Rais Samia umetuchanganya, uchumi umekua tena lini?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Leo wakati wa kupokea ndege mpya, Rais Samia amesema pia wamenunua ndege nyingine ya mizigo kutokana na kukua kwa uchumi.

Ikumbukwe siku chache nyuma Rais Samia alisema kuwa uchumi umeshuka sana kutokana na janga la corona.Viongozi wakapiga makofi

Wengi tulimsifu kwa kusema ukweli kuwa uchumi unashuka na tukaenda mbali kwa kusema hata ile kuingia uchumi wa kati ilikuwa ni janjajanja tu.

Sasa leo tena ghafla anatuambia uchumi unakua ndio maana mmeamua kununua ndege ya mizigo.kama kawaida viongozi wakapiga makofi

Swali linabali huu uchumi umekuwa lini tena?

Hapa mnatuchanganya sana, ipo wapi consistency kwenye mnayotuambia?

Nakumbuka kipindi cha mwendazake tuliaminishwa chanjo hazifai na viongozi wote wakapiga makofi, ghafla tunaambiwa zinafaa na viongozi wote wanapiga makofi.

Tatizo kwenye hii nchi ni nini haswa? Mbona kama tunatesana sana? Au tuache tu kufatilia kila linaloendelea ili tubaki na amani.
Hii nchi nimeamini ni ngumu sana.

Au kama mmetuchoka basi si mkubali tu kuwaachia wenzenu nao tuone watatufikisha wapi. pumzikeni sasa miaka 60 inawatosha.
Maana hizi drama sio za kawaida.

Screenshot_20210730-210824_1.jpg
 
Kukua kwa uchumi maana yake huweza kuwa haya:

1)Kuliwekwa "TRANSIT RESTRICTIONS" baina ya mipaka yetu mathalani KENYA/TANZANIA,RWANDA/TANZANIA,BURUNDI/TANZANIA.

-Leo hii mipaka hiyo IMEFUNGULIWA....Mizigo inapita

(Huku ni kukua kwa uchumi).

2)Serikali imeajiri watumishi 8000 naa wa elimu na afya(huku ni kuinua uchumi wao binafsi na wa nchi pia kwani wanakwenda kuboresha huduma za wananchi).

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Afadhali sasa ameshamaliza kufungua uchumi tuanze mchakato wetu wa katiba mpya kama alivyotuahidi kuwa tutauwanza punde baada ya kufungua uchumi.
Hapo ndio ulilo mtego, maana alisema wamuache akuze uchumi. Leo kasema uchumi umekua, hivyo basi aruhusu suala la katiba mpya
 
By the way, process za kununua hiyo ndege zimeanze yeye akiwa rais? Kama taratibu za kuinunua ndege hiyo zilianza kabla hajwa Raisi, na huku baada ya kuwa Rais alisema uchumi upo HOI, basi changa la macho limejificha au limefichwa sehemu.
 
Back
Top Bottom