Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,047
Amani iwe nawe Mama yetu Mpendwa!
Leo naomba nikuandikie ushauri wangu juu ya suala la mipango miji hasa kwenye mikoa yetu / majiji yetu, ikiongozwa na Jiji la Mfano Dodoma!
Kusema kweli nilitembelea Dodoma kipindi Kunambi akiwa Mkurugenzi wa Jiji na wiki hii iliyopita nilikuwa tena Dodoma kwa shughuli zangu za kuchakarika kutafuta kipato!
Napenda nikiri kuwa nilipenda sana jinsi Kunambi alivyoshughulikia suala la mipango miji kwa Dodoma. Alipima makazi na viwanja vingi na akaweka Pia utaratibu wa namna ya kujenga mfano aina ya mabati yanayotakiwa kuezekwa kwa kila eneo.
Napenda nikiri pia kuwa Kunambi ni kielelezo cha vijana waliotakiwa kupewa madaraka kwenye nchi hii kutokana na jinsi alivyosimamia maendeleo chanya hasa kwenye eneo ambalo Tanzania tumefeli kwa miaka mingi , eneo la mipango miji. Alisimamia vyema, viwanja vingi vikapimwa, makazi yakapimwa kwa kushirikiana kati ya sekta binafsi na serikali.
Kusema kweli Mama Samia, hivi juzi nilivyoenda Dodoma nilishtuka kuona kama tangu Kunambi alivyoondoka kuwa Mkurugenzi wa Jiji, ni kama watu wameanza kujenga kama wanavyopenda kwa pale Dodoma. Nimeona hata yake maelekezo ya bati za kuweka kwa kila eneo yameanza kutofuatiliwa.
Naomba Mama yetu Samia mulika na hili eneo. Kama ofisi ya Mkurugenzi Dodoma imepwaya Naomba muondoe na tafuta mwingine Kama kunambi ili asimamie suala la mipango miji kwa Dodoma.
Sijajua kama utateua Wakurugenzi wengine kwenye maeneo mengine mama, ila Naomba kama hutateua basi hawa hawa waliopo wape maelekezo rasmi ya kuanza kupima na kupanga maeneo yao. Kama utateua wengine Naomba nao fanya kikao nao kwa kuwapa maelekezo ya kupima na kupanga maeneo ya Tanzania yetu. Washirikiane na sekta binafsi na hata kutumia wanafunzi wa vyuo vya ardhi walioko kwenye mafunzo kufanikisha haya.
Mwisho mama yetu napenda kukwambia kuwa , huu ni wakati sahihi kwa watanzania kuanza kuishi maisha mazuri yenye mpangilio sawa na watu wa sehemu zilizoendelea huko. Naomba simamia miji yetu ipangwe, makazi yetu yapangwe, watu waishi sehemu nzuri zilizo pangwa na zinazotunza heshima ya binadamu.
Nikutakie weekend njema Mama.