Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Wauza mahindi wetu wenye soko la uhakika huko Kenya sidhani kama hata wanasoma maoni yetu ya jamii forum.Hakika hatuwezi kutajirika kwa kufanya kila kitu pekee au kuishi kama kisiwa, lakini vile vile hatuwezi kushindana pasipo na mazingira yaliyo ya usawa na rafiki.Ni jibu tosha la hoja yake Phillipo Bukililo, kwamba tuwe makini na Wakenya ambao hadi kesho wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani. Wayatendayo kwa jirani zao mipakani (Uganda, Tanzania, Somali) yanatosha kueleza jinsi walivyo. Isitoshe tuna majirani zaidi wa kufanya nao biashara kuliko Kenya.
Swali la kujiuliza ni kwa nini Uhuru ghafla alimwarika Rais SSH mara tu baada ya kuhutubia Bunge letu?
Watu waliokwisha kuchanganyikiwa wakijua soko la mazao yao limetoweka hawana muda wa kufuatilia Kenya ni jirani wa namna gani.
Sisi wenyewe watanzania tunapojadiliana namna tunavyofanyiana mambo ya hovyo sisi kwa sisi, sidhani kama tunakuwa na haki ya kimaadili ya kuhukumu majirani.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuongelea juu ya usisi wetu tunapoongelea wengine lakini tunapokuwa wenyewe kwa wenyewe tunagundua kuwa huo usisi wetu ni mwepesi sana.