Rais Samia: Walimu mambo mazuri yanakuja, Bandari ya Musoma kujengwa

Rais Samia: Walimu mambo mazuri yanakuja​

walimu pic

Serikali imeahidi neema kwa walimu huku ikiwataka waendelee kufanya kazi kwa ari na moyo wa kujituma,

Ahadi hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Februari 7, 2022 wakati aliposimama Wilayani Butiama kwaajili ya kusalimia wakazi wa wilaya hiyo.

"Walimu hoyeee, walimu mpo eehh sasa naomba niwaambie walimu mambo mazuri yanakuja endeleeni kuchapa kazi tumewajengea madarasa mazuri sasa kazi kwenu" amesema bila kufafanua zaidi.

Rais Samia amewataka wakazi wa Wilaya ya Butiama kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiletea maendeleo huku akisema kuwa Serikali itaendela kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo endelevu,

"Nimewasikiliza Wabunge wa mkoa wenu na ninachowambia ni kwamaba sisi tutaendelea kutoa fedha kwaajili ya maendeleo lakini wananchi nanyi lazima muendelee kufanya kazi, mkulima lima,mfanyabiashara pia endelea " amesema

Awali akizungumza na wananchi wa Butiama, Rais Samia alisema Serikali imedhamiria kufufua bandari ya Musoma ianze kufanye kazi ili kuwezesha usafiri wa meli katika kuufungua uchumi wa Mkoa wa Mara na Taifa,

Mkuu huyo wa nchi alisema nia ya Serikali ni kuona Mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo ndio maana imeendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na uwanja wa ndege wa Musoma.

Pitia hapa pia Rais Samia awaweka njiapanda RC, ma-DC, DED Mara

Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho kwaajili ya kuanza ujenzi wa soko la madini Wilayani humo.

Dk Kiruswa amesema kuwa serikali inatambua mchango unaotokana na sekta ya madini hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa mazuri.

"Tunataka muwe na soko zuri kama wenzenu wa sehemu zingine kama vile Geita na hii itaboresha na kurahisisha shughuli zenu amesema" Dk Kiruswa.

Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa, Kupitia mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari- Butiama utasaidia kumaliza changamoto ya maji katika Wilaya ya Butiama.

Amesema mbali na mradi huo lakini wapo kwenye mchakato wa kufunga Pampu katika mradi wa maji wa Butiama ambao umeshindwa kutoa maji kwa muda baada ya Pampu hiyo kuharibika hivyo kukakimilika kwa ufungaji huo pia kutasaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa maji katika mji wa Butiama

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 72, na shule shikizi vyumba vyumba 6.
Rais huyu anafanya mambo ya kutisha aise,

Mpaka 2030 kwa kudra za manani tutakuwa mbali sanaa,
 
Hakika Rais Samia ameletwa Tanzania kuliponya Taifa,

Kitendo cha kukutana na Tundu Lissu Brussels Ubelgiji ni kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo kwa Taifa,

Tumuunge mkono Rais wetu kwa haya kwani anastahili sana,
 
Rais Samia: Walimu mambo mazuri yanakuja​

walimu pic

Serikali imeahidi neema kwa walimu huku ikiwataka waendelee kufanya kazi kwa ari na moyo wa kujituma,

Ahadi hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Februari 7, 2022 wakati aliposimama Wilayani Butiama kwaajili ya kusalimia wakazi wa wilaya hiyo.

"Walimu hoyeee, walimu mpo eehh sasa naomba niwaambie walimu mambo mazuri yanakuja endeleeni kuchapa kazi tumewajengea madarasa mazuri sasa kazi kwenu" amesema bila kufafanua zaidi.

Rais Samia amewataka wakazi wa Wilaya ya Butiama kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiletea maendeleo huku akisema kuwa Serikali itaendela kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo endelevu,

"Nimewasikiliza Wabunge wa mkoa wenu na ninachowambia ni kwamaba sisi tutaendelea kutoa fedha kwaajili ya maendeleo lakini wananchi nanyi lazima muendelee kufanya kazi, mkulima lima,mfanyabiashara pia endelea " amesema

Awali akizungumza na wananchi wa Butiama, Rais Samia alisema Serikali imedhamiria kufufua bandari ya Musoma ianze kufanye kazi ili kuwezesha usafiri wa meli katika kuufungua uchumi wa Mkoa wa Mara na Taifa,

Mkuu huyo wa nchi alisema nia ya Serikali ni kuona Mkoa huo unapiga hatua kimaendeleo ndio maana imeendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na uwanja wa ndege wa Musoma.

Pitia hapa pia Rais Samia awaweka njiapanda RC, ma-DC, DED Mara

Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho kwaajili ya kuanza ujenzi wa soko la madini Wilayani humo.

Dk Kiruswa amesema kuwa serikali inatambua mchango unaotokana na sekta ya madini hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa mazuri.

"Tunataka muwe na soko zuri kama wenzenu wa sehemu zingine kama vile Geita na hii itaboresha na kurahisisha shughuli zenu amesema" Dk Kiruswa.

Naye Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa, Kupitia mradi wa maji wa Mugango- Kiabakari- Butiama utasaidia kumaliza changamoto ya maji katika Wilaya ya Butiama.

Amesema mbali na mradi huo lakini wapo kwenye mchakato wa kufunga Pampu katika mradi wa maji wa Butiama ambao umeshindwa kutoa maji kwa muda baada ya Pampu hiyo kuharibika hivyo kukakimilika kwa ufungaji huo pia kutasaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa maji katika mji wa Butiama

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 72, na shule shikizi vyumba vyumba 6.
Kazi nzuri Sana
 
Elimu, Elimu, Elimu,
 
Back
Top Bottom