Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Hahahaha mkuu nakuona ukiamini sukuma gang Wana nguvu sana hahahaha hivi ni vichekesho kama vile vya Voda/tigo tu .

Hawana lolote na hawajawahi kuwa na lolote Hawa wa kupiga chini

Stori za wabunge ni zao la magu na Bado wanaamini kwenye upuuzi wa magu ni stori za kitoto tu sijui watapitisha azimio hawana imani na raisi (wakati wanapitisha ye amekaa tu akiwasubiri wajikusanye kusanye ) anawaachaje kulifuta bunge

Mkuu kifupi we ni mnufaika wa sukuma gang na unawapigia promo kijanja hawa wapuuzi wataondoka mmoja baada ya mwingine na hawatakuwa na Iyo nguvu uisemayo (wakitoka tu nje ya mfumo kwisha habari yao)
Huijui Siasa ya nchi hii.

Karata ya nchii hii imeshukiliwa na Kanda ya Ziwa na ndiko kwenye sukuma gani..lakini Imani hii imesambaa nchi nzima wanaimba sukuma gang.
 
Sehemu kubwa ya matatizo amejisababishia yeye mwenyewe kwa kutokuwa na msimamo unaojulikana, na badala yake akawa anayumbayumba tu kama bendera na upepo.

Alipoanza, akawa anajitambulisha yeye na mtangulizi wake ni kitu kimoja kwa maneno, huko vitendo vikionyesha tofauti. Hii ilionyesha alitamani kurekebisha yale aliyoona hayafai katika yale yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake. Hili lilipelekea baadhi ya watu waanze kumtazama kwa karibu zaidi na kuwa na matumaini juu yake.

Wakati hajatulia vizuri ili atekeleze hayo aliyotaka kurekebisha, kama kufuta mashtaka kwa watu ambayo kesi zake hazikueleweka; mara ghafla kisharukia kwenye yale yale ambayo watu walidhani yanamchukiza. Mbowe kawekwa gerezanikihuni kihuni, pengine kuliko hata ilivyokuwa ikifanyika wakati wa dikteta Magufuli.

Watu wakawa wamechanganyikiwa na hawajui Samia anasimamia wapi.

Kuna mambo mengine yaliyoambatana na safari yake ya Kenya yaliyofanya watu wengine kumtazama kwa jicho la wasiwasi kutokana na aliyokuwa akitamka wakati wa ziara hiyo. Kiongozi mgeni, na hasa anayepokea uongozi ambao hakujinadi yeye mwenyewe kwa wananchi hupashwa kuwa na subira nayo. Huwezi kuingia mara moja na kutaka ubadili kila kitu kufuatana na matakwa yako.

Samia kajitambulisha yeye ni rais anayejali maslahi ya walanguzi/madalali na wapigaji kuliko maslahi ya wananchi wa kawaida. Hili nalo limestua watu na kuanza kuwa na wasiwasi juu yake.

Rais Samia Suluhu Hassan, kaingia akiwa na haraka ya kufanya yake ambayo ni tofauti na yale ya mtangulizi wake. Sijui haraka hii ni ya nini, na haieleweki itamfikisha wapi.

Sasa itabidi achague, ili kurudisha matumaini ya watu kwake. Akichagua kupambana kwa dhati na hawa wanaotafuta kila njia ya kuzoa mali za waTanzania, na akaonekana kweli kasimama kidete bila kujali muhusika, watu watarudi kwake. Na kama atataka kuwa Rais wa hilo kundi linalotumia kila mwanya wa kuwadumaza wananchi katika vipato vyao, sina shaka yoyote hapo atakutana na mapambano mazito zaidi katika miaka hii michache kabla ya 2025.
Mimi namuomba asimame na wananchi, asimamie kwa dhati kabisa juhudi za wananchi kuleta maendeleo ya nchi hii. Wawekezaji wenye hadhi zaidi ya wote ni wananchi wenyewe, hao wanaompapatisha ni kuunga tu juhudi za wananchi wetu.

Yeye anasema: "Tanzania inahitaji zaidi Wawekezaji wa nje, kuliko Wawekezaji wanavyoihitaji Tanzania"? Nadhani haelewi umuhimu wa Tanzania ulivyo kwa wawekezaji hao. Ndiyo, ni sawa kuweka mazingira mazuri ya kuwavutia waje, lakini hii haina maana ya kwamba thamani ya Tanzania kwa wawekezaji hao ni ndogo kuliko uwekezaji wanaouleta wao.
Magufuli hakuwahi kuwa Dikteta sahihisha hapo. Samia atavuna anachopanda inaonekana moyoni hakuwa mwema na hakuwa na utiifu wa dhati kwa Magufuli.

Kama ni ushauri anapewa sana, kwanini wakati wake mambo yawe hivi? Kwanini ashindwe jukumu la kuwa kiranja mkuu?

Kwa nini hana anachojua kwa uhakika na kutolea majibu kwa haraka?
 
Leo kwa mara ya kwanza Rais Samia amekuja hadharani na kukiri wazi kuwa anaongoza serikali iliyogawanyika vibaya, amezungukwa na wasaidizi wanao mhujumu wazi wazi na yuko kwenye vita kali ya kuupambania urais wake kwa hali na mali. Hali ni tete mnoo kwake, na hatakubali!

Bila kumumunya maneno, wacha tuuseme ukweli ili kumsaidia Rais Samia popote alipo na ikibidi utafute njia ya kutokea.

Kwanza niweke wazi jambo moja kubwa na muhimu, kwa sasa Rais Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa, yaani umechokwa. Hili halina ubishi na halihitaji takafari yote yote kubwa.

Kitendo cha mama Samia kuja hadharani na kukiri kuwa 'wenzake wanamzunguka' hivyo hatakubali! Hapo tunaona picha kubwa moja tu, maji yamezidi unga na mama Samia anahitaji msaada ili avuke.

Sasa kuna jambo moja kubwa pekee linaloweza kumuokoa mama Samia mahali alipo, hana ujanja inabidi alikimbilie. Kwa ufupi, jambo hilo ni;

Kutafuta muafaka wa kitaifa ili kuweza kuiunganisha nchi iliyoparaganyika vibaya kisiasa. Kama Samia hataweza kukaa na kumaliza tofauti zake na kundi kubwa la wafuasi wa Magufuli (sukuma gang) au wapinzani (hususani Chadema) basi ajue hawezi kutoboa. Hayo ndio makundi yenye nguvu kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, na kwa sasa yote mawili kwa pamoja (pasipo kuongozwa na mtu yoyote) yanasema wazi wazi kuwa mama Samia hafai, hatoshei kwenye kiti cha urais na hayamtaki tena. Huo ni uasi wa kisiasa.

Wakati ukuta, na majuto ni mjukuu, wenye hekima wameshaelewa!
Sukuma gang mnadhani mnaweza kumzuia Samia kuwa Rais 2025-2030?

Acha nicheke kwa dharau 🤣🤣🤣

Rudini tu mkachunge ng’ombe sahauni hii nchi kuongozwa tena kikabila na kikanda wapuuzi nyie
 
Magufuli hakuwahi kuwa Dikteta sahihisha hapo. Samia atavuna anachopanda inaonekana moyoni hakuwa mwema na hakuwa na utiifu wa dhati kwa Magufuli.

Kama ni ushauri anapewa sana, kwanini wakati wake mambo yawe hivi? Kwanini ashindwe jukumu la kuwa kiranja mkuu?

Kwa nini hana anachojua kwa uhakika na kutolea majibu kwa haraka?
Acha kuongea upuuzi jaribio la kutaka kumuua Tundu Lissu ni nini kama sio udikteta?
 
Kama hujui Hili kundi Lina kura zaidi ya asilimia 60 anzia Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Tabora , Dodoma, Shinyanga,Katavi, kigoma, Morogoro, Kagera unafikili hizo kura ni Chache?
Mpuuzi wewe kwa iyo Kagera, Mara, Dodoma na Morogoro kumejaa wasukuma??😂😂😂

Kweli nyie jamaaa ni washamba na wajinga sana!!

Na kwa ukabila wenu huo sahauni tena kushika madaraka ya hii nchi wajinga nyie
 
Acha kuongea upuuzi jaribio la kutaka kumuua Tundu Lissu ni nini kama sio udikteta?
Nani kasema kuhusu Tundu Lissu?huo ni mtazamo na fikra zako na sio tafsiri ya Udikteta kwenye hilo, Hao vibaka waliomdhuru Tundu watafuteni acheni uzushi kuhusu Magufuli, Mwambie Samia awaibue wabaya wa Lissu.

Upanzi katika mtazamo sio poa, Daudi Mwangosi, Ulimboka?Kubanda? Vifo vya kusini kuhusu bomba la gesi, Bomu la kindezi kule Arusha mmesahau et eeeh?
 
no 5 itowe maana awam iliyopta ndo ilifanya vzur na yy akiwemo ko anafanya yy anavyotaka no maana watu hawamuelewi
 
Ulivyo mpuuzi sasa! Hujui waliohusika na mauaji ya Daud Mwangosi walichukuliwa hatua? Hujui mabomu ya Arusha watu walichukuliwa hatua? Au hujui kesi za ugaidi Arusha?

Utakuwa mburundi wewe ambae unabisha Magufuli hakuwa dikteta! Utakuwa huna kumbukumbu kuwa aliongea wazi kuhusu kushughulikia watu wanaopingana nae kwenye suala la Barric na kesho yake Tundu Lissu akapigwa risasi
 
no 5 itowe maana awam iliyopta ndo ilifanya vzur na yy akiwemo ko anafanya yy anavyotaka no maana watu hawamuelewi
Watu gani hawamuelewi zaidi ya nyie wapuuzi mliojaa ukabila?

Mbona sie tunamuelewa?
 
Ulivyo mpuuzi sasa! Hujui waliohusika na mauaji ya Daud Mwangosi walichukuliwa hatua? Hujui mabomu ya Arusha watu walichukuliwa hatua? Au hujui kesi za ugaidi Arusha?

Utakuwa mburundi wewe ambae unabisha Magufuli hakuwa dikteta! Utakuwa huna kumbukumbu kuwa aliongea wazi kuhusu kushughulikia watu wanaopingana nae kwenye suala la Barric na kesho yake Tundu Lissu akapigwa risasi
Neno mpuuzi ni mhemko wako katika kufikiri au ni kionjo cha akiri yako? Huwezi kushinda kwa kupiga mawe maoni, Tukio la Mwangosi hujui vizuri nimekupa rejea tu kuwa hakuna serikali Utopolo ukizingua inakuzingua kwa maangamizi.
 
Sijui vizuri nini tukio la Mwangosi wakati aliyehusika alishahukumiwa na Mahakama??

Nikikuita mpuuzi sio tusi iyo ni sifa yako kwa Jinsi unavyotoa hoja za kipuuzi humu!
 
Sijui vizuri nini tukio la Mwangosi wakati aliyehusika alishahukumiwa na Mahakama??

Nikikuita mpuuzi sio tusi iyo ni sifa yako kwa Jinsi unavyotoa hoja za kipuuzi humu!
Kesi ya Lissu iko mikononi mwa Police, Magufuli anahusika vipi kwenye Udikteta? Kumbe unanyege na mimi katika kutumia neno mpuuzi?!!! Sema unatakaje? Lissu ndio vile alishachakaa tafuteni wabaya wake mmepata Rais mdemokrasia awape majibu
 
Na kama ulihusika jiandae tu! Mama Samia lazima afukue hili kabuli! Mtatafutana na kutajana wenyewe mliompiga risasi Lissu
 
Leo kwa mara ya kwanza Rais Samia amekuja hadharani na kukiri wazi kuwa anaongoza serikali iliyogawanyika vibaya, amezungukwa na wasaidizi wanao mhujumu wazi wazi na yuko kwenye vita kali ya kuupambania urais wake kwa hali na mali. Hali ni tete mnoo kwake, na hatakubali!

Bila kumumunya maneno, wacha tuuseme ukweli ili kumsaidia Rais Samia popote alipo na ikibidi utafute njia ya kutokea.

Kwanza niweke wazi jambo moja kubwa na muhimu, kwa sasa Rais Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa, yaani umechokwa. Hili halina ubishi na halihitaji takafari yote yote kubwa.

Kitendo cha mama Samia kuja hadharani na kukiri kuwa 'wenzake wanamzunguka' hivyo hatakubali! Hapo tunaona picha kubwa moja tu, maji yamezidi unga na mama Samia anahitaji msaada ili avuke.

Sasa kuna jambo moja kubwa pekee linaloweza kumuokoa mama Samia mahali alipo, hana ujanja inabidi alikimbilie. Kwa ufupi, jambo hilo ni;

Kutafuta muafaka wa kitaifa ili kuweza kuiunganisha nchi iliyoparaganyika vibaya kisiasa. Kama Samia hataweza kukaa na kumaliza tofauti zake na kundi kubwa la wafuasi wa Magufuli (sukuma gang) au wapinzani (hususani Chadema) basi ajue hawezi kutoboa. Hayo ndio makundi yenye nguvu kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, na kwa sasa yote mawili kwa pamoja (pasipo kuongozwa na mtu yoyote) yanasema wazi wazi kuwa mama Samia hafai, hatoshei kwenye kiti cha urais na hayamtaki tena. Huo ni uasi wa kisiasa.

Wakati ukuta, na majuto ni mjukuu, wenye hekima wameshaelewa!
Mama anapwaya sana kilo ya nyama imefika tsh 10000/= bei ya mafta ya kula juu mafta ya nishati juu machinga kila mwezi tsh 20000/= haijalishi unauza mchicha au unashona viatu! Vifaa vya ujenzi baadhi ya mikoa kigoma kagera mara mwanza shinyanga na geita bei juuuuuuu zaidi katika hali hiyo hakuna wa kumpenda
 
Mi sioni kigumu hapo,ushauri wangu ni kuwa tu achangamshe yale waliyoyaanzisha awamu ya 5 kwani inaonekana kama kuna kupungua kwa speed kidogo,otherwise she is still on right track,lastly asiwe mvivu kumfyatua mtu ambaye anahisi kutokwenda na speed yake hii itamsaidia sana itajenga discipline...
Speed yake ipi??
 
Umesema ukweli kabisa mkuu. Wabunge wengi walioko mjengoni walipata mteremko ndani ya chama, na kwa wananchi kwa sababu ya Magufuli (rip), hata wao wenyewe wanalijua hilo. Ule upepo wa JPM ulikuwa unavuma kivingine kabisa huko mitaani. Kwa hiyo kumshauri rais Ssh asifanye kazi na watu wa JPM ni kumchimbia kaburi.
Watu wengi huku mtaani wanamnanga kwa sababu wanamwona amejitenga sana na mtangulizi wake, ambaye yeye alikuwa makamu wake. Rais Samia anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu sana na watu aliochaguliwa nao, na kujikita zaidi kwenye kutekeleza ilani yao ya uchaguzi.
Ushauri kuntu akina makamba ambao amewaamini kuwa ndo mhimu hawaaminiki tena kwa wanachi .kww hiyo hata hapa mtaani watu wameshaampuuzia sana mama kuwa anarudish yale mambo ya ajabu ajbau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom