Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Urais wa Samia Suluhu Hassan umeanza na upole. Umeanza na uungwana wa kuwa tayari kupoteza baadhi ya marafiki ili mradi tu taswira yake kimataifa iweze kubakia na heshima. Akaenda Ubelgiji akaonana na Tundu Lissu wakati ambao wapo wana CCM wengi tu wasingependa kumuona akijishusha (kwa mujibu wa fikra zao) namna ile.
Akamfungulia Mbowe na kumualika ikulu kufanya nae mazungumzo. Baada ya kukisia kilio cha muda mrefu cha maaskofu na wanaharakati wenye kutoa maoni yao kwa vyombo vya habari. Ameonyesha uwezo wa kujishusha na kufanya mijadala ya kimaongezi. Amejitahidi kuliishi jina lake 'suluhu' kwa vitendo.
Lakini anao maadui kwani huwezi kuongoza nchi ukakubalika kwa kila raia unayemuongoza, haijawi kutokea hali ya aina hiyo mahali popote haswa kwenye nchi zilizo katika michakato ya ukuzaji wa demokrasia ya kivitendo kama Tanzania. Binafsi nimemuelewa sana Rais Samia.
Wapo wale wenye mawazo ambayo kwa kingereza wanaitwa ni conservative. Wapo wale wenye hulka kwamba Mwanamke hana hadhi ya kuwaongoza wanaume, wapo wale waliomkubali mno hayati JPM na kile alichokuwa akikihubiri majukwaani na kukiishi kila siku. Wapo wale ambao ni 'waafrika' kweli kweli wenye mawazo yale yale ya mzungu kuvalishwa mtumba baada ya mwafrika kutengeneza nguo akaivaa na kisha akaisafirisha kuipelekea Ulaya.
Hawa wanaona siku zote kuwa viatu vya hayati JPM ni vikubwa mno kwa Samia kuweza kuvivaa na vikamtosha, tatizo lao lipo akilini zaidi. Ndani ya ufikiriaji mzima (mindset) walionao. Ni ngumu kuweza kuwabadilisha kile wanachofikiria. Hawakuweza kuijua mipango ya Mungu walidhani maadam JPM alishaapa na kuingia ikulu basi angeendelea mpaka 2025. Kipindi kile cha msiba, hawa ni miongoni mwa waliolia hadharani na kwa uchungu mkubwa.
Ni kama wana hasira fulani japokuwa wakiulizwa wanakana kwamba hawana kinyongo au ghadhabu inayowasumbua. Hawa ni maadui wanaokua katika suala zima la mbinu za kuupinga uongozi wa awamu ya sita. Walimpenda JPM lakini wanashindwa kuelewa ni kwamba Samia alikuwa msaidizi muhimu wa JPM. Wanamnyanyapaa kwa sasa wakiwa mbali ya kamera lakini enzi za uhai wa JPM walifanya hivi hadharani kabisa, hawakuijua mipango ya Muumba ni ipi.
Ninapenda kumkumbusha Rais SSH kwamba upole wa awamu yake unaweza huko mbeleni kuleta ugumu wa kuelezea haya anayoyafanya kwa sasa, kama yameyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja. Kwa maana kwamba hawa wanaojichekesha mbele ya macho yake wanaitumia mitandao kwa mapana ili aonekane hana anachokifanya.
Hawa jamaa wa JPM wamegeuka kuwa ni mabingwa wa utengenezaji wa hizi fake news zinazozagaa mitandaoni. Tatizo ni kwamba habari inaweza kuwafikia watanzania 10000 na kati yao watakaoamini ni 9500 na pakawepo watu makini 500 wenye kuweza kuielewa hiyo propaganda kwa kina.
Lakini tayari wapo wale 9500 waliokwisha kuaminishwa na kile kinachokuwemo katika habari ya kubuni isiyo na ukweli wowote. Ikiwekwa mtandaoni habari nyingine itasomwa na watu milioni moja. Kati ya hao watakaoiamini wanaweza kuwa ni laki tisa na ile laki moja ikaweza kuitilia mashaka. Wale laki tisa ni wengi kiasi cha kuamini uzushi kuwa ni habari ya ukweli.
Rais SSH aitumie nafasi hii kulishughulikia hili tatizo kabla halijawa sugu na kukwamisha ufanisi wa kile anachokifanya ambacho kwa kiasi kikubwa na umaliziaji wa miradi iliyoachwa na hayati JPM. Akiwa hai JPM aliweza kuishughulikia mitandao inayosambaza fake news na akaogopwa kwani msimamo wake ulieleweka kwa kila mtu.
Rais SSH kwa upole na uungwana wake ataivumilia hii hali lakini itakwenda ikiharibu kile anachotaka kukifanya. Wanaopotoshwa na fake news ni wengi, na uwezo wetu wa kupima ukweli na mantiki ya kile kinachoandikwa na kusambazwa mtandaoni siku zote unatofautiana.
Wanaopaka matope ufanisi wa serikali hufanya hivyo kwa kivuli cha demokrasia hata kama wanawafanyia kazi watu wenye nia ovu dhidi ya serikali na mipango yake. Ni hali ya kuishughulikia kwa kutumia busara na umakini wa hali ya juu.