Teknocrat
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 3,816
- 8,456
Aisee...Nyie watu ndo maana mnadanganywa kirahisi sana kwa sababu ni wakurupukaji!! Kwavile umetumia magazeti kama source yako, ngoja nikukumbushe ambacho kiliwahii kuandikwa hapo nyuma:-
Hapo juu, ni habari ya mwaka May 2015 kutoka Reuters. Habari kama hiyo ilichapishwa na Gazeti la Mwananchi November 2015 ambapo lilitujuza:-
Utaona hapo ingawaje zilizochapwa na vyombo viwili tofauti kwa nyakati tofauti, lakini wote wanasema umbali wa 2560km kwa $7.6 Billion ambayo ni sawa na TZS 16 Trillion by the time.
Sasa chukua hiyo TZS 16 trillion au hata TZS 17 Trillion na gawanya kwa 2560 km ambapo utapata less than 7 billion per kilometer!! Sasa wewe hizo 14 Billion sijui mmezitoa wapi!!
Mbaya zaidi, Shirika la Reli wenyewe wanasema:-
View attachment 1948857
Wanatuambia Dar to Makutupora wamejenga kwa 7.1 Trillion! Je, ni umbali gani huo? Wenyewe hawa hapa tena:-
View attachment 1948855
Utaona hapo kipande cha Dar to Makutupora ni 722km, na kimejengwa kwa 9.8 billion per kilometer!!!
Na kwa nyongeza tu, hapo kabla mpango ilikuwa ni kujenga Mtandao wa Reli and not just SGR from Dar to Kigali.
Hizo figures ulizoweka ambazo hata hivyo hazieleweki inawezekana mwandishi kachanganya madesa kati SGR from Dar es salaam to KIgali vs Railway Network!!
Tafuta makarabrasha ya mpango wa ujenzi wa MTANDAO wa reli nchini, ndipo utagundua Mtandao wa Reli ni total ya SGR plus matawi yake ndo hayo gharama zake zilikuwa $9 Billion.
Moja ya matawi maarufu yanayoweza kukumbukwa na kila mmoja ni lile ambalo lilikusudia kuunganisha Bandari ya Bagamoyo na Central Railway inayoenda Kigali.
Tawi lingine ni lile ambalo lilikuwa liende Mchuchuma!
Lakini kama ni SGR ya kutoka Dar to Kigali, tenda ambayo ilitolewa ilikuwa $7.6 Billion, na kwa hesabu za wakati ule ilikuwa ni takribani Sh 17 Triilion.
Hapo ndipo narudia, kwavile tunachukulia gharama ni flat rate, chukua basi hiyo Sh 17 trillion kisha gawanya kwa 2560km, ambayo kama average ya gharama itakuwa kama hii iliyopo sasa, it means itakuwa more expensive ukilinganisha na ile mnayodanganya watu kwamba tulipigwa!!
Umeyachambua mataputapu kwa vielelezo vyenye timeline
Halafu mpango mzima ulikuwa wa JK, wengine walidandia treni kwa mbele....