Habari wana JF,
Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.
Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.
Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!
Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.
1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.
Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.
Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.
Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.
Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!
Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?
Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!
Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.
2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.
Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?
Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.
Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.
Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.
Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.
Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.
Naomba hii iwe part 1
Asante Mh Rais kwa usikivu wako.