masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Kujenga umoja wa kitaifa ni kazi ngumu kuliko kujenga mabarabara marefu nchini.
Umoja huu wa kitaifa umejengwa mwa miaka mingi na kwa gharama kubwa kutoka Awamu ya kwanza na zilizofuatiwa.
Kuna ambao shula za kidini zilitaifishwa, hospitali zikafanya za umma, ubaguzi wa kidini, kieneo hata kikabila vilionekana ni anti progressive.
Mwalimu alifanikiwa katika hili.
Hata hivyo lets call a spade a spade, Awamu ya tano haikufanya vizuri katika kuendeleza umoja huo.
Upendeleo wa wazi wa kikabila uliwekwa mbele.
Maendeleo kiujumla yalipelekwa kule tunakokujua sasa kama kanda ya ziwa.
Kuna wananchi walinyimwahuduma kutokana na imani zao kwa vyama na hili lilisemwa wazi.
Kuponya vidonda hivi vya ubaguzi haichukui siku moja au mwaka mmoja.
Lakini tukubali kuwa Mama Samia kaanza vizuri katika kurekebisha hali hiyo kisiasa kwa matamshi yake ya awali.
Kinachotia shaka ni viongozi wale wale waliokuwa mstari wa mbele katika kubagua na kuonea, hawa siyo siri inabidi waondolewe ili kurudisha imani ya wananchi.
Waswahili wa pwani husema, akumilikaye mchana, usiku hukuchoma.
Mama Samia, hao usiwaonee haya.