Rais Samia umemuachaje Waziri Lukuvu bila kumtumbua?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Kongole kwa reshuffle.

Nipongeze kwa mabadiliko kidogo ya Baraza la Mawaziri,kuna watu walikuwa mizigo kama Waziri wa Ujenzi na Nishati na umewatumbua.

Lakini sasa kuna watu umewaacha Barazani ila ni mizigo mizito,mtu kama Lukuvi na Mkuchika wameshachoka kwa sasa inafaa wapumzishwe.

Ukiangalia Migogoro ya ardhi anayokumbana nayo RC wa Dar utafikiri hakuna Waziri mhusika.

Ujenzi holela umerudi kwa kasi, Watu wa Ardhi saizi wako mikoani sio Halmashauri tena,ukimpa mtendaji wa Mtaa au kata 20,000 unajenga unavyojiskia, sasa kuna haja gani ya kuwa na huyo Waziri ikiwa hata kodi ya kibali cha ujenzi hakusanyi?

Hata kama ni wakongwe sijui wakwe usiwaangalie usoni kama hawakusaidii.

Nimalizie kwa kusema Rais hapangiwi wala halazimiki kufuata ushauri wangu.
 
Back
Top Bottom