji na ufisadi, na hili litakuandama kisiasa kwa muda mrefu sana.

Ndugu Rais, uchunguzi wa hizi pesa uliuagiza hadharani, wananchi tukishuhudia, tukisikia, na kwa hiyo tuna haki ya kujua je pesa zetu ziko salama au la!, kama zilitumika zilitumika kwa kufuata misingi ya sheria? Maadamu uliagiza uchunguzi wa suala hili hadharani, wananchi tunataka kujua yaliyojiri katika hili suala, kinyume cha hapo ni kulindanalindana tu ambako sisi wananchi hatutaki.

Ndugu Rais, hizi pesa ni mali yetu wananchi, ni kodi zetu, kama ni za mkopo basi tutalipa sisi na pengine watoto wetu, kwa hiyo tunaomba hiyo ripoti iwekwe wazi tujue kinachojiri katika hizo pesa.

Ndugu Rais, Uliunda tume ya ushauri juu ya masuala ya korona na ndani ya miezi miwili tu imekupa majibu na imetoa mrejesho wa mapendekezo yake hadharani, Sasa hiki kigugumizi kuhusu ripoti ya PESA zetu cha nini?

Ndugu Rais, tunaomba utupe imani kuwa Unapambana na Ufisadi kwa Vitendo, Unapambana na Ubadhirifu wa pesa ya umma kwa Vitendo na ili uweze kutupa imani hiyo TUNATAKA RIPOTI YA MIAMALA YA FEDHA ZETU KUANZIA Mwezi January hadi March Mwaka huu tuione na tujue kiluchojiri, Kinyume cha hapo sisi tutajua unachofanya ni kulindana tu kwenye mambo ya Upigaji.
 
Wengine haya tuliyajua mapema tu kwani wahusika/watuhumiwa wanajulikana.

Hii nchi itasafishwa siku chama tofauti na CCM kitaposhika uongozi wa hii nchi ila kwa sasa mtaeendelea kushuhudia unafiki na doublestandard katika ku- deal na issue za aina hii.

Inawezekana alizokwapua Sabaya kutoka kwa watu wanaomtuhumu ni tone tu ya kile kilichokwapuliwa huko BOT.
 
Tutaendelea kukumbusha tu Mh Rais Samia Suluhu Hassan wala hatutachoka. Tunaomba ripoti hii iwekwe bayana kama ulivyowahi kuagiza.



Usiruhusu jambo hili likutie doa...kama ulivyoagiza hadharani, itoe hadharani.
 
Mwisho wa siku CCM lazima walindane, isomwe au isisomwe, nachotaka sio isomwe wahalifu wajulikane halafu kesi iishie hapo, nataka wapelekwe mbele ya vyomno vya sheria haki itendeke, na kama kuna viongozi waliohusika kwenye hii serikali mpya ndio kabisa hiyo ripoti haitakaa isomwe.
 
Ndugu Rais,

Ukifunika ripoti hii unatupa wasiwasi sisi wananchi kuwa unalinda upigaji na ufisadi, na hili litakuandama kisiasa kwa muda mrefu sana.

Ndugu Rais, uchunguzi wa hizi pesa uliuagiza hadharani, wananchi tukishuhudia, tukisikia, na kwa hiyo tuna haki ya kujua je pesa zetu zilo salama, kama zilitumika zilitumika kwa kufuata misingi ya sheria? Maadamu uliiunda uliagiza uchunguzi wa suala hili hadharani, wananchi tunataka kujua yaliyojiri katika hili suala, kinyime cha hapo ni kulindanalindana tu ambako sisi wananchi hatutaki.

Ndugu Rais, hizi pesa ni mali yetu wananchi, ni kodi zetu, kama ni za mkopo basi tutalipa sisi na pengine watoto wetu, kwa hiyo tunaomba hiyo ripoti iwekwe wazi tujue kinachojiri katika hizo pesa.

Ndugu Rais, Uliunda tume ya ushauri juu ya masuala ya korona na ndani ya miezi miwili tu imekupa majibu na imetoa mrejesho wa mapendekezo yake hadharani, Sasa hiki kigugumizi kuhusu ripoti ya PESA zetu cha nini?

Ndugu Rais, tunaomba utupe imani kuwa Unapambana na Ufisadi kwa Vitendo, Unapambana na Ubadhirifu wa pesa ya umma kwa Vitendo na ili uweze kutupa imani hiyo TUNATAKA RIPOTI YA MIAMALA YA FEDHA ZETU KUANZIA Mwezi January hadi March Mwaka huu tuione na tujue kiluchojiri, Kinyume cha hapo sisj tutajua ni Kulindana tu kwenye mambo ya Upigaji.
Yumo Ntibazonkiza. Case closed.
 
Au majamaa yameirudisha kimya kimya na kuombana msamaha kimya kimya?
Hata zikirudishwa kwa siri, kama ni siri unadhani zitarudi zilipokuwepo hapo awali? Kwasababu ni siri, hakuna atakayeuliza. Ndiyo maana ninaamini wanaweza wakawa wamegawana.
 
Hata Yesu Alituagiza kwa Ukali


MT. 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
 
Rais amekuwa aakiunda tume lakini matokeo yake hayatolewi kwenye umma.

Hii inaweza fanya loop hole ya Kulindana hasa akiguswa mtu wake wa karibu.

Tume ya COVID nayo ilileta mapendekezo lakini hatukuona maamuzi ya Rais. Kisha tunasikia waziri wa fedha anatakamka mkopo wa Trn 1.3.
 
Wapo wachangiaji watapiga kimya kama vile hawaioni hii mada, wapo watakaojaribu kutuhamisha kwenye mada na wapo watakaotetea wakidai Mh. SSH hulazimiki kuitoa hiyo ripoti hadharani.

Naomba nikutahadharishe Mh Rais kwamba ahadi ni deni. Njia pekee itakayokulindia heshima yako ni moja tu…itoe kwa njia ili ile uliyotumia kutoa agizo la uchunguzi kufanyika na ripoti kutolewa.

Wengine tungependa na tunajitahidi sana kukupa kinachoitwa benefit of doubt kwamba uko imara, huyumbishwi hovyo wala hukurupuki, tafadhali usituangushe…timiza kwa matendo.
 
Watakuwa wameamuwa kugawana na kuja kuzitumia kwenye uchaguzi. Mama ataweka doa kubwa sana akiacha huu ufisadi uliotokea ufunikwe. Ndiyo shida ya ccm hiyo.
Zitatumika kuwahonga Wajumbe huko CCM ili mipango yao ya kumng'oa Mama ikamilike
 
Back
Top Bottom