Rais Samia vunja Serikali ya Magufuli, unda ya kwako kabla hujachelewa

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,703
11,639
Mheshimiwa sana rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, naomba nikushauri kwa heshima na taadhima.

Acha kuweka viraka kwenye serikali ya awamu ya tano na kuifanya iwe ya awamu ya sita. Badala yake ivunje serikali ya awamu ya Magufuli na uunde ya kwako.

Kwani si umeshashika hatamu kwenye chama, au bado? Maana hicho ndicho kikwazo pekee kilichokuwepo na sasa hakipo tena.

Bila kusahau badilisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wote, weka watu wako. Hii iende pamoja na viongozi wengine waandamizi ndani ya vyombo hivyo.

Drafti wanaloanza kulicheza CCM Magufuli halina afya kwako wala chama kuelekea 2025.
 
Back
Top Bottom