Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Nchi nyingine ya pili inayounda Jamuhuri ya muungano ni ipi?
Hii ya sehemu ya Tanzania munaisema nyinyi lkn Zanzibar haiko. Zanzibar ni moja ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.
KWAHIYO MAGU KUFA NI BARAKA KWAKE???
 
Mm kama jina langu lilivyo nasema mama apewe 10 tena kwa sababu zifuatazo.
1. Yeye ndie mwenye uwezo wa kubadili katiba na kubadili kila kitu.
2. Upinzani uendelee kujiandaa
3. CCM hawajawahi kumweka madarakani mtu sahihi naamini atakuja mpuuzi mwingine kama kichaa aliyekufa,
3. Rais mpya anakuwa na wafadhili wengi sana pamoja na wahisani kwa hiyo automatically ataliangamiza taifa kama kawaida yao.
4. Mama atafanya vitu kuprove wrong watu kuwa wanawake hawafai na hawana uwezo kuongoza nchi. Japo kuna wanaume hawalidhiki kupelekwa putaputa na mwanamke ila mvumilie tu.
6. Akija rais mwingine kutoka ndani ya CCM basi umasikini utaongezeka zaidi.
 
Hakuna logic basi ya Muungano. Muungano haupo 100%
Nikuhakikishie tu kwamba muungano upo tena kisheria. Hii huitwa international contract. Kwenye muungano huu tunapotofautiana pande mbili kinachoangaliwa ni sheria ya muungano ya 1964 ( Act of the union) na Articles of the union na katiba ni katika kuendesha mambo tu.
 
Mawazo mazuri ila hapo sidhani kama ataweza kufanya hayo kwa kuwa nao mfumo ndio bado unaaongoza nchi wala cio yeye
Ana settle vitu taratibu, anamfunga sabaya na the likes huku anapuliza kwa mbowe. CCM hadi kuja kujua baadae sana. Najua mama ni mbishi sana kwa sababu wazee wa ccm watataka awafinye wapinzani magufuri styles lakini atafanya kwa kuwaridhisha tu ila ukimuona kiundani Samia anajua History yake na maisha yake hayana nafasi katika urais kwa hiyo hana cha kupoteza. Yy akimaliza mda wake atasaurika kama karumi, kwani hajui marais wa Zanzibar Tanzania hawana nafasi. Marais wanaokumbukwa Tanzania ni Nyerere,Mkapa,Kikwete na Magufuri. Hao wa Zanzibar taa inazimagwa
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.


Alisema Rais Samia Suluhu


Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Nduguyo 2025 ni mbali msiwaze huko tuwatumikie wananchi
 
Back
Top Bottom