FUWAVITA - TANZANIA
Member
- Jul 23, 2021
- 5
- 6
Kwa miaka mingi tangu Tanzania ipate uhuru wa bendera haijawahi kutokea kiziwi akapata nafasi katika uongozi , iwe
Ubunge, Udiwani, Umeya, ukuu wa wilaya , Ukuu wa Mikoa, Katibu tawala na hata Ukurugenzi. Katika teuzi za wakurugenzi za Rais Samia hatujaona akiwakumbuka walemavu wa uziwi.
Tutazidi kupiga kelele ipo siku viziwi tutapata mwakilishi maana walemavu wa aina zingine karibu aina zote zina wawakilishi kasoro wenyte changamoto ya uziwi.
Kuna wabunge wenye ulemavu wa ualibino,wenye ulemavu wa viungo, kuna katibu wa sheria asiyeona na katika uteuzi wa makatibu wa Wizara uliofanyika miezi michache iliyopita na Rais Samia aliteaua makatibu wawili wenye ulemavu wa viungo katika Wizara mbili tofauti.
Sio kwamba viziwi hatuna vigezo, wapo wenye vigezo na elimu na uzoefu wa kutosha ila tunanyimwa fursa sawa.
Hii imepelekea sauti watu wenye changamoto ya uziwi kutosikika na kusababisha umasikini pamoja na kushindwa kuboresha mfumo wa elimu ya viziwi Tanzania kwani hatuna mwakilishi wa kutusemea.
Hatutakaa kimya mpaka tupate mwakilishi.