Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Leo wakati wa kupokea ndege mpya, Rais Samia amesema pia wamenunua ndege nyingine ya mizigo kutokana na kukua kwa uchumi.
Ikumbukwe siku chache nyuma Rais Samia alisema kuwa uchumi umeshuka sana kutokana na janga la corona.Viongozi wakapiga makofi
Wengi tulimsifu kwa kusema ukweli kuwa uchumi unashuka na tukaenda mbali kwa kusema hata ile kuingia uchumi wa kati ilikuwa ni janjajanja tu.
Sasa leo tena ghafla anatuambia uchumi unakua ndio maana mmeamua kununua ndege ya mizigo.kama kawaida viongozi wakapiga makofi
Swali linabali huu uchumi umekuwa lini tena?
Hapa mnatuchanganya sana, ipo wapi consistency kwenye mnayotuambia?
Nakumbuka kipindi cha mwendazake tuliaminishwa chanjo hazifai na viongozi wote wakapiga makofi, ghafla tunaambiwa zinafaa na viongozi wote wanapiga makofi.
Tatizo kwenye hii nchi ni nini haswa? Mbona kama tunatesana sana? Au tuache tu kufatilia kila linaloendelea ili tubaki na amani.
Hii nchi nimeamini ni ngumu sana.
Au kama mmetuchoka basi si mkubali tu kuwaachia wenzenu nao tuone watatufikisha wapi. pumzikeni sasa miaka 60 inawatosha.
Maana hizi drama sio za kawaida.