Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
555
500
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
MABADILIKO YATATOKA NDANI YA CCM
 
Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
697
1,000
Katiba ipi hiyo unaizungumzia,Samia ana sifa zote za kugombea,by the way CCM huwa Wana utamaduni ambao wanamwachia raisi aliyeko madarakani awe mgombea tena.kwa hiyo Kuna uwezekano mkubwa 2025 tukaendelea na raisi wetu mwanamke ,MUNGU akitupa uhai .
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
 
James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,092
2,000
Jiwe na ukatili wake na ubabe wake Ila jasho lilimtoka 2020.

Huyu bibi Hangaya Hadi kufika hiyo 2025 atakuwa kishasusa
Wewe ndio unaomba asuse, hasusi ng'o. Bora uanze kujiandaa kisaikolojia kwasababu mama atachukua mitano tena!
 
sirkaka

Member
Jul 22, 2021
16
45
kwa darubini ya ndani ukiangalia kwa umakini ,mama hana nia ya kusimama kugombea urais 2025,ila atahakikisha ataweka mazingira rafiki ya mwanamke kusimama .Ukiangalia hata waziri wa ulinzi aliye mteua hivi majuzi huyu mama Tax ni madhingra ya kuandaa wakina mama majembe yatayo kuja kusimama 2025 kuomba ridhaa wa wananchi mnukuu kauli yake "tusipo fanya kipindi hichi ambacho tuna nafasi haitakuja kutokea mwanamke kusimama" that's her wish.
 
Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
327
500
Rais anajikanganya. Anaongea kitu ambacho ni patently untrue,anaposema wanawake walipigania ili mwanamke awe makamu wa rais.
Anajipinga maneno yake mwenyewe aliposema uamuzi ulikuwa wa Magufuli bila yeye kufanya jitihada yoyote,zaidi tu ya kusubiri na macho ya kulegea.
Hii msg nataka kicraft vizuri,lakini all of a sudden hii simu yangu inanisumbua. Labda ndio baraka zake yule mdada.
Lakini, honestly,mi namuhofia huyu rais usalama wake,nikifikiria Nebukadneza aliondoka ghafla,sasa huyu itakuwaje.
Kinachotokea hapa,nimebaini,ni mambo kuonekana yanakwenda absolutely normal,kumbe all the while serikali inakwenda kwenye cul de sac,,halafu ghafla rais anatoweka
 
Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
8,178
2,000
Mungu asaidie mama apite inshaalah. Wacopenda wavimbe adi wapasuke.
Mnakosea kushabikia hii kitu. Na inaonesha mnafurahia kifo cha DKT JPM. Sawa, subirini 2025 kauli zenu zinawagharimu.
Kumuombea mama kwa Mungu apite 2025 ndio kushabikia na kufurahia kifo cha mwamba magufuli!!!!

Sinaga upumbafu wa kufurahia kifo cha mtu mzehe.
Muwe makini na kusherehekea kwenu. Kumbukeni mwaka haujaisha.
 
nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,440
2,000
Yaani we unaongea kama hauko tanzania. Wapinzani mbona wanashindaga lakini anayetangazwa ni mwingine. Jpm tu kabla hata watu hawajapiga kura alikuwa tayari ana kura nyingi ametengenezewa na tume na hilo lisu alilizungumzia. Ushindi wa ccm hautegemeani na kura za wananchi.
Mhhh. Lissu hakuwa na ubavu wa kumshinda JPM. Hata akigombea 2025 atapigwa tu. Huyo hakuna kitu.
 
Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
661
1,000
Mhhh. Lissu hakuwa na ubavu wa kumshinda JPM. Hata akigombea 2025 atapigwa tu. Huyo hakuna kitu.
Kwa,nini mikitano yake ilikuwa inavamiwa na polisi na wakati mwingine mawasiliano yanakatwa baada ya kuona nyomi ya watu. Amefanyiwa kila figisu lakini bado watu wanajaa bila hatamatangazo tofauti na jpm ambapo vyombo vyote vilitangaza popote alipo. Hata ushindi wake unafikiri ilikuwa rahisi kuutangaza!!
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,846
2,000
Mhhh. Lissu hakuwa na ubavu wa kumshinda JPM. Hata akigombea 2025 atapigwa tu. Huyo hakuna kitu.
Hata Magu mwenyewe aliliona mapema kwamba hatobowi asingefanya alie fanya asinge kua Raisi tena, wa tzania anataka mabadiliko ya kisiasa ole wake huyu Mtemi hangayi akijisahau kufanya yake hata tomboa, haijalishi ni Lissu au Mbowe, wataznia walishaelimika kwa sasa
 
Jan 17, 2016
27
45
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom