Rais Samia, una kitu cha kujifunza kutoka Zambia, jifunze!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
JE, ZAMBIA NI SHULE YA DEMOKRASIA?

Miaka ya 1990s kulifanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Zambia, Rais Kenneth Kaunda, baba wa taifa la Zambia alishindana na mwanasiasa kijana wa upinzani Frederick Chiluba akashindwa uchaguzi ule.

Mzee Kaunda(Mungu amrehemu) alipelekewa taarifa mapema na Watu wa usalama kuwa upepo wa uchaguzi ulikua ukienda vibaya, wakamtaka maoni yake wafanye Nini kumuokoa na aibu ya kushindwa, jibu lake lilikua rahisi tu, 'acheni tume itangaze kile wazambia wameamua'!

Ulikua uamuzi wa uungwana na ujasiri mkubwa,akaachia madaraka bila sokomoko lolote, ingawa kwa ujinga Chiluba alikuja kumtia misukosuko mingi baadae lakini Mzee Kaunda aliendelea kubaki muungwana.

Hili lilinifanya nimheshimu na kumpenda Sana,yeye na Nelson Mandela kwangu wamebaki kuwa wanademokrasia na wapenda haki wa kweli Katika historia ya Afrika!!!

Kuchaguliwa kwa mwanasiasa wa upinzani Hakainde Hichilema kunaifanya Zambia kuwa mwalimu wa Demokrasia kusini mwa jangwa la Sahara, Zambia inawaonyesha madikteta wengi Katika Afrika kuwa vyama vinaweza badilishana madaraka bila kuvuruga amani ya nchi na kuwa si ajabu kwa chama tawala kushindwa,si ajabu Rais aliye madarakani kushindwa!

Kwa miaka isiyopungua sita nchi yetu imerudi nyuma Sana Katika eneo hili la Demokrasia,na sasa Tanzania imekuwa nchi inayokandamiza haki za kisiasa za raia wake, yanayoendelea Tanzania kwa Sasa ni mambo ya aibu, yanayoudhi na kusikitisha Sana!!!

Rais Samia Suluhu,unayo nafasi ya kujifunza kutoka Zambia, ni fursa kwako kujenga historia yenye sifa Kama marehemu Mzee Kenneth Kaunda, ni juu yako kuamua njia ya kuelekea!!!
Binafsi nakuombea upate nuru na kulitoa taifa Katika mtanziko mkubwa kwa kisiasa tulio nao sasa, hujachelewa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom