Rais Samia: Vijana wa leo wanakimbilia kwenye kutaka utajiri, baada ya muda utajiri unawapiga

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
“Nilikuwa na mazungumzo na Katibu wa Chama, katipa somo, nalikopa kutoka kwake. Vijana wa leo tunakimbilia kwenye kutaka utajiri.

“Uwe na jumba zuri, gari zuri, mambo yako yaende hivyo, lakini bahati mbaya baada ya muda utajiri unakugeuka na unakupiga, kama ni nyumba au gari huwezi kutunza, utajiri ulioutaka kwa haraka haraka unakupiga.

“Tunalotakiwa kufanya vijana ni kutengeneza ukwasi, upatikanaji wa fedha kila muda, kila mara kila wakati, muwe na miradi midogomidogo

“Kazi ya Serikali ni kufanya makusanyo makubwa na kutekeleza miradi tunayoitekeleza

“Kazi yenu vijana ni kutengeneza miradi ambayo itawapatia fedha ambayo italeta mzunguko na si Serikali kuambiwa isababishe mzunguko kwa vijana.

“Vijana nendeni kajitumeni, fursa zipo.”
 
Kauli hii inadhihirisha kuwa elimu yetu ni outated.

Tafsiri unayo wewe mwenyewe🤪
 
Vijana wengi wanabeti maisha, watapata shida sana uzeeni.

Always kijana anafanya Jambo ambalo kuna mtu alifanya na akafanikiwa, vijana ndio wako hivyo, kama unaona wanataka utajiri wa haraka then wanajua kuna watu wamekuwa matajiri wakubwa Kwa short times Tu

Ukiona kijana anabet basi ujue kuna mtu alifanikiwa Kwa kubet tu na yeye ana hope atafanikiwa
 
Hamjamuelewa hapo, yaani anamaanisha kijana ukipewa teuzi fasta tu unajilimbikizia mali halafu ukitumbuliwa huna njia ya kuingiza pesa tena CCM asee!!
 
Back
Top Bottom