Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

NGARA one

New Member
May 29, 2021
4
49
Ninashauri ni wakati wa serikali kufikiria namna nzuri kufanya teuzi mbalimbali katika nafasi za serikali kwa kuzingatia uzoefu wa Kazi serikalini, uadilifu ili kutengeneza uzalendo.

Kwa mfano haileti taswira nzuri kumuacha katibu wa tarafa au maafisa wameoshika nyadhifa mbalimbali ktk Idara zao wilayani au mikoani aliekaa kazini miaka 15 na zaidi serikalini mwenye elimu ya kutosha wengine wanawazidi hata elimu Ma DC ma Das na Ma RC lkn ukapuuza utumishi wao ukatoa watu mtaani kuja kuwa Ma DC, DAS, RC’s, RAS etc.

Zamani Kila mfanyakazi alijua iwapo atahudumu kwa mda mrefu na uadilifu angefika katika nafasi ya juu kwa bidii yake ya Kazi uadilifu na kujituma, na hiyo ndio kulikozaa uzalendo hapo zamani ma Afisa utumishi, makatibu tarafa, maafisa maendeleo, kilimo, Afya, Walimu, walipanda nafasi za juu za kiselikali na hiyo ilijenga kuwa na viongozi wengi wenye uadilifu uzalendo na kupenda nchi sbb walipanda nafasi kwa mafaili yao na si kwa majina yao.

Maafisa wakuu wa idara mbalimbali kutoka sekta tofauti mfano elimu, Afya, kilimo, maendelo, utawala iwe wilayani au mkoani wenye miaka 20 ktk kazi, uzoefu na weledi serikalini ndoto zao nao ni kushika nafasi za juu ktk wilaya au mkoa unapowaletea mtu ambae hajawahi kuwa mtumishi huwaongezei tija ila unawavunja moyo na hiyo inashusha uzalendo wa nchi na tija kwenye Kazi zao, Hawa walitegemea miongoni mwao ndio atakaepanda na huo ndio utaratibu wa huko nyuma.

Mfumo huu uangaliwe upya kwa nini mfano makatibu tarafa na maafisa wengine wa wilaya wasipande kuwa Ma DAS na ma DC na wakurugenzi wa halmashauri halafu hao wapya nao wakaanzia chini kupata uzoefu na kupimwa huko chini na kujifunza kujua mifumo ya serikali inafanyaje Kazi kuanzia chini. Huko nyuma hatukuwahi kuona Ma DC ma Ma RC wakivunja maadili sbb walitokana na mfumo mzuri vyeo havikuwapa ukichaa kwani walipanda navyo polepole, hivyo waliheshimu sana utu na maadili ya Kazi na miiko ya kazi zao.

Zamani watu waioshika nafasi hizo Walionekana ni watu wenye heshima iliotukuka na wazalendo kweli kweli na Jamii ziliwaheshimu sana ila leo jamii inaziona nafasi hizo kama ni zakupewa kwa wateule fulani waliokosa fursa mahali pengine.

Na shauri serikali ianze marekebisho kwa Kurekebisha hili kwenye mkeka wa MA DAS iwapo kutakuwa na mabadiliko kwenye nafasi hizo.
 
Sikubaliani na ushaur wako aisee ulisema wawe watumishi wa serikali vipi wanaofanya private sector na wako vizuri hafu unasema achukue waliokaa serikalini 20 years hao hata utendaji huwa wa mazoea Tena hawana exposure yoyote, Bora kuteua hata wa binafsi wenye exposure ili kuleta mabadiliko
 
Hiyo ilikuwa kwa Nyerere,, Mwinyi na Mkapa ilipofika zamu ya Mkwere ndio habari ya kupeana fadhira ilipoanzia, mtu akishindwa ubunge kwenye kura za maoni au wakati wa uchaguzi basi anapozwa na UDC au U RC, URAS AU UDAS.

Na ndio maana wakienda huko makazini wanajaa kusifia tu na siasa kwa yule aliyewateua hivyo kupindisha Sheria kulinda Ugali.

Watumishi wilayani na mikoani wamekuwa yatima sana hakuna promotion wala ongezeko la mishahara.

HATA HIVYO,,, HIVYO VYEO NI VYA KUILINDA CCM IENDELEE KUBAKI MADARAKANI.
 
Watumishi wa umma wako kama watoto Wadogo kudanganywa na pipi. 2025 wapeni tena CCM Kura.
 
Hapana..! Kuchanganya ndio njia bora. Hao watendaji wa serikali unaowasema wawepo, na hao wa mtaani pia wawepo, wa private sector wawepo, wa vyama pinzani wawepo, wa jumuiya na asasi za kiraia pia wawepo, nk. Hapo ndipo tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano..
 
Hapana! Kuchanganya ndio njia bora. Hao watendaji wa serikali unaowasema wawepo, na hao wa mtaani pia wawepo, wa private sector wawepo, wa vyama pinzani wawepo, wa jumuiya na asasi za kiraia pia wawepo, nk. Hapo ndipo tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano..
Udini pia
 
Sikubaliani na ushaur wako aisee ulisema wawe watumishi wa serikali vipi wanaofanya private sector na wako vizuri hafu unasema achukue waliokaa serikalini 20 years hao hata utendaji huwa wa mazoea Tena hawana exposure yoyote, Bora kuteua hata wa binafsi wenye exposure ili kuleta mabadiliko
Bila shaka we utakuwa Delila au Eva
 
Pamoja na kuwepo na ile dhana ya kupandishwa cheo lakini bado kuna nafasi nafasi hazihitaji waliopo ofisi husika kuchukua.

Mfano, mtu kama Lazaro kalist aliyekuwa mwanasiasa baadaye meya wa jiji la Arusha, mtu kama huyo kutokana na ile nafasi ya umeya anakuwa na nafasi nzuri kutumikia kuliko yule jamaa pale.

Pia maisha yanabadirika kwa kasi, kitabu cha Mwl. Nyerere "Tanzania na hatima ya uongozi" kinatoa funzo kubwa namna bora ya kuchuja na kumpata kiongozi mzuri.
 
Hii nchi ni ya wote mwacheni rais ateue wale wenye uwezo na elimu ya isiyo na shaka bila kuzingatia wanatoka sekta gani by the way si lazima watumishi wapate promotion ya aina hiyo na uzalendo si zao promotion.
 
Hapana..! Kuchanganya ndio njia bora. Hao watendaji wa serikali unaowasema wawepo, na hao wa mtaani pia wawepo, wa private sector wawepo, wa vyama pinzani wawepo, wa jumuiya na asasi za kiraia pia wawepo, nk. Hapo ndipo tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano..
Sawa, lakini wawe na angalau mwelekeo mwema katika jamii.
 
45 Reactions
Reply
Back
Top Bottom