Ninashauri ni wakati wa serikali kufikiria namna nzuri kufanya teuzi mbalimbali katika nafasi za serikali kwa kuzingatia uzoefu wa Kazi serikalini, uadilifu ili kutengeneza uzalendo.
Kwa mfano haileti taswira nzuri kumuacha katibu wa tarafa au maafisa wameoshika nyadhifa mbalimbali ktk Idara zao wilayani au mikoani aliekaa kazini miaka 15 na zaidi serikalini mwenye elimu ya kutosha wengine wanawazidi hata elimu Ma DC ma Das na Ma RC lkn ukapuuza utumishi wao ukatoa watu mtaani kuja kuwa Ma DC, DAS, RC’s, RAS etc.
Zamani Kila mfanyakazi alijua iwapo atahudumu kwa mda mrefu na uadilifu angefika katika nafasi ya juu kwa bidii yake ya Kazi uadilifu na kujituma, na hiyo ndio kulikozaa uzalendo hapo zamani ma Afisa utumishi, makatibu tarafa, maafisa maendeleo, kilimo, Afya, Walimu, walipanda nafasi za juu za kiselikali na hiyo ilijenga kuwa na viongozi wengi wenye uadilifu uzalendo na kupenda nchi sbb walipanda nafasi kwa mafaili yao na si kwa majina yao.
Maafisa wakuu wa idara mbalimbali kutoka sekta tofauti mfano elimu, Afya, kilimo, maendelo, utawala iwe wilayani au mkoani wenye miaka 20 ktk kazi, uzoefu na weledi serikalini ndoto zao nao ni kushika nafasi za juu ktk wilaya au mkoa unapowaletea mtu ambae hajawahi kuwa mtumishi huwaongezei tija ila unawavunja moyo na hiyo inashusha uzalendo wa nchi na tija kwenye Kazi zao, Hawa walitegemea miongoni mwao ndio atakaepanda na huo ndio utaratibu wa huko nyuma.
Mfumo huu uangaliwe upya kwa nini mfano makatibu tarafa na maafisa wengine wa wilaya wasipande kuwa Ma DAS na ma DC na wakurugenzi wa halmashauri halafu hao wapya nao wakaanzia chini kupata uzoefu na kupimwa huko chini na kujifunza kujua mifumo ya serikali inafanyaje Kazi kuanzia chini. Huko nyuma hatukuwahi kuona Ma DC ma Ma RC wakivunja maadili sbb walitokana na mfumo mzuri vyeo havikuwapa ukichaa kwani walipanda navyo polepole, hivyo waliheshimu sana utu na maadili ya Kazi na miiko ya kazi zao.
Zamani watu waioshika nafasi hizo Walionekana ni watu wenye heshima iliotukuka na wazalendo kweli kweli na Jamii ziliwaheshimu sana ila leo jamii inaziona nafasi hizo kama ni zakupewa kwa wateule fulani waliokosa fursa mahali pengine.
Na shauri serikali ianze marekebisho kwa Kurekebisha hili kwenye mkeka wa MA DAS iwapo kutakuwa na mabadiliko kwenye nafasi hizo.