Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.

View attachment 1938704
Wananchi wanataka rais wa kupigania maslahi ya umma sio mtu anatuletea habari ya rais mwanamke. Awe mwanamke au mwanaume umma hawana haja na rais wa kutetea maslahi ya mabwanyenye. Wanataka mtu muadilifu na shupavu. Asiye muoga au kutishika. Sio mtu unagombea urais ili eti kwenda waonesha wanawake kwamba na wao wamekua rais.
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Nani aachie URais kizembe zembe? Safi Sana mama umewapasha live
 
Ndiyo maana kagoma kutoa katiba, madaraka ni matamu usisubutu kuyaonja unaweza kufia ofisini.
 
UNAFIKI ni kitu kibaya sana si alipiga marufuku watu kutangaza kuhusu kugombea 2025? 😳
Hayo ameyasema leo akizungumza na wanawake
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo akishiriki katika maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani DIAMOND JUBILEE Dodoma kwa kusema wanawake hao wanapaswa kusimika Rais kwa kumchagua na yeye amesema mwaka 2025 ndio mwaka ambao Rais wa kike atachaguliwa.

Amesema hayo baada ya kurejea kwamba Rais mwanamke aliyepo kwa sasa ni kwa kudura za mwenyezi Mungu na matakwa ya katiba.
Hivyo mwaka 2025 wanawake wajitafakari na kuweka/kusimika Rais wa kike.
 
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
Katiba ipi na kifungu kipi?!!..Yeye alikua Makumu wa Raisi/amekuja kuwa Raisi Kwa Mujibu wa Katiba!!..2025 anagombea rasmi!!.. anaweza kuongoza for 14 Years kama akipenda na chama kikiona inapendeza!!
 
Back
Top Bottom