Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
Hakika nichukue nafasi hii kukupongeza kwa hatua mbalimbali ulizochukua na unazochukua kurekebisha mambo ya nchi yetu.
Kubwa nililotaka kukushauri ni hili la wabunge 19 waliofukuzwa na Chadema kuendelea kuwa bungeni na kulipwa mishahara ambayo ni kodi za masikini wa nchi hii.
Rais Samia uliapa kuilinda na kuihifadhi katiba ya nchi na katiba inatamka wazi moja ya sifa ya mbunge kupoteza ubunge ni kufukuzwa na chama chake wabunge hao 19 wamefukuzwa na chama chao lakini mpaka leo wanalindwa na spika haijulikani ni kwa faida ya nani.
Kitendo cha kuwalipa mishahara wakati sio wabunge halali ni wizi na uhujumi uchumi. Ni imani yetu utalichukulia hatua hilo ili kuokoa kodi za wananchi.