Bara na pwani
New Member
- Jan 2, 2014
- 2
- 9
MHESHIMIWA RAIS SASA NI MUDA WA KUWAKUMBUKA WATUMISHI WA UMMA KATIKA TEUZI ZA MA-DED, MA-DAS na Wakuu wa Taasisi za Umma
1. Tunatambua nguzo kuu mbili katika utendaji wa serikali. Ya kwanza ni ile ya watendaji katika shughuli za kisiasa ikiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri, ma-RC, na ma-DC. Ya pili ni ile watendaji walio katika utumishi wa umma ambao ni Makatibu wakuu, Naibu Katibu wakuu, ma-RAS, ma-DED, ma-DAS na Wakuu wa Taasisi za Umma.
2. Mheshimiwa Rais teuzi za ma-DC zilizotoka hivi karibuni, zimekamilisha orodha ya kujaza nafasi za watendaji wa kisiasa serikalini. Tunakupongeza sana kwa kuzingatia uwiano wa makundi mbalimbali hasa vijana kama ulivyoahidi katika hotuba yako ulipozungumza na vijana kutokea Mwanza.
3. Watumishi wa umma nao huwa wanakua katika ngazi mbalimbali za utumishi wao serikalini. Wengine wao hujiunga na utumishi wa umma katika ngazi ya uofisa utumikia katika ya miaka 3 hadi 9 kutegemea na kujiunga kupitia utumishi au kupitia taasisi zingine za umma. Kisha hupanda kuingia daraja la ofisa mwandamizi na kutumikia hapo katika ya miaka 4 hadi 6. Ngazi ya mwisho ni ya ofisa mkuu ambayo ndio ya juu kabisa kabla ya watendaji hawa kupandishwa katika ngazi ya uongozi ndani ya wizara, taasisi au kuteuliwa katika nafasi za utumishi wa umma nje ya wizara au taasisi zao.
4. Mheshimiwa Rais, watendaji hawa huwa wamekomaa na kuiva pale wanapokuwa wamefika ngazi ya maafisa wakuu lakini katika awamu zilizopita wachache sana wamekuwa wakiteuliwa na hivyo kusababisha mlundikano wa maafisa hawa wenye uzoefu mkubwa katika utendaji popote pale watakapopelekwa.
5. Katika kipindi cha nyuma teuzi nyingi zinazowahusu watumishi wa umma zimekuwa zikipewa makada na wanasiasa waliowahi kushika nafasi za kisiasa, ile mheshimiwa hii ni kuwanyima motisha watendaji wako ukizingatia wengi walio katika kada hii wametumikia kwa muda usiopungua miaka 10, kwa kuwapandisha au kuwapa majukumu mengine inatoa nafasi kwa serikali kuajiri vijana kujaza nafasi katika utumishi wa umma.
6. Mheshimiwa naomba nitoe wito kwako katika nafasi za teuzi zijazo za ma-DAS, ma-DED na wakuu wa Taasisi za Umma uwakumbuke watendaji wako ambao wako tayari kuendelea kutumikia serikali yao na ikiwezekana uwe na kanzi data ya watumishi hawa wakuu kutoka sekta zote kwenye serikali yako ili mara zote uwe unaweza kuitumia pale unahitaji kuboresha maeneo ya kiutendaji katika serikali yako.