Rais Samia, Wananchi hatutaki madalali wa kisiasa kuingilia ujenzi wa reli ya SGR, tunataka plan ya Hayati Magufuli iheshimiwe kwenye SGR

Huyo Chige ni kati ya watu waliokuja ghafla kutetea mradi wa wachina wa bandari ya Bagamoyo muda mfupi baada ya Magufuli kufa. Ana maslahi flani na hao wazalendo waliotajwa. Kwenye thread ile nilimuambia "watanzania hawajasahau ...."
Mwangalieni huyu!!

FYI, nimeanza kuzungumzia mradi wa Bandari ya Bagamoyo tangu JPM akiwa hai kwahiyo ni kiroja kusema eti mimi ni kati ya watu "waliokuja ghafla" kutetea mradi muda mfupi mbaada ya JPM kufa!!
Hivyo nilitegemea atakuja kwa kasi kutetea upigaji huo unaotaka kufanywa kwenye SGR.
Ilikuwa lazima afanye hivyo sababu makala ya gazeti la Jamhuri imeponda uhuni wa mradi wa bandari ya Bagamoyo kwa kuwahusisha wapigaji hao wanaojiita wazalendo.
Hivi unaonaje ungejadili hoja niliyoweka badala ya kunijadili mimi? Are you this low?!!

Unaonaje ukianza na hoja ya wapi mmepata figure ya 14.2 Billion/kilometer wakati mamlaka zilisema 2560km zingejengwa kwa USD7.6 Billion>

Tuanze hapo kwanza....
 
Nyie watu ndo maana mnadanganywa kirahisi sana kwa sababu ni wakurupukaji!! Kwavile umetumia magazeti kama source yako, ngoja nikukumbushe ambacho kiliwahii kuandikwa hapo nyuma:-

Hapo juu, ni habari ya mwaka May 2015 kutoka Reuters. Habari kama hiyo ilichapishwa na Gazeti la Mwananchi November 2015 ambapo lilitujuza:-

Utaona hapo ingawaje zilizochapwa na vyombo viwili tofauti kwa nyakati tofauti, lakini wote wanasema umbali wa 2560km kwa $7.6 Billion ambayo ni sawa na TZS 16 Trillion by the time.

Sasa chukua hiyo TZS 16 trillion au hata TZS 17 Trillion na gawanya kwa 2560 km ambapo utapata less than 7 billion per kilometer!! Sasa wewe hizo 14 Billion sijui mmezitoa wapi!!

Mbaya zaidi, Shirika la Reli wenyewe wanasema:-
View attachment 1948857

Wanatuambia Dar to Makutupora wamejenga kwa 7.1 Trillion! Je, ni umbali gani huo? Wenyewe hawa hapa tena:-

View attachment 1948855

Utaona hapo kipande cha Dar to Makutupora ni 722km, na kimejengwa kwa 9.8 billion per kilometer!!!

Na kwa nyongeza tu, hapo kabla mpango ilikuwa ni kujenga Mtandao wa Reli and not just SGR from Dar to Kigali.

Hizo figures ulizoweka ambazo hata hivyo hazieleweki inawezekana mwandishi kachanganya madesa kati SGR from Dar es salaam to KIgali vs Railway Network!!

Tafuta makarabrasha ya mpango wa ujenzi wa MTANDAO wa reli nchini, ndipo utagundua Mtandao wa Reli ni total ya SGR plus matawi yake ndo hayo gharama zake zilikuwa $9 Billion.

Moja ya matawi maarufu yanayoweza kukumbukwa na kila mmoja ni lile ambalo lilikusudia kuunganisha Bandari ya Bagamoyo na Central Railway inayoenda Kigali.

Tawi lingine ni lile ambalo lilikuwa liende Mchuchuma!

Lakini kama ni SGR ya kutoka Dar to Kigali, tenda ambayo ilitolewa ilikuwa $7.6 Billion, na kwa hesabu za wakati ule ilikuwa ni takribani Sh 17 Triilion.

Hapo ndipo narudia, kwavile tunachukulia gharama ni flat rate, chukua basi hiyo Sh 17 trillion kisha gawanya kwa 2560km, ambayo kama average ya gharama itakuwa kama hii iliyopo sasa, it means itakuwa more expensive ukilinganisha na ile mnayodanganya watu kwamba tulipigwa!!
Mnapenda sana kujitetea, but we know what was there by then, hatudanganyiki...The history betrays you...Kwa mara nyingine tena neno ufisasi limerudi kwenye midomo ya watanzania, ask yourself why?
 
Mwangalieni huyu!!

FYI, nimeanza kuzungumzia mradi wa Bandari ya Bagamoyo tangu JPM akiwa hai kwahiyo ni kiroja kusema eti mimi ni kati ya watu "waliokuja ghafla" kutetea mradi muda mfupi mbaada ya JPM kufa!!

Hivi unaonaje ungejadili hoja niliyoweka badala ya kunijadili mimi? Are you this low?!!

Unaonaje ukianza na hoja ya wapi mmepata figure ya 14.2 Billion/kilometer wakati mamlaka zilisema 2560km zingejengwa kwa USD7.6 Billion>

Tuanze hapo kwanza....
Acheni hizo, we know you better!
 
Ji
Acha propaganda za kitoto kutaka kumchafua Rais..

Wewe kwa akili yako unaamini huu upuuzi? Inawezekana vipi gharama inajulikana afu eti ije kuwa kubwa kuliko ya awali kwa ajili ya nini hasa?

Sio kila kinachoandikwa gazetini ni sahihi maandishi mengine ni ya kuuzia gazeti..

Bei haikupangwa na Magu bali ilisimamiwa na wataalamu wa ndani ambao bado wapo .
Jinga kabisa wewe, unajifanya huijui tanzania?
Ni mala ngapi miladi inabadilika bei tofauti za mikataba ya kwanza,
Sema kama na wewe.unataka kupata hilo gawio.
Bila magufuli kukataa hizo ghalama si ungejengwa wakati hao wataalamu unaowasema waliupisha mwanzo?
 
Japo alikuwa na mabaya mengi zaidi ikiwemo vikundi vya watu wasiojulikana, lakini yale mazuri yake tunataka yaheshimiwe
Kosa lake kubwa; plani zake nyingi zilikuwa hazijulikani kwa yeyote. Hakutaka kutumia taratibu zilizowekwa na Bunge kuendesha nchi!
Kwa kuwa alikuwa muovu alihisi watu wengine nao walikuwa waovu maradufu!
Ukiwa kiongozi elewesha watu kwa Uwazi wajue nini kinafanyikaje ili uondokapo mradi usijue umeondoka!
 
Ji

Jinga kabisa wewe, unajifanya huijui tanzania?
Ni mala ngapi miladi inabadilika bei tofauti za mikataba ya kwanza,
Sema kama na wewe.unataka kupata hilo gawio.
Bila magufuli kukataa hizo ghalama si ungejengwa wakati hao wataalamu unaowasema waliupisha mwanzo?
Porojo za kitoto,weka miradi iliyobadilika bei hapa
 
Unapoona polepole anapigwa ubapa, fikiri zaidi!!

Unadhani polepole kaishiwa kiasi hiko?
 
Wala sina haja ya kusikiliza kwa sababu TAYARI NAFAHAMU, unless kama unataka kuniambia maelezo ya JK yanasema alitaka kujenga Meter Gauge na sio Standard Gauge!!!

Tofauti kati ya reli ya JK na ya JPM ni electrification TU lakini zote ni SGR!!!

Man, tumia common sense!!!

JPM alipoingia tu madarakani akaanza ujenzi wa reli!! Endapo JPM angeleta reli tofauti na plan ya JK, feasilibity study LAZIMA ingeanza upya, na kwahiyo ujenzi usingeanza wakati ulioanza kwa sababu feasilibity study ingechukua muda mrefu!!!

Lakini kwavile tangu zamani ilikuwa ni kujenga SGR, hapakuhitajika new feasilibity study cuz' all you need is either to include what's so-called "third rail" or overhead traction system.

Sisi nadhani tuliamua kwenda na overhead traction system
Tofauti ni electrification na Locomotive Speed capacity ambayo hiyo reli inaweza kuaccomodate.

By all standards, SGR ya JPM ni ya viwango vya Juu kuliko aina ya SGR ambayo Kikwete alikuwa anataka.

Kwa hiyo sisi tunakwenda na Hayati kwenye SGR, hatutaki kusikia plan yake ikichezewachezewa
 
Mnapenda sana kujitetea, but we know what was there by then, hatudanganyiki...The history betrays you...Kwa mara nyingine tena neno ufisasi limerudi kwenye midomo ya watanzania, ask yourself why?
Kama alikuwa msafi kwanini alikataa kukaguliwa, SGR ,bwawa la umeme ,Tanesco n.k yote haya mashirika hayajafanyiwa ukaguzi... halafu mnabaki kusifia tu.
 
Acha propaganda za kitoto kutaka kumchafua Rais..

Wewe kwa akili yako unaamini huu upuuzi? Inawezekana vipi gharama inajulikana afu eti ije kuwa kubwa kuliko ya awali kwa ajili ya nini hasa?

Sio kila kinachoandikwa gazetini ni sahihi maandishi mengine ni ya kuuzia gazeti..

Bei haikupangwa na Magu bali ilisimamiwa na wataalamu wa ndani ambao bado wapo .
Wewe uwezo wako wa kufikili ni mdogo Sana Wala Rais hajachafuliwa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikukubaliana na JPM kwenye mambo mengi ikiwemo Udikteta, Uonevu na Mradi wa Ndege

Lakini namuunga mkono sana kwenye mradi wa Stieglers na SGR

Kwa hiyo Mheshimiwa Rais Taarifa hii ya Gazeti la Jamhuri imetushtua sana wanananchi, na hivyo tunasema hivi hatutaki Madalali wa Kichina kwenye ujenzi wa SGR
--------------------------------------------------------

Mafisadi wajipanga

Jamhuri September 21, 2021 Mafisadi Wajipanga

Ni vigogo wazito serikalini, waanza figisu ujenzi wa reli ya SGR

Washirikiana na wazabuni wa nje kuhujumu ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’

Waanzisha kundi wakijiita wazalendo, latajwa ni fedha mbele

Kenya walipigwa bilioni 18.4 kila kilomita, wailengesha Tanzania

DODOMA
Na Mwandishi Wetu

Sikio la kufa halisikii dawa. Hili ndilo linaloweza kusemwa kutokana na baadhi ya wanasiasa na watendaji serikalini kuanza mpango wa hatari wa kukwamisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR; JAMHURI limebaini.

Mpango huo unaosukwa kwa umakini mkubwa, una malengo mawili. Kwanza, kujipatia fedha kwa njia yoyote ile na pili ni kuihujumu Serikali ya Awamu ya Sita kuonyesha kuwa haiwezi kusimamia ujenzi wa reli kama ilivyokuwa awali.

Hivi karibuni kumekuwapo taarifa inayosambazwa na watu wanaojiita ‘wazalendo’ ikitoa shutuma za kuhusu mchakato wa ununuzi unaoendelea vipande viwili; ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’, wakitaka utumike utaratibu uliokwamisha ujenzi wa reli tangu enzi za uhuru.

Kuna mgogoro mkubwa unapikwa chini kwa chini na baadhi ya wanasiasa na wataalamu wakitaka vipande viwili vya reli vya kutoka Makutupora hadi Tabora (Lot 3) na Makutupora hadi Isaka (Lot 4) zabuni itangazwe tena, waingize kampuni zao.

Tayari kuna kampuni kadhaa kutoka China ambazo zimewasilisha serikalini nia ya kujenga vipande hivyo na bei wanayotaka kutoza hata kabla zabuni haijatangazwa.
Mbaya zaidi, moja ya kampuni zilizoomba mwaka 2015, iliomba kujenga reli yote kwa gharama ya dola milioni 6.2 kwa kila kilomita, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita.

Kwa urefu wa reli unaojengwa wa kilomita 1,063 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, mkandarasi huyu alitaka alipwe dola za Marekani bilioni 6.59, sawa na Sh trilioni 15.2 za Tanzania.

Ukiacha ughali wa gharama, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa mkandarasi huyu na wengine walikuwa na upungufu mkubwa uliomsukuma hayati Rais Dk. John Magufuli kuwakataa.

“Muhimu Watanzania wakajua hili group (kundi) la wanaojiita wazalendo ni kina nani. Kwa kudokeza tu hili ni group la watu ambao wanatetea masilahi binafsi, hasa kwa sababu tayari walishakula huko nyuma na wanataka ‘ku-retire imprest’,” anasema Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na kuongeza:

“Huu ni mlolongo wa matukio. Mwaka 2016 serikali ilipoanza hatua za ujenzi, kampuni pekee iliyojitokeza kuunga mkono serikali ilikuwa Kampuni ya Yapi Merkezi. Katika hatua za awali zilijitokeza kampuni 40, lakini wakati wa kurudisha zabuni kampuni 39 kutoka China zote zilijitoa. Cha kusikitisha hata benki moja ya China iliyokuwa imeahidi kutoa fedha, ilikataa ikitoa sababu zisizokubalika.

“Kwanza, benki hiyo ilisema Tanzania imeamua kujenga reli kufuata ‘standards’ (viwango) za kimataifa, yaani kwa kufuata AREMA Standard. Wao hawakulifurahia hili kwa sababu walitaka kufuata standard za Kichina, ikiwa na maana vitu vyote viwe vya Kichina. Kama kuna mtu haelewi tunachozungumza, waulize majirani zetu Kenya. Walifanyiwa mchezo huu.

“Pili, hawakutaka Tanzania ijenge reli kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kisasa, yaani ‘European Level 2 (digital)’, ambayo ndiyo inayotumiwa duniani kote. Walitaka kutuletea teknolojia ya zamani (analogy) kama ya Kenya.

“Tatu, hawakutaka kutumia upembuzi yakinifu wa kwetu. Walitaka wafanye upembuzi wao mpya, na watwambie wanatujengea kwa bei gani. Walitaka makandarasi wote watoke kwao, ‘consultant’ wa mradi wa kwao, ‘design’ Mchina, ‘insurer’ wao na pengine mwishoni kuwa na masharti ya kuendesha wao kama walivyowafanyia majirani zetu. Na hili halikukubalika, na halikubaliki serikalini Tanzania.

“Nne, hawakupenda kubadilishwa kwa mipango yao ya kushirikiana na mafisadi wachache kufuja fedha za walipa kodi waliopanga kufanya na watu wao ambao ndio wanaohaha kila mahala kuihujumu serikali iliyopo madarakani. Mipango haikuwa yenye heri kwa taifa. Kwanza, reli iliyokuwa ijengwe Tanzania ilikuwa kama ile ya Kenya ambayo ni ‘Second hand railway with old technology’, ambayo duniani haitumiki tena,” anasema mtoa habari wetu.

Mtaalamu huyo anatofautisha reli waliyotaka kujenga makandarasi hao na hii iliyojengwa sasa na Yapi Merkezi kwa kusema: “Kwanza, reli yetu ina uwezo mkubwa sana, kwa maana ya kubeba mzigo mkubwa ekseli 35. Reli nyingi zilizojengwa Afrika zina ekseli 25. Ni reli ambazo haziwezi kuchukua mizigo mizito, hasa kwa mtindo wa ‘double stack’.

“Ukitaka kubadilisha reli ya ekseli 25 kwenda ekseli 35, hii pekee itaongeza bajeti kati ya asilimia 15-17.5 ya jumla ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Pili, reli inayojengwa Tanzania inatumia teknolojia ya kisasa ‘digital’ (European Train Control System Level) ikilinganishwa na analojia inayotembea kasi ya kilomita 80 kwa saa hapo kwa jirani zetu. Kubadilisha mfumo kutoka ‘analogy’ kwenda ‘digital’ unahitaji kutumia asilimia 7 hadi 7.5 ya jumla ya bajeti ya ujenzi wa reli ya kisasa. Na ujue kwamba unapozungumzia teknolojia kwenye reli, unazungumzia mawasiliano (signaling na telecommunications).

“Tatu, reli inayojengwa Tanzania inafanyiwa kitu kinachoitwa ‘continue welding’. Maungio ya reli yamechomelewa kwa teknolojia ya hali ya juu sana. Kubadilisha reli kuipeleka kwenye ‘continue welding’ bajeti inaongezeka kwa asilimia tano ya bajeti ya ujenzi wa reli.

“Nne, reli inayojengwa Tanzania ni ‘electrified line’ (ya umeme). Reli itatumia umeme badala ya dizeli, lakini pia itaweza kupitisha treni za dizeli ukilinganisha na walizotaka kujenga za injini za dizeli pekee.

“Mambo mawili muhimu; kwanza, treni ya umeme ni rahisi mara tatu kuliko treni ya dizeli. Ukitaka kubadilisha treni ya dizeli uweke miundombinu ya umeme inabidi utumie asilimia 25 ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Tano, reli inayoijenga Tanzania ina kasi ya kilomita 160 kwa saa ikilinganishwa na hiyo waliyotaka kutujengea ya kilomita 80 kwa saa waliyojenga Kenya. Kubadilisha kasi ya kilomita 80 kwa saa kwenda kilomita 160 kwa saa, itahitaji kutumia bajeti isiyo chini ya asilimia 15 ya gharama zilizotumika kujenga reli yote,” anasema.

Anaongeza kuwa iwapo Kenya wangependa kujenga reli sawa na ya Tanzania katika hiyo gharama ya dola za Marekani milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita, ilibidi waongeze asilimia 70 ya bei hiyo na kuwa dola milioni 10.5, sawa na Sh bilioni 24.15 kwa kilomita au asilimia 70 ya gharama zote za kujenga reli.

Hii ina maana kuwa Tanzania imejenga reli hii kwa gharama ndogo ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka. Kwa wastani hii reli ya umeme ya ‘Standard Gauge’, Tanzania inajenga kilomita moja kwa dola milioni 4.1, sawa na Sh bilioni 9.43.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa ujenzi wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro; ambacho ni kilomita 300, kwa maana ya kilomita 205 za njia kuu na kilomita 95 za njia ya kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 1.22 ikijumuisha na VAT. Ukigawa kilomita 300 kwa kiasi hicho cha fedha, unapata wastani wa dola milioni 4.07 kwa kila kilomita, ikiwamo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Kipande cha pili cha Morogoro mpaka Makutupora ya Singida chenye urefu wa kilomita 422, zikiwa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishania, kinajengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.924. Ukigawanya kwa kilomita 422 ni sawa na dola milioni 4.6 kwa kilomita moja ikijumuisha VAT.

Ikumbukwe kipande hiki cha reli kimepita milimani kwa zaidi ya kilomita 120, ikiwamo na kuchoronga mahandaki (tunnels) zaidi ya kilomita 2.7.

Kipande cha tano cha Mwanza mpaka Isaka chenye urefu wa kilomita 341 kikiwa ni njia kuu kilomita 249 na kilomita 92 zikiwa njia za kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.33. Ukigawa kwa kilomita 341 inakuwa dola bilioni 3.9 kwa kila kilomita moja, gharama hii ikijumuisha VAT.

“Sasa angalia kituko cha upembuzi yakinifu uliofanywa Novemba 2015 na kampuni inayoomba sasa kujenga vipande vilivyobaki kwa kutumia wanasiasa na wataalamu wachumia tumbo. Hawa walitaka wapewe mradi wote wa reli kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma. Kila kilomita moja walitaka kuijenga kwa dola milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita moja,” anasema mtoa taarifa na kuongeza:

“Na hiyo reli ambayo ingejengwa ni kama ya Kenya. Na kama ingejengwa tukataka ‘ku- upgrade’ ifanane na ya sasa ya kwetu, serikali ingetakiwa kutumia gharama zaidi ya asilimia 70. Maana yake nini? Ukiongeza asilimia 70 ya dola milioni 6.2 kwa kilomita moja, maana yake tungejenga kilomita moja kwa dola milioni 10.5 ili tupate reli ya ‘standard’ inayojengwa na Yapi Merkezi.

“Nini maana ya gharama hizo nilizozitaja? Maana yake ni kuwa gharama inategemea na eneo (terrain) ukipita kwenye milima na kuchoronga mahandaki, gharama ni tofauti na ujenzi wa sehemu nyingine. Hao hao waliotaka kutujengea reli ya kizamani kwa kilomita moja kwa dola milioni 6.2, leo ndio wanaopigiwa debe na wanataka kuwaamanisha Watanzania kuwa ni wazalendo. Walikwisha kusaini mkataba mwaka 2015 ambao Rais Magufuli alisema hautambui,” amesema.

JAMHURI limefahamishwa kuwa nchi nyingi Afrika zimeliwa katika ujenzi wa reli kwa kutumia gharama ya kati ya dola milioni 5.1, sawa na Sh bilioni 11.73 hadi dola milioni 8.0, sawa na Sh bilioni 18.4 kwa kilomita bila asilimia 18 ya VAT.

“Sasa kelele zimeanza wanataka tuwape hawa kazi hii. Sisi tunasema hapana. Tumsaidie Rais Samia [Suluhu Hassan] nchi yetu isiingizwe majaribuni. Utaratibu uliotumika kupata wazabuni kwa ‘Lot 2’ na ‘Lot 5’ ndiyo utumike kupata wa ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’. Kinacholengwa kufanywa hakina masilahi kwa taifa letu,” amesema mtoa habari mwingine.

Duniani ujenzi kama uliofanywa na Tanzania kwa takwimu za mwaka 2015, wastani wa ujenzi wa kilomita moja ya reli ni dola milioni 3.5, sawa na Sh bilioni 8.05 bila kodi ya VAT.
Kwa mabadiliko yaliyotokea ya bei za vifaa ikijumuisha na kupanda kwa bei ya chuma, bei ya mafuta, bei ya saruji na vifaa vingine inakadiriwa sasa kuwa wastani wa kujenga reli ya umeme kilomita moja inagharimu dola milioni 4.0, sawa na Sh bilioni 9.2.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa kelele zinazoendelea zinatokana na kuzipigia debe kampuni tatu za Kichina ambazo zimewasilisha serikalini maombi ya kujenga kipande cha 3 na cha 4 kwa wastani wa bei ya dola milioni 5.5, sawa na Sh bilioni 12.65 kwa kilomita. Gharama hii iko juu kwa zaidi ya dola milioni 1.5, sawa na Sh bilioni 3.45 ikilinganishwa na gharama za sasa za ujenzi zinazotumika.

“Kaka hapa kinachofanyika ni watu wanataka wagawane hizo Sh bilioni 3.45. Tukiwakubalia nchi itapoteza zaidi ya Sh trilioni 2. Hizi fedha zitaingia mifukoni mwa watu na kwa kweli haikubaliki. Tujenge reli kwa utaratibu wa zamani ambao tumeanza nao. Huu mchakato wa zabuni ukianza sasa, kwanza, hautakamilika, lakini hata ukikamilika ni miaka mitatu ijayo. Tutapoteza mwelekeo. Tuendelee kama tulivyokuwa tumalize hii reli, wanaopigania matumbo yao tuachane nao,” amesema mtoa habari mwingine.

JAMHURI limezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, aliyekiri kuyasikia hayo maelezo wanayotaka mchakato uanzishwe wa kutangaza vipande vya 3 na 4 vya reli naye akasema: “Sisi tupo kumsaidia Mheshimiwa Rais. Tunaamini kwa masilahi mapana ya nchi hii, reli hii ujenzi wake ulianza na unaendelea vizuri.

“Kuna utaratibu wa kisheria wa ‘single sourcing’ ikiwa anayetoa zabuni anazifahamu gharama halisi za mradi. Naamini utaratibu huu ni mzuri na utatupunguzia kelele. Rejea yaliyotokea mwaka 2016. Kelele zilikuwa nyingi kuliko sasa na tuliendelea kwa masilahi mapana ya taifa letu. Matunda bora kabisa ya ujenzi yanaonekana.”

Kadogosa anasema anasubiri mchakato wa kumpata mzabuni unaondelea serikalini ukamilike ‘Kazi Iendelee’.
JAMHURI linafahamu kuwa kuna kundi la watu wanaoamini kuwa baada ya kufariki dunia Rais John Magufuli, kwa sasa wanaweza kupenyeza masilahi yao binafsi katika miradi ya kitaifa na kujipatia fedha nyingi. Gazeti hili litaendelea kufuatilia sakata la mradi huu kuhakikisha nchi haiingizwi katika gharama zisizostahili na wajanja wachache.

Mwisho.....
Siwezi kua na uhakika na usahihi wa kile kilichoelezwa. Ila jambo moja la uhakika ni juu ya wapigaji kutafuta mwanya maana kwa magufuli aliwabana roho hadi kupindukia. Jambo muhimu mama samia japo hana ujuzi kama shujaa magufuli afuate model ya magufuli maana walaji wana moyo mpya na wamemzunguka. Wanafanya kila hila awachukie makomrade waliyoaminiwa na magufuli ili waweze kupenyesha mirija yao kuibia taifa. Akifuata magufulists na kuwaamini mradi wa reli utamalizika bila fisadi kuongeza gharama mara mbili au hata tatu kuibia nchi yetu.
 
Mafisadi watetea wachina na wezi wa kichina naona washaanza ufisadi.. Bahati nzuri sana sanaaa, Mama Samia naamini kwa 100% hawezi kuruhusu huu upuuzi.

Mh. Rais wetu awe makini sana sanaaa na wastaafu wa serikali ya 4 na Spika, sbb Spika amekuwa nae mtetezi wa wachina, hivyo, Mh. Rais wetu naamini yuko macho sana.

Mungu utusaidie, mafisadi wanajipanga na wako tunawaona. Mungu waangamize, Mungu utuokoe watanzania.
Pengine humjui mama Samia vizuri, tutaacha lini kuwaamini Hawa viongozi wa CCM?
 
Yote haya yanatokana na watu kutosema ukweli ulio bayana ili watu wajue. Unapofumbafumba na kuficha taarifa, hapo unawapa hao madalali nguvu za kuendelea.

Hawa watu ni akina nani. Siyo lazima kuwataja majina lakini kuna njia za kuwaelezea kiasi kwamba hata wao wataanza kuona hatari ya wanayotafuta kuyatekeleza.
Sintashangaa sana kama ndio wale wale wanaohusika na bandari ya Bagamoyo!

Kuandika tu kijumla jumla namna hii na kuficha kabisa taarifa zao hakuwazuii kamwe kuendelea na hujuma zao.

Hawa ni maadui wa taifa, haisaidii kuwaonea aibu hata kidogo.
Kumbe unawajua!
 
Sikukubaliana na JPM kwenye mambo mengi ikiwemo Udikteta, Uonevu na Mradi wa Ndege

Lakini namuunga mkono sana kwenye mradi wa Stieglers na SGR

Kwa hiyo Mheshimiwa Rais Taarifa hii ya Gazeti la Jamhuri imetushtua sana wanananchi, na hivyo tunasema hivi hatutaki Madalali wa Kichina kwenye ujenzi wa SGR
--------------------------------------------------------

Mafisadi wajipanga

Jamhuri September 21, 2021 Mafisadi Wajipanga

Ni vigogo wazito serikalini, waanza figisu ujenzi wa reli ya SGR

Washirikiana na wazabuni wa nje kuhujumu ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’

Waanzisha kundi wakijiita wazalendo, latajwa ni fedha mbele

Kenya walipigwa bilioni 18.4 kila kilomita, wailengesha Tanzania

DODOMA
Na Mwandishi Wetu

Sikio la kufa halisikii dawa. Hili ndilo linaloweza kusemwa kutokana na baadhi ya wanasiasa na watendaji serikalini kuanza mpango wa hatari wa kukwamisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR; JAMHURI limebaini.

Mpango huo unaosukwa kwa umakini mkubwa, una malengo mawili. Kwanza, kujipatia fedha kwa njia yoyote ile na pili ni kuihujumu Serikali ya Awamu ya Sita kuonyesha kuwa haiwezi kusimamia ujenzi wa reli kama ilivyokuwa awali.

Hivi karibuni kumekuwapo taarifa inayosambazwa na watu wanaojiita ‘wazalendo’ ikitoa shutuma za kuhusu mchakato wa ununuzi unaoendelea vipande viwili; ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’, wakitaka utumike utaratibu uliokwamisha ujenzi wa reli tangu enzi za uhuru.

Kuna mgogoro mkubwa unapikwa chini kwa chini na baadhi ya wanasiasa na wataalamu wakitaka vipande viwili vya reli vya kutoka Makutupora hadi Tabora (Lot 3) na Makutupora hadi Isaka (Lot 4) zabuni itangazwe tena, waingize kampuni zao.

Tayari kuna kampuni kadhaa kutoka China ambazo zimewasilisha serikalini nia ya kujenga vipande hivyo na bei wanayotaka kutoza hata kabla zabuni haijatangazwa.
Mbaya zaidi, moja ya kampuni zilizoomba mwaka 2015, iliomba kujenga reli yote kwa gharama ya dola milioni 6.2 kwa kila kilomita, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita.

Kwa urefu wa reli unaojengwa wa kilomita 1,063 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, mkandarasi huyu alitaka alipwe dola za Marekani bilioni 6.59, sawa na Sh trilioni 15.2 za Tanzania.

Ukiacha ughali wa gharama, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa mkandarasi huyu na wengine walikuwa na upungufu mkubwa uliomsukuma hayati Rais Dk. John Magufuli kuwakataa.

“Muhimu Watanzania wakajua hili group (kundi) la wanaojiita wazalendo ni kina nani. Kwa kudokeza tu hili ni group la watu ambao wanatetea masilahi binafsi, hasa kwa sababu tayari walishakula huko nyuma na wanataka ‘ku-retire imprest’,” anasema Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na kuongeza:

“Huu ni mlolongo wa matukio. Mwaka 2016 serikali ilipoanza hatua za ujenzi, kampuni pekee iliyojitokeza kuunga mkono serikali ilikuwa Kampuni ya Yapi Merkezi. Katika hatua za awali zilijitokeza kampuni 40, lakini wakati wa kurudisha zabuni kampuni 39 kutoka China zote zilijitoa. Cha kusikitisha hata benki moja ya China iliyokuwa imeahidi kutoa fedha, ilikataa ikitoa sababu zisizokubalika.

“Kwanza, benki hiyo ilisema Tanzania imeamua kujenga reli kufuata ‘standards’ (viwango) za kimataifa, yaani kwa kufuata AREMA Standard. Wao hawakulifurahia hili kwa sababu walitaka kufuata standard za Kichina, ikiwa na maana vitu vyote viwe vya Kichina. Kama kuna mtu haelewi tunachozungumza, waulize majirani zetu Kenya. Walifanyiwa mchezo huu.

“Pili, hawakutaka Tanzania ijenge reli kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kisasa, yaani ‘European Level 2 (digital)’, ambayo ndiyo inayotumiwa duniani kote. Walitaka kutuletea teknolojia ya zamani (analogy) kama ya Kenya.

“Tatu, hawakutaka kutumia upembuzi yakinifu wa kwetu. Walitaka wafanye upembuzi wao mpya, na watwambie wanatujengea kwa bei gani. Walitaka makandarasi wote watoke kwao, ‘consultant’ wa mradi wa kwao, ‘design’ Mchina, ‘insurer’ wao na pengine mwishoni kuwa na masharti ya kuendesha wao kama walivyowafanyia majirani zetu. Na hili halikukubalika, na halikubaliki serikalini Tanzania.

“Nne, hawakupenda kubadilishwa kwa mipango yao ya kushirikiana na mafisadi wachache kufuja fedha za walipa kodi waliopanga kufanya na watu wao ambao ndio wanaohaha kila mahala kuihujumu serikali iliyopo madarakani. Mipango haikuwa yenye heri kwa taifa. Kwanza, reli iliyokuwa ijengwe Tanzania ilikuwa kama ile ya Kenya ambayo ni ‘Second hand railway with old technology’, ambayo duniani haitumiki tena,” anasema mtoa habari wetu.

Mtaalamu huyo anatofautisha reli waliyotaka kujenga makandarasi hao na hii iliyojengwa sasa na Yapi Merkezi kwa kusema: “Kwanza, reli yetu ina uwezo mkubwa sana, kwa maana ya kubeba mzigo mkubwa ekseli 35. Reli nyingi zilizojengwa Afrika zina ekseli 25. Ni reli ambazo haziwezi kuchukua mizigo mizito, hasa kwa mtindo wa ‘double stack’.

“Ukitaka kubadilisha reli ya ekseli 25 kwenda ekseli 35, hii pekee itaongeza bajeti kati ya asilimia 15-17.5 ya jumla ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Pili, reli inayojengwa Tanzania inatumia teknolojia ya kisasa ‘digital’ (European Train Control System Level) ikilinganishwa na analojia inayotembea kasi ya kilomita 80 kwa saa hapo kwa jirani zetu. Kubadilisha mfumo kutoka ‘analogy’ kwenda ‘digital’ unahitaji kutumia asilimia 7 hadi 7.5 ya jumla ya bajeti ya ujenzi wa reli ya kisasa. Na ujue kwamba unapozungumzia teknolojia kwenye reli, unazungumzia mawasiliano (signaling na telecommunications).

“Tatu, reli inayojengwa Tanzania inafanyiwa kitu kinachoitwa ‘continue welding’. Maungio ya reli yamechomelewa kwa teknolojia ya hali ya juu sana. Kubadilisha reli kuipeleka kwenye ‘continue welding’ bajeti inaongezeka kwa asilimia tano ya bajeti ya ujenzi wa reli.

“Nne, reli inayojengwa Tanzania ni ‘electrified line’ (ya umeme). Reli itatumia umeme badala ya dizeli, lakini pia itaweza kupitisha treni za dizeli ukilinganisha na walizotaka kujenga za injini za dizeli pekee.

“Mambo mawili muhimu; kwanza, treni ya umeme ni rahisi mara tatu kuliko treni ya dizeli. Ukitaka kubadilisha treni ya dizeli uweke miundombinu ya umeme inabidi utumie asilimia 25 ya gharama yote ya ujenzi wa reli.

“Tano, reli inayoijenga Tanzania ina kasi ya kilomita 160 kwa saa ikilinganishwa na hiyo waliyotaka kutujengea ya kilomita 80 kwa saa waliyojenga Kenya. Kubadilisha kasi ya kilomita 80 kwa saa kwenda kilomita 160 kwa saa, itahitaji kutumia bajeti isiyo chini ya asilimia 15 ya gharama zilizotumika kujenga reli yote,” anasema.

Anaongeza kuwa iwapo Kenya wangependa kujenga reli sawa na ya Tanzania katika hiyo gharama ya dola za Marekani milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita, ilibidi waongeze asilimia 70 ya bei hiyo na kuwa dola milioni 10.5, sawa na Sh bilioni 24.15 kwa kilomita au asilimia 70 ya gharama zote za kujenga reli.

Hii ina maana kuwa Tanzania imejenga reli hii kwa gharama ndogo ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka. Kwa wastani hii reli ya umeme ya ‘Standard Gauge’, Tanzania inajenga kilomita moja kwa dola milioni 4.1, sawa na Sh bilioni 9.43.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa ujenzi wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro; ambacho ni kilomita 300, kwa maana ya kilomita 205 za njia kuu na kilomita 95 za njia ya kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 1.22 ikijumuisha na VAT. Ukigawa kilomita 300 kwa kiasi hicho cha fedha, unapata wastani wa dola milioni 4.07 kwa kila kilomita, ikiwamo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Kipande cha pili cha Morogoro mpaka Makutupora ya Singida chenye urefu wa kilomita 422, zikiwa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishania, kinajengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.924. Ukigawanya kwa kilomita 422 ni sawa na dola milioni 4.6 kwa kilomita moja ikijumuisha VAT.

Ikumbukwe kipande hiki cha reli kimepita milimani kwa zaidi ya kilomita 120, ikiwamo na kuchoronga mahandaki (tunnels) zaidi ya kilomita 2.7.

Kipande cha tano cha Mwanza mpaka Isaka chenye urefu wa kilomita 341 kikiwa ni njia kuu kilomita 249 na kilomita 92 zikiwa njia za kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.33. Ukigawa kwa kilomita 341 inakuwa dola bilioni 3.9 kwa kila kilomita moja, gharama hii ikijumuisha VAT.

“Sasa angalia kituko cha upembuzi yakinifu uliofanywa Novemba 2015 na kampuni inayoomba sasa kujenga vipande vilivyobaki kwa kutumia wanasiasa na wataalamu wachumia tumbo. Hawa walitaka wapewe mradi wote wa reli kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma. Kila kilomita moja walitaka kuijenga kwa dola milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita moja,” anasema mtoa taarifa na kuongeza:

“Na hiyo reli ambayo ingejengwa ni kama ya Kenya. Na kama ingejengwa tukataka ‘ku- upgrade’ ifanane na ya sasa ya kwetu, serikali ingetakiwa kutumia gharama zaidi ya asilimia 70. Maana yake nini? Ukiongeza asilimia 70 ya dola milioni 6.2 kwa kilomita moja, maana yake tungejenga kilomita moja kwa dola milioni 10.5 ili tupate reli ya ‘standard’ inayojengwa na Yapi Merkezi.

“Nini maana ya gharama hizo nilizozitaja? Maana yake ni kuwa gharama inategemea na eneo (terrain) ukipita kwenye milima na kuchoronga mahandaki, gharama ni tofauti na ujenzi wa sehemu nyingine. Hao hao waliotaka kutujengea reli ya kizamani kwa kilomita moja kwa dola milioni 6.2, leo ndio wanaopigiwa debe na wanataka kuwaamanisha Watanzania kuwa ni wazalendo. Walikwisha kusaini mkataba mwaka 2015 ambao Rais Magufuli alisema hautambui,” amesema.

JAMHURI limefahamishwa kuwa nchi nyingi Afrika zimeliwa katika ujenzi wa reli kwa kutumia gharama ya kati ya dola milioni 5.1, sawa na Sh bilioni 11.73 hadi dola milioni 8.0, sawa na Sh bilioni 18.4 kwa kilomita bila asilimia 18 ya VAT.

“Sasa kelele zimeanza wanataka tuwape hawa kazi hii. Sisi tunasema hapana. Tumsaidie Rais Samia [Suluhu Hassan] nchi yetu isiingizwe majaribuni. Utaratibu uliotumika kupata wazabuni kwa ‘Lot 2’ na ‘Lot 5’ ndiyo utumike kupata wa ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’. Kinacholengwa kufanywa hakina masilahi kwa taifa letu,” amesema mtoa habari mwingine.

Duniani ujenzi kama uliofanywa na Tanzania kwa takwimu za mwaka 2015, wastani wa ujenzi wa kilomita moja ya reli ni dola milioni 3.5, sawa na Sh bilioni 8.05 bila kodi ya VAT.
Kwa mabadiliko yaliyotokea ya bei za vifaa ikijumuisha na kupanda kwa bei ya chuma, bei ya mafuta, bei ya saruji na vifaa vingine inakadiriwa sasa kuwa wastani wa kujenga reli ya umeme kilomita moja inagharimu dola milioni 4.0, sawa na Sh bilioni 9.2.

Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa kelele zinazoendelea zinatokana na kuzipigia debe kampuni tatu za Kichina ambazo zimewasilisha serikalini maombi ya kujenga kipande cha 3 na cha 4 kwa wastani wa bei ya dola milioni 5.5, sawa na Sh bilioni 12.65 kwa kilomita. Gharama hii iko juu kwa zaidi ya dola milioni 1.5, sawa na Sh bilioni 3.45 ikilinganishwa na gharama za sasa za ujenzi zinazotumika.

“Kaka hapa kinachofanyika ni watu wanataka wagawane hizo Sh bilioni 3.45. Tukiwakubalia nchi itapoteza zaidi ya Sh trilioni 2. Hizi fedha zitaingia mifukoni mwa watu na kwa kweli haikubaliki. Tujenge reli kwa utaratibu wa zamani ambao tumeanza nao. Huu mchakato wa zabuni ukianza sasa, kwanza, hautakamilika, lakini hata ukikamilika ni miaka mitatu ijayo. Tutapoteza mwelekeo. Tuendelee kama tulivyokuwa tumalize hii reli, wanaopigania matumbo yao tuachane nao,” amesema mtoa habari mwingine.

JAMHURI limezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, aliyekiri kuyasikia hayo maelezo wanayotaka mchakato uanzishwe wa kutangaza vipande vya 3 na 4 vya reli naye akasema: “Sisi tupo kumsaidia Mheshimiwa Rais. Tunaamini kwa masilahi mapana ya nchi hii, reli hii ujenzi wake ulianza na unaendelea vizuri.

“Kuna utaratibu wa kisheria wa ‘single sourcing’ ikiwa anayetoa zabuni anazifahamu gharama halisi za mradi. Naamini utaratibu huu ni mzuri na utatupunguzia kelele. Rejea yaliyotokea mwaka 2016. Kelele zilikuwa nyingi kuliko sasa na tuliendelea kwa masilahi mapana ya taifa letu. Matunda bora kabisa ya ujenzi yanaonekana.”

Kadogosa anasema anasubiri mchakato wa kumpata mzabuni unaondelea serikalini ukamilike ‘Kazi Iendelee’.
JAMHURI linafahamu kuwa kuna kundi la watu wanaoamini kuwa baada ya kufariki dunia Rais John Magufuli, kwa sasa wanaweza kupenyeza masilahi yao binafsi katika miradi ya kitaifa na kujipatia fedha nyingi. Gazeti hili litaendelea kufuatilia sakata la mradi huu kuhakikisha nchi haiingizwi katika gharama zisizostahili na wajanja wachache.

Mwisho.....
Mimi Kama Mtanzania ambaye naishi maisha magumu lakini nataka nchi yangu iendeleee kimaendeleo naumia sana kusikia ufisadi Tanzania unarudi kwa kasi sana Tanzania.Inauma roho jamani kusikia watu wataweka tirrioni 02 mfukoni inauma roho sana aseee.
 
Hapa hatuzungumzii plan na uasisi wa mradi bali tunazungumzia gharama za mradi!!

Kwamba mkataba na Mchina ulikuwa kujenga 2560m kwa USD 7.6 Billion, ikiwa ni less than TZS 7 billion per kilometer; hapa tunadanganywa Mkataba na Mchina ungegharibu TZS 14.2 Billion per kilometer... yaani twice na taarifa rasmi!

Yaani watu kwa makusudi wanasema uongo ili kulinda legcy!!
Habau wee upo less informed amna atakayekujengea reli ya umeme kww hiyo pesa mchina alitaka kujenga kama ile ya Kenya hata kikweta alisema hilo wew unashupa shingo tu
 
Design ya SGR ya Magufuli ni bora kuliko design ya SGR ya Kikwete. Huo ndiyo ukweli.
Sasa kujaribu kuturudisha kwenye SGR dizaini ya kizamani wakati JPM alikuja na kitu kizuri zaidi "electrified" hatuwezi kukubali
Watu mnapopoma tu bila kufikiri.Magufuli ndio alikuwa sterling wa kusimamia michakato yote ya ujenzi wa Reli ya kisasa na baada ya kujifunza SGR ya kenya ndipo Tanzania ikaja kivingine kabisa,nakumbuka pale jangwani wakati wa kampeni za kumnadai Magufuli,Kikwete akiwa Rais alisema wameenza Mpango wa kujenga Reli ya kisasa na akeenda mbali kusema chini ya Magufuli anaamini mpango huo utafanikiwa.Magufuli naye akaahidi.Immediately alipoapishwa mipango ikaanza, kwa kinywa chake Magufuli baada ya kukutana na Rais wa Uturuki Magufuli akasema walikuwa wameomba kwa ajili ya Ujenzi wa SGR ikiwemo bank ya EXIM CHINA, lakini wamepewa masharti magumu kuwa kila kitu kitoke china,ndipo wakaamua kuongea na waturuki na akamwahidi Rais wa Uturuki kuwa kampuni za kituruki zitapewa kipaumbele kwa Rais wa Uturuki amonesha kuunga mkono.Na ikumbukwe Rais wa uturuki alikuja bongo kuchochea machakato.Hivyo hayo ya kusema SGR ya magufuli ni bora kuliko ya kikwete ni ujuha tu kikwete hadi anaondoka hakuwa ameanza mradi SGR ili ikuwa ni ahadi iliyokuja kuchochewa sana na ile COALITION OF THE WILLING" Kenya,Uganda na Rwanda.
 
Labda hujui kuwa Samwel Sitta wakati huo akiwa waziri mwenye dhamana ya mambo ya usafirishaji kipindi cha JK alishaanza mchakato wa ujenzi wa hiyo reli, Kikwete akamzuia, akasema Wangoje rais mpya afanye hiyo kazi.

Kikwete mwenyewe alipokuwa kwenye trip ya kuangalia ujenzi wa SGR alisema kuwa mpango wao wa awali wa SGR Magufuli aliuboresha kwa kuifanya iweze kuaccomodate locomotives zinazotumia umeme
 
Labda hujui kuwa Samwel Sitta wakati huo akiwa waziri mwenye dhamana ya mambo ya usafirishaji kipindi cha JK alishaanza mchakato wa ujenzi wa hiyo reli, Kikwete akamzuia, akasema Wangoje rais mpya afanye hiyo kazi.

Kikwete mwenyewe alipokuwa kwenye trip ya kuangalia ujenzi wa SGR alisema kuwa mpango wao wa awali wa SGR Magufuli aliuboresha kwa kuifanya iweze kuaccomodate locomotives zinazotumia um
kumbe unakubaliana na mimi kua Kikwete aliucha mchakato na hakuanza mradi.
 
Kama habari ni za kweli,uwezekano Mkubwa wa atakayejaribu kuzuia matakwa ya wale wanaotaka kule hizo trilioni kadhaa za reli,hakika nahisi kupotezwa kwake.Hela nyingi sana hizo,damu inaweza ikamwagika.
Yes.

Up to all hilo ndilo linaweza kutokea.
Nimeona ndg Kadogosa amejibu kiutu uzima, amefaham hapo kuna watu wanataka pesa na akajibu akijua yeye hawezi kuwazuia ila yupo kumsaidia Rais.

Tatizo Rais mwenyewe haeleweki kwenye issue sensitive kama hii, unaweza kudhani yupo na wananchi kumbe 😳!.
 
Back
Top Bottom