Rais Samia wakumbuke walemavu wa Uziwi katika teuzi zako

Jul 23, 2021
5
45
Kwa miaka mingi tangu Tanzania ipate uhuru wa bendera haijawahi kutokea kiziwi akapata nafasi katika uongozi , iwe
Ubunge, Udiwani, Umeya, ukuu wa wilaya , Ukuu wa Mikoa, Katibu tawala na hata Ukurugenzi. Katika teuzi za wakurugenzi za Rais Samia hatujaona akiwakumbuka walemavu wa uziwi.

Tutazidi kupiga kelele ipo siku viziwi tutapata mwakilishi maana walemavu wa aina zingine karibu aina zote zina wawakilishi kasoro wenyte changamoto ya uziwi.

Kuna wabunge wenye ulemavu wa ualibino,wenye ulemavu wa viungo, kuna katibu wa sheria asiyeona na katika uteuzi wa makatibu wa Wizara uliofanyika miezi michache iliyopita na Rais Samia aliteaua makatibu wawili wenye ulemavu wa viungo katika Wizara mbili tofauti.

Sio kwamba viziwi hatuna vigezo, wapo wenye vigezo na elimu na uzoefu wa kutosha ila tunanyimwa fursa sawa.

Hii imepelekea sauti watu wenye changamoto ya uziwi kutosikika na kusababisha umasikini pamoja na kushindwa kuboresha mfumo wa elimu ya viziwi Tanzania kwani hatuna mwakilishi wa kutusemea.

Hatutakaa kimya mpaka tupate mwakilishi.

WhatsApp Image 2021-08-02 at 00.22.31.jpeg
 
Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
670
1,000
Suala lenu naona linakuwa gumu sana na ndio maana mnatoswa. Huwezi kuteua kiziwi bila kuajiri mtu wa kumsaidia kwenye mawasiliano.
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
3,037
2,000
Una hoja.

Ndugu zetu walemavu wa viungo ama ngozi ama ulemavu wowote ni kundi linalotakiwa kupewa kipaumbele.

Ingekua ni ushauri wangu, atleast kwenye kila uteuzi kuwe na uwakilishi wa angalau 5% kutoka kwa walemavu.

Hawa watu wanapitia changamoto nyingi sana, tuwasaidie.
 
Jul 23, 2021
5
45
Kumbe ni LAZIMA na VIPI UTENDAJI wao hebu tupe ufafanuzi.
Unajua wapo viziwi wenye elimu na uzoefu mfano Mkurugenzi wa FUWAVITA, Bi Aneth Gerana ambaye ni kiziwi wa kwanza Tanzania kufika chuo kikuu ana uzoefu mkubwa sana.

Amesaidia wanawake wenye ulemavu karibia 550 kupitia kuwawezesha kwa kuwapa mbinu za Ujasiriamali.

Pia ana degree ya sociology pamoja na shahada ya uzamili (master of strategic and peace studies).

Ameteuliwa kuwa mshauri wa bodi ya watoa ruzuku za Women Win Free Fund.

Tafadhali nenda kamfuatilie uone anavyochapa kazi na pia aligombea Ubunge kwa mara kwanza kule Dodoma akashika nafasi ya pili nyuma ya Keisha, nenda kaangalie kazi anazofanya sasa hivi Aneth na Keisha ulinganishe
 
Jul 23, 2021
5
45
Kumbe ni LAZIMA na VIPI UTENDAJI wao hebu tupe ufafanuzi.
Suala lenu naona linakuwa gumu sana na ndio maana mnatoswa. Huwezi kuteua kiziwi bila kuajiri mtu wa kumsaidia kwenye mawasiliano.
Suala la mkalimani ni kama kifaa ambacho mtumishi yeyote anahitaji kama vile computer kuwezakufanya kazi zake vizuri.

Walemavu viziwi wanatengwa kwa kisingizio cha mkalimani, je mbona kuna wasaidizi wengi wa vongozi wanaajiriwa iweje mkalimani?

kama kiziwi ana uzoefu na anawakilisha vizuri kundi lake wanaweza kushindwa kumuajiri mkalimani kwa kufuata mshahara wa watumishi wa umma?

Haya ndo yalipelekea viziwi darasa zima kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao mwaka 2018 Iringa wakati shule ni maalumu ni kwa sababu hatuna mwakilishi wa kuishauri serikali masuala ya viziwi.

Tunataka uwakilishi kwa uwiano sawa makundi yote ya watu wenye ulemavu, yawakilishe kuanzia ngazi ya kata,wilaya, majimbo, mikoa nk, ili changamoto zetu zisikike kupitia hao wawakilishi.
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
25,104
2,000
Unajua wapo viziwi wenye elimu na uzoefu mfano Mkurugenzi wa FUWAVITA, Bi Aneth Gerana ambaye ni kiziwi wa kwanza Tanzania kufika chuo kikuu an uzoefu mkubwa sana.

Amesaidia wanawake wenye ulemavu karibia 550 kupitia kuwawezesha kwa kuwapa mbinu za Ujasiriamali.

Pia ana degree ya sociology pamoja na shahada ya uzamili (master of strategic and peace studies).

Ameteuliwa kuwa mshauri wa bodi ya watoa ruzuku za Women Win Free Fund.

Tafadhali nenda kamfuatilie uone anavyochapa kazi na pia aligombea Ubunge kwa mara kwanza kule Dodoma akashika nafasi ya pili nyuma ya Keisha, nenda kaangalie kazi anazofanya sasa hivi Aneth na Keisha ulinganishe
Ukiwa unatoa majibu usifanye udogoisho haswa kwa ID yako.

Kua proffessional na ukiwa proffessional utagundua kwamba kumtaja Mkurugenzi wenu kama mfano siyo sahihi kwakua utaonekana unafanya lobbying na una uchungu na yeye kukosa nafasi.

Badala ya kumtaja yeye ungemtaja mwingine ambaye ni mwanachama wa kawaida tu.
 
Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
654
1,000
Suala la watu wasio sikia( viziwi) serikali inabidi iliangalie kwa jicho la tatu.

Kungekuwepo na mwakilishi wa watu wasiosikia katika serikali ili aweze kuwasemea maana yeye ndiye atakayejua changamoto na mahitaji yao kwa usahihi ili serikali iweze kuyafanyia kazi.

Kuna suala la gharama kubwa ya vifaa vinavyowasaidia wao kudaka mawimbi, serikali ingeliangalia swala hili angalau ikawa inachangia sehemu ya gharama ili watu hawa waweze kupata vifaa hivyo kwa bei rafiki.
 
Grena

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
597
1,000
Mbona hii inawezakana Sana tu.

Serikali ikiamua inaweza, muhimu wakalimani wa lugha za ishara wawepo.

Speaker wa bunge la vijana la Africa mashariki ni dada mwenye ulemavu wa kusikia kutoka Kenya, na anaongoza Bunge vizuri tu.

Ndo uone jinsi wenzetu wanavyowapa wenye ulemavu nafasi.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,102
2,000
Kwa miaka mingi tangu Tanzania ipate uhuru wa bendera haijawahi kutokea kiziwi akapata nafasi katika uongozi , iwe
Ubunge, Udiwani, Umeya, ukuu wa wilaya , Ukuu wa Mikoa, Katibu tawala na hata Ukurugenzi. Katika teuzi za wakurugenzi za Rais Samia hatujaona akiwakumbuka walemavu wa uziwi.

Tutazidi kupiga kelele ipo siku viziwi tutapata mwakilishi maana walemavu wa aina zingine karibu aina zote zina wawakilishi kasoro wenyte changamoto ya uziwi.

Kuna wabunge wenye ulemavu wa ualibino,wenye ulemavu wa viungo, kuna katibu wa sheria asiyeona na katika uteuzi wa makatibu wa Wizara uliofanyika miezi michache iliyopita na Rais Samia aliteaua makatibu wawili wenye ulemavu wa viungo katika Wizara mbili tofauti.

Sio kwamba viziwi hatuna vigezo, wapo wenye vigezo na elimu na uzoefu wa kutosha ila tunanyimwa fursa sawa.

Hii imepelekea sauti watu wenye changamoto ya uziwi kutosikika na kusababisha umasikini pamoja na kushindwa kuboresha mfumo wa elimu ya viziwi Tanzania kwani hatuna mwakilishi wa kutusemea.

Hatutakaa kimya mpaka tupate mwakilishi.

View attachment 1877494
Uteuzi unafanywa kwa kulipa fadhila kwa makada wa CCM.

Wangekuwa kweli wanachagua kuendana na merit basi wangechaguliwa watu wa kila aina
 
billionea alpha

JF-Expert Member
Apr 10, 2014
1,018
2,000
Kwa miaka mingi tangu Tanzania ipate uhuru wa bendera haijawahi kutokea kiziwi akapata nafasi katika uongozi , iwe
Ubunge, Udiwani, Umeya, ukuu wa wilaya , Ukuu wa Mikoa, Katibu tawala na hata Ukurugenzi. Katika teuzi za wakurugenzi za Rais Samia hatujaona akiwakumbuka walemavu wa uziwi.

Tutazidi kupiga kelele ipo siku viziwi tutapata mwakilishi maana walemavu wa aina zingine karibu aina zote zina wawakilishi kasoro wenyte changamoto ya uziwi.

Kuna wabunge wenye ulemavu wa ualibino,wenye ulemavu wa viungo, kuna katibu wa sheria asiyeona na katika uteuzi wa makatibu wa Wizara uliofanyika miezi michache iliyopita na Rais Samia aliteaua makatibu wawili wenye ulemavu wa viungo katika Wizara mbili tofauti.

Sio kwamba viziwi hatuna vigezo, wapo wenye vigezo na elimu na uzoefu wa kutosha ila tunanyimwa fursa sawa.

Hii imepelekea sauti watu wenye changamoto ya uziwi kutosikika na kusababisha umasikini pamoja na kushindwa kuboresha mfumo wa elimu ya viziwi Tanzania kwani hatuna mwakilishi wa kutusemea.

Hatutakaa kimya mpaka tupate mwakilishi.

View attachment 1877494
Mada nzuri sana.
 
Mr Books Tanzania

JF-Expert Member
May 20, 2021
311
500
Nafikiri mngepigania maslahi ya kundi kubwa la wasiosikia,hizi nafasi za kuteuliwa anayefaidika ni yule anayeteuliwa tu.

Mfano unaweza kuniambia wasioona wamefaidika vipi kwa Amon Mpanju kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria?

Walemavu wamefaidika vipi kwa Ummy kuwa Naibu Waziri anayehusika na walemavu?
 
The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
365
1,000
Ni jambo jema sana kuwa determined kupata muwakilishi katika ngazi mbalimbali za maamuzi ya kiserikali.

Naunga mkono sana hoja hiyo. Mimi huwa nafikiri ni muhimu kwa elimu ya Lugha ya Alama kuwa sehemu ya mitaala ya ngazi zote za elimu nchini .

Msingi hadi angalau Kidato cha Nne. Watu watapata ABC's "za kuombea maji" au kuwa fasaha kabisa. Hii itasaidia kuwapa wenye ulemavu huu fursa ya kuweza ku-socialize na jamii nzima kwa urahisi.

Huenda ikapunguza kidogo ile dhana ya kuwa wao ni kundi maalum.

Kwahivyo basi, kama changamoto iliyopo sasa huenda ni fikra ya kwamba akipewa nafasi fulani katika ngazi ya maamuzi inaweza kusababisha gharama kubwa kwa uhitaji wa kuajiri mkalimani, then kila mmoja akiifahamu Lugha ya Alama itaweza kuondoa hii changamoto.

Yeyote katika ofisi anaweza kujitolea ukalimani pale unapohitajika, au asihitajike kabisa kwakuwa kila mmoja anaelewa.

Huu ni mpango wa muda mrefu lakini kufikia huko juhudi ni vema zikaanza leo.

Kwa sasa ni vema kuendelea na mpango ulio mezani, lakini pia tusibanwe kufikiri nje yake.

Poleni na hongereni kwa mapambano.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom