Rais Samia, unaweza kuanzisha timu ya mpira wa miguu kuchochea ajira na 'legacy' yako

Merci

Member
Feb 6, 2012
90
135
Ahsante sana mama yetu mheshimiwa rais kwa kuanza kuja maeneo yetu sisi wananchi wako kututembelea, tumekuona na umesikia na kufahamu adha mbalimbali tunazopata na hata kuwachukulia hatua watendaji mbalimbali ambao hawaleti ubunifu katika kutatua kero zetu au hata kuongeza ugumu wa maisha.

Tutashukuru sana ukiendelea kufanya hivi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu tena ukija kwa msafara wa magari ndio nzuri kweli maana utapata nafasi ya kuonana na wananchi wengi waliokando kando ya barabara na nje ya miji.

Mheshimiwa rais ikikupendeza tutashukuru kuona unaweka "legacy" katika mambo yatakayodumu kwa wakati wote kwenye eneo la ajira kwa vijana. Katika eneo hili naomba nikushauri uweze kuanzisha timu ya mpira wa miguu itakayoitwa kwa jina lako mfano Samia Suluhu Hassan Football Club 2021 (SSH FC 202X), nimeshauri timu ya mpira wa miguu kwakua ndio mchezo wenye washabiki wengi na ligi imara ingawa mimi ni mshabiki na mchezaji wa mpira wa kikapu.

Timu hii utaipata kwa kuanzisha mashindano ya kimikoa kupata timu bora ya mkoa hapa siongelei timu zilizokuwepo tayari bali vijana wa mikoa wanaunda timu zinashindana mkoani na kupata best team iliotokana na wachezaji bora waliochaguliwa kwenye hayo mashindano.

Kisha, Mh Rais kutafuatiwa na mashindano ya kitaifa ambapo wachezaji wale waliounda timu bora za mkoa watacheza "Super Samia National Football Cup" na kupata timu bingwa na kisha kuchagua wachezaji bora wa kitaifa walau 22 pamoja na makocha na wataalam bora na hapo ndipo itakua imepatikana timu mpya ya SSH FC 202X (x ni mwaka wa kuanzisha timu). Najua ukianzisha jambo hili utapata wadhamini wengi sana na pesa za kuendesha mashindano haya zitapatikana na hata za kusajili na kuiendesha timu hii.

Pia, timu hii iweze kuanzishwa kwa mfumo wa kampuni ili wadau mbalimbali wanunue hisa ambazo zitachangia mtaji wa kuiendesha timu na pia kuweza kuwapa fursa wananchi kumiliki hisa za kampuni na kuifanya timu iendeshwe kisasa. Naamini ukipata nafasi utaweza kufikiria jambo hili likaloleta ajira, burudani na kufanya "legacy" yako iwepo siku zote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom