Ukweli lazima usemwe tu, Kuna kakikundi flani ambako Wana jaribu sana kutumia nguvu ili kuafifisha juhudi na kazi kubwa anayo Ifanya Rais wetu mpendwa.

Kwa muda mfupi aliokaa madarakani amefanya kazi kubwa ya kuirudisha nchi yetu kwenye mahusiano ya kimataifa, mahusiano ambayo yalikuwa yamepotea kabisa, wawekezaji sasa Wana miminika kwa sababu mazingira ya uwekezaji sasa ni rafiki, Jambo ambalo hapo kabla lilikuwa limeharibiwa na kakikundi flani kilicho jificha kwenye joho lauzalendo huku likiwa genge la wizi tu.

Jambo ambalo Watanzania tunapaswa kufanya ni kumshukuru Mungu kwa kulinusuru Taifa letu toka katika mikono ya maharamia wa kiuchumi waliokuwa wamekumbatia na kuhodhi njia zote za kiuchumi, Tena hawakuta kabisa mtu yeyote ajaribu kuhoji matumizi ya fedha za serikali, Jambo ambalo unge jaribu kufanya bila ya Shaka lolote linge kuletea kifo.

Mama Samia chapa kazi, hiki NI kipindi ambacho Kila anaye lipenda Taifa lake lazima atakuunga mkono.

MUNGU MBARIKI RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU HASSAN
 
Samia awe na amani! Hawa wapuuzi wachache waliozoea mbeleko kutokana na ukabila hawatusumbui. Tutadeal Nao
 
Mmakunduchi anajikwamisha yeye mwenyewe, kwa sababu hatoshi-uwezo mdogo, na kichwa chake kiko hivyo-asipambane na nuture anaweza kuumwa; angejiuzuru akabaki na heshima, CCM wakapendekeza mtu mwingine
Huko ni kujitia upofu, mbona kafanya kazi hata kumzidi mtangulizi wake, mama ana uwezo mkubwa Sana Tena itachukua muda mrefu Sana kumpata Rais mwenye uwezo Kama wa mama pale atakapo kuwa ametoka madarakani.

Ebu muacheni mama achape kazi.
 
Walikuwepo viongozi wengi toka nchi jirani mbalimbali kuaga mwili wa hayati Magufuli,mengi walizungumza mema kuhusu kiongozi huyu,
Nakumbuka hotuba ya uhuru Kenyatta ,alikwambia dada yetu njia umekwisha onyehwa na hayati Magufuli,wengi walishangilia na wewe imani yangu ulipata ujasiri

Nini kimekukuta ndani ya muda mfupi ikiwa njia ulikwisha onyeshwa?
Hebu tafakari upya tena maneno ya Uhuru Kenyatta.

Kuteleza sio kuanguka,muda unao wa kujisahihisha,serikali bado ni ileile na wewe ndio Amiri jeshi mkuu
Power power
 
🐒🐒🐒
imgvfdage12.png
 
Hadi sasa hongera sana,

Ila angalia wamachinga umetuondoa sisi ila umeacha malori kariakoo ambayo ni shida kuliko sisi.

Barabara zote mpya zinakufa ndani ya muda mfupi tu kariakoo.

Huu ni ufisadi na uhujumu uchumi,

Eti wanasema malori ni ya wakubwa hayawezi ondoka kariakoo hata yakiharibu barabara basi mujue wamachinga wanawasubiri kwenye boksi
 
Hadi sasa hongera sana,
Ila angalia wamachinga umetuondoa sisi ila umeacha malori kariakoo ambayo ni shida kuliko sisi
Barabara zote mpya zinakufa ndani ya muda mfupi tu kariakoo
Huu ni ufisadi na uhujumu uchumi,
Eti wanasema malori ni ya wakubwa hayawezi ondoka kariakoo hata yakiharibu barabara basi mujue wamachinga wanawasubiri kwenye boksi
Utashi wa raisi uko mdogo pia uwezo wa kujieleza ni mdogo pia udini unamtesa pia uzanzibari unamtesa pia

Kingine anapenda starehe pia anapenda sifa
.hawezi kujenga hoja nadhani MUNGU AMETUACHA TANZANIA
 
Namfuatilia Rais Samia anafaidi matunda ya Awamu ya Tano (Yeye akiwa Makamu). Kuna viwanda vingi sana vinazinduliwa huko Pwani na Rais, Huu uwekezaji tuipe Kongole awamu ya Tano.

Kuna watu hawakujua huu uwekezaji ila sasa wanaona.

Pongezi kwa awamu ya Tano.

Kimsingi Rais anatakiwa kufaidi matunda mda huo huo asichoke kuyafanyia kazi mapungufu yaliyochwa bila kulalamika.

Kilala kheri Rais Samia, Ukifanikisha Maji ama umeme tunafurahi sote.
 
Hujasikia leo ikisemwa kiwanda cha leo ni matokeo ya ziara kule Misri? Hujamsikia Makala akimwomba mama aongeze zaidi safari za nje ili wawekezaji zaidi waje?

Hivyo basi, ni matunda ya ziara za awamu ya sita na siyo kujifungia kwa awamu ya tano.
 
Hujasikia leo ikisemwa kiwanda cha leo ni matokeo ya ziara kule Misri? Hujamsikia Makala akimwomba mama aongeze zaidi safari za nje ili wawekezaji zaidi waje?

Hivyo basi, ni matunda ya ziara za awamu ya sita na siyo kujifungua kwa awamu ya tano.
Misiri kaenda Juzi kiwanda kinaota tu kama mchicha?. Achana na wapambe ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom