robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 740
- 1,214
Kuharibu sifa za watangulizi ni mtindo ulioanzishwa na Kikwete ndani ya chama kile kile cha CCM! Nauona ukiendelea kwa nguvu zote. Maofisini wizi umepamba moto.
Alipoingia Kikwete alimfanya Mkapa kama ni hovyo kabisa! Wafuasi wake wakaanza kumzomea barabarani. Hata sherehe za kitaifa akasusia nchi ikawa ni ya wana-Mtandao. Sifa zoote zikawa ni za Kikwete naye akaamini ni kiongozi bora. Waliokuwa wanamsifu wakafanya yao, nchi ikawa ni kwa sifa zote kwa rais.
Akaingia Magufuli. Wafuasi wake wakasema bora! Yako wapi? Kikwete kaa mbali umeharibu nchi. Mfumo wa nchi ukaundwa upya. Wanamtandao wakaona kama wanaonewa maana walishaaminishwa nchi ni yao kwa miaka 10. Mkapa akaibuka toka mafichoni kwa urafiki na JPM. Wananchi wakashangilia na wengine wakasononeka. Kikwete hakukata tama, akatembelea ikulu mara nyingi sana, hatimaye akagundua hana chake bora aendelee na biashara mitaani. Lakini biashara bila wizi wa kiserikali hailipi! Naamini tamaa ikarudi kwenye madaraka.
Ameingia Samia. Kikwete kaibuka kama ilivyokuwa kwa MKapa. Wafuasi wa Kikwete wakasema nafuu!! Teuzi zikaanza upya yeye akisema anafungua nchi. Walioachwa wakaokotwa tena bila kusafishwa. Waliokuwa kwa magufuli baadhi wakatoswa. Sifa zimehamia kwa Samia. MAMA! MAMA! Kila kona anaitwa MAMA.
Je, kweli anafanya kazi vizuri au ni mtindo ule ule wa kutukuzwa na kumfanya aliyepita hana maana ili waendelee ‘kuipiga’ nchi? Ndivyo tuonavyo! Tangu lini waliochafuka wakawa wasafi bila kusafishwa?