Rais Samia, Usiruhusu wakugombanishe na umma

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Mh Rais, Kwasiku 100 ulizoongoza nchi zimekuwa za kutukuka sana, Taifa limepumua na kuonyesha mageuzi makubwa sana, Kwahakika nakupongeza sana sana, Umewathibitishia wazi unaweza kwa wale waliodhani huwezi kuongoza nchi.

Jambo la msingi leo naomba kuzungumzia kikao chako cha jana, ambapo nimesikiliza mazungumzo yako na Wahariri vya Vyombo vya habari nchini ambayo ni mazuri sana,

Pamoja na uzuri huo, Majibu yako kuhusu shughuli za kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya yamenitia hofu huko tuendako kama kweli tutatibu tatizo la nchi ama tunafunika kombe la utawala uliopita.

Kimsingi jana tulitaraji utengue AMRI YA KIRAIS iliyotolewa na utawala uliopita kuhusu kusitisha shughuli za kisiasa (za wapinzani). Lakini pia tulitaraji utupe mwelekeo wa lini mchakato wa katiba mpya utaanza, Japo la Katiba ulilijibu lakini jibu lake limekuwa lilelile alilotwambia Rais Magufuli wakati anaingia madarakani.

Suala la shughuli za kisiasa ni la kikatiba na kisheria sio la hisani ya Rais, Nimelazimika kwenda kusoma sheria ya vyama vya siasa iliyofanyiwa marejeo 2019, kifungu cha 11, haki ya chama cha siasa kufanya mikutano ipo sio hisani ya mtu yoyote bali ni utekelezaji wa sheria tu.

Sasa rais wangu UMEAPA KUILINDA KATIBA NA SHERIA ZAKE, Ninakuomba sana, liangalie hili kwa umakini, huenda kuna wasaidizi wanakupotosha kuwa shughuli za vyama vya siasa zinakwamisha maendeleo, Hao wanakugombanisha na umma.

Watanzania sisi ukitaka tusikusumbue tuache tuongee, tulie na kucheka, tutanyamaza wenyewe, lakini sio utulazimishe tuongee, utulazimishe tulie wala utulazimishe kunyamaza. Kwahakika tutakusumbua kwelikweli, si jela wala mahakama havitatutibu. Shahidi utawala uliopita.

Labla nirejee nyuma kidogo, Msingi wa mpasuko wa taifa hili hadi kufika kuvuruga uchumi na mengineyo, ulitokana mwanzo kabisa kuzuia haki za watu kukutana na kutoa mawazo yao ambayo ni haki ya kikatiba na kisheria, Waliozuia walikuja na hoja hiyohiyo ambayo leo Rais umesema kuwa unanyoosha nchi.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipoanzisha mchakato wa Katiba nchi ilikuwa hivihivi wala hakuwa na kigezo cha nchi imenyooka au imepinda, na alipoahirisha nchi ilibaki vilevile, Mchakato wa Katiba mpya hauwezi kuzua miradi ya maendeleo nchini wala hauwezi kukuzuia Mh Rais kuendesha nchi. Vivyo hivyo shughuli za kisiasa.

Katiba mpya ndio msingi wa mambo yote katika nchi, Tukipata katiba mpya itaondoa kazi ya kunyoosha uchumi wa nchi unayoifanya leo Mh Rais kwakuwa hakuna atakayekuja kuipindisha nchi tena.

Na Yericko Nyerere

IMG_20210629_092823_630.jpg
IMG_20210629_092823_640.jpg
 
Tatizo mlimsifia sana mkasahau kama huyo ni kiongozi wa CCM, vyovyote iwavyo maslahi yake na chama chake lazima ayaweke mbele, sasa mnasubiri hisani toka kwake kwa kumbembeleza hata kama anavunja sheria wazi, mnatakiwa muamke sasa mjue ni njia gani mtaitumia kudai haki yenu, muache na ule ushamba wa mapambio yasiyo na maana.
 
Hii katiba mpya mnaioverrate sana.

Katiba ina mambo mengi, mueleze mnataka kitu gani kwenye hiyo katiba mpya

Hivi hujui unaweza kupata katiba mpya na mambo yakawa vilevile!

Kenya kwa mfano, nini kimebadilika? au hukumbuki kiongozi wa tume ya uchaguzi aliyeuawa kipindi cha uchaguzi?

Nani alifuatilia? Katiba ilisaidia?

Wakati flani katiba ni muhimu ila fikra za watu ni muhimu zaidi

Hata uwe na katiba nzuri kiasi gani, ila ukiwa na watu wenye fikra za kipuuzi, haisaidii.
 
Hii katiba mpya mnaioverrate sana,

Katiba ina mambo mengi, mueleze mnataka kitu gani kwenye hiyo katiba mpya....
Ukiwauliza wakutajie preambles za kwenye katiba ya nchi not sure kama wanaweza kuzielezea.

Au ni kitu gani haswa kwenye katiba chenye tatizo ambazo akiwezi fanyiwa amendements.

Katiba ya 1977 ni ya kijamaa wangesoma rights za mwananchi ndani ya ile katiba na viherehere kama kina Fatma Karume kama kweli wapo serious na kutetea wananchi. Basi asilimia kubwa ya sheria za nchi zingekuwa challenged mahakamani.

Mfano katiba inasema taasisi ya serikali inayotoa huduma aitakiwi kuweka criteria itayomnyima mtu mmoja kupata huduma.

Sasa nenda muhimbili kaangilie baadhi ya tozo za huduma kama watu wa kima cha chini wataziweza.

Hawa watu wasumbufu tu katiba mpya katiba mpya; iweje nina uhakika hawana majibu zaidi ya kelele za kasuku.
 
Ukiwauliza wakutajie preambles za kwenye katiba ya nchi not sure kama wanaweza kuzielezea.

Au ni kitu gani haswa kwenye katiba chenye tatizo ambazo akiwezi fanyiwa amendements.
Mkuu unakumbuka tume ya nyalali na zile 40 draconian law.

Pia kuna constitutional case kibao zimefunguliwa.

ie Mtikila's case on private candidate.

Mwalimu Paul John Mhozyaa
 
Back
Top Bottom