Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Genge linalopinga SSH kuwa Rais kwa muhula wa pili, mgetafuta tu kazi za kufanya

Hii nchi Rais tena wa CCM akiishashika muhula wa kwanza ndo imetoka hvyo hadi amalize vipindi vyote viwili labda afe...
Halijawahi tokea ktk nchi hii Raisi kujipigia debe mapema hivi as if kampeni zimeanza,huyu muda wake unahesabika,anajilisha tu upepo anapima maji ya bahari kwa njiti ya kiberiti
 
Sisi kama watanzania huru Tusio na Vyama na wale wa vyama mbalimbali, tunaandaa mpango mkakati wa kuitisha maandamano ya amani kushinikiza Rais Samia agombee tena Urais 2025, hata kama yeye hataki sisi tutamlazimisha

Tunafanya hivyo kwasababu tumeridhishwa na kasi ya maendeleoo yake ndani ya miezi sita hii, pia ameonekana kukomaa kisiasa hana visasi vya ajabu ajabu anajua kukontroo uchumi,

nyote mmejionea miezi sita hii vituo vya afya vinajengwa kila kona madarasa jila kona, wafanyakazi wamepandishwa madaraja, mei mosi ijayo mishahara ibaongezeka,

ujenzi wa miradi mikubwa unaendelea, ndege tano zimeagizwa, Ajira zimemwagwa na bado zingine zinakuja kwa vijana,

tutakua sio waungwana kama tutashindwa kumpongeza, Rais huyu hapendi sifa ila kazi yake inaonekana,

Twende na samia mpaka 2030,

FB_IMG_16317275264021188.jpg
 
Mtoa mada upo sahihi kabisaaa.

Kwa katiba hii mbovu kuna watu wanaamini mama atapigwa chini kitu ambacho sio kweli,ni Bora kutafuta kazi ya kufanya kuliko kutegemea mama ataachia kiti
 
Sisi kama watanzania huru Tusio na Vyama na wale wa vyama mbalimbali, tunaandaa mpango mkakati wa kuitisha maandamano ya amani kushinikiza Rais Samia agombee tena Urais 2025, hata kama yeye hataki sisi tutamlazimisha...
Uchuro huo!
 
Halijawahi tokea ktk nchi hii Raisi kujipigia debe mapema hivi as if kampeni zimeanza,huyu muda wake unahesabika,anajilisha tu upepo anapima maji ya bahari kwa njiti ya kiberiti
amekanusha maneno yaliyoandikwa na gazeti la uhuru, hajajipigia debe
 
Huyu ndo twamtaka awe Mgombea wenu ili tumchalaze kwenye uchaguzi saa 4 hasubuhi, 2025 hakuna ccm Kama CHAMA tawala nawambia
Sisi kama watanzania huru Tusio na Vyama na wale wa vyama mbalimbali, tunaandaa mpango mkakati wa kuitisha maandamano ya amani kushinikiza Rais Samia agombee tena Urais 2025, hata kama yeye hataki sisi tutamlazimisha...
 
Kukiwa na fair competition kwenye chama hawezi kuingia hata kwenye 5 bora.
Kwanini kuwe na fair competition kama kwenye general election hakuwi na fair competition, kwenye chama atapita kwa mwendo wa kata funua kama wanavyofanya kwenye uchaguzi mkuu.

Unadhani akina January wamewekwa kwa kazi gani, anatengeneza strong base and believe me ndani ya mwaka watatengenezwa watu ambao watakuwa wanaogowa kama walivyotengenezwa akina Bashiru, Polepole, Makonda and the likes.

Kwa msaada wa mkali wa strategies Mzee wa Msoga bi SASHA hatoyumbishwa na makundi yote yanayompinga ndani ya CCM yatapigwa roba slowly but surely mpaka yataishiwa pumzi. Ndiyo raha ya kushika mpini, Jiwe alianza hivyo hivyo mpaka ikafikia waziri mzima na akili zake akamuita Mungu.
 
Ameshasema atagombea, sasa wewe unataka maandamano ya nini?

Au kwa vile Sirro rafiki yenu ndio mnajidai.
 
Mnakosea kushabikia hii kitu. Na inaonesha mnafurahia kifo cha DKT JPM. Sawa, subirini 2025 kauli zenu zinawagharimu.

Kumuombea mama kwa Mungu apite 2025 ndio kushabikia na kufurahia kifo cha mwamba magufuli!!!!

Sinaga upumbafu wa kufurahia kifo cha mtu mzehe.
 
Heri ukae kimya mzehe. Una statistics za kuonyesha mama hapendwi??? Au vicomment vya mitandaoni vinawaongopea 😁😁😁😁 amini ucamini mama anapita. Mwenyezi Mungu ajaarie inshaalah
Tulia, SSM ina wenyewe wewe
 
Nimeipigia kura CCM reasonably kabisa 2015/2020 lakini siwezi kuupigia ujinga wa hivi eti kura 2025. Bibi ni very unfit to run the state and state matters. Wapinzani nawapa kura zangu diwani-raisi regardless whatsoever
 
Kama anafikri kupata urais ni kazi Rahisi mwaka 2025 nchi ingie kwenye uchaguzi wa urais ikiwa na katiba mpya, tume huru ya uchaguzi,polisi na vyombo vingine vya dola wajiweke kando na kuipigania CCM aone kama atatoboa.
 
Tanzania ina population ya watu zaidi ya m60. Ukisema ufuatilie maoni ya watu mitandaoni wanaomchukia hawafiki hata 1000 wanaomsema vibaya, sawa na idadi ya mtaa/kitongoji.

Samahani kukukwaza kuusu gwajima n.k.
Haya bwana mkuu, tuombe Mungu hiyo 2025 tuendelee kuwepo Ili tushuhudie.
 
Inshaalah apite mamaetu 2nampenda sana.
Tumwombee afya njema na umri mrefu maana wahafidhina hawajapendezwa na nia yake ya kuwania kiti hivyo wanaweza kufanya kila hila kumdhuru au kumkwamisha ili asifike 2025
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu


Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
MABADILIKO YATATOKA NDANI YA CCM
 
Back
Top Bottom