Rais Samia umekubali kutukuzwa hivi? Yanayofanyika shuleni siku yako ya kuzaliwa siyo sawa

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Nimeona jambo ambalo sikuwahi kuliona kwa maraisi wengine wote na imebibidi nishtuke kidogo. Wanafunzi wa mashule mbalimbali za msingi na sekondari Dar na mikoani nimeona leo wameimbishwa na kurekodiwa madarasani kuhusu birthday ya mama Samia.

Hawa wanafunzi hawajui chochote kuhusu siku yako ya birthday ni wazi waliletewa hilo Jambo na kuambiwa waimbe.
Sasa nachojiuliza haya yote ya nini? Yana faida gani?

Shule ya Benjamini Mkapa leo hapo inafanywa sherehe ya birthday yako na Watoto wapo nje kusheherekea hii birthday yako. Nasisitiza hawa hawafanyi kwa utashi wao kwa kuwa hata pegine hawajui tarehe yako ya kuzaliwa bali wanafanya kwa msukumo.

Kusheherekea birthday ni Jambo zuri na sina tatizo nalo, Ila huku kwenda mashule mbalimbali hadi mikoani na kuwaimbisha kisha kuwarekodi Sio sawa kabisa.

Nimeona kituo kimoja cha redio wakisema hii siku ya tarehe 27 iwe siku ya mama kitaifa.
Umekubali kutukuzwa hivi? Ikiwa umeridhia haya basi pia sina tatizo.
Happy birthday SSH.

Screenshot_20220127-111557_1.jpg
Screenshot_20220127-111505_1.jpg
Screenshot_20220127-111612_1.jpg
Screenshot_20220127-111534_1.jpg
Screenshot_20220127-111447_1.jpg
 
kwenye nchi ya ki republiki na kidemokrasia kama Tanzania, birthday ya Rais ni suala binafsi ...Haya mambo ya kutukuzana hivi tuwaachie huko kwa akina Kim Jong Un na King Mswati

Mfano Kenya hawana mambo kama haya, eti birthday ya Uhuru inasheherekewa kama sikukuu ya kitaifa?
 
Duu aibu naona mimi sasa hapo kwenye jukwaa la mwenye basidei nani atakaa au Mama itabidi aende pale Benjamini Mkapa? Kwao walitenga bajeti kwaajili ya Besidei ya Rais? No wonder unaweza kukuta shule ina upungufu wa madawati au maji yamekwatwa kwa kudaiwa lakini wana bajeti ya besidei ya Rais duu

Hichi ni kiwango cha juu sana cha kujipendekeza aiseee...
 
madawati na madarasa yanajengwa kwa fedha za mkopo
 
Nimeona jambo ambalo sikuwahi kuliona kwa maraisi wengine wote na imebibidi nishtuke kidogo. Wanafunzi wa mashule mbalimbali za msingi na sekondari Dar na mikoani nimeona leo wameimbishwa na kurekodiwa madarasani kuhusu birthday ya mama Samia...
Ukiona Binadamu anatukuzwa sana jua nyuma yake ana Dhambi nyingi ambazo hata Shetani Mkuu Mwenyewe Lucifa anazishangaa na anaziogopa pia.
 
Nimeona jambo ambalo sikuwahi kuliona kwa maraisi wengine wote na imebibidi nishtuke kidogo. Wanafunzi wa mashule mbalimbali za msingi na sekondari Dar na mikoani nimeona leo wameimbishwa na kurekodiwa madarasani kuhusu birthday ya mama Samia...
Jean Bedel Bokasa, Rais, Mfalme, Jenerali wa Majenerali wote Afrika ya Kati aliigeuza siku yake ya kuzaliwa kuwa sikukuu ya Kitaifa.
Asante Mama yetu, tunaona mwelekeo wako unakotupeleka.
 
Nimeshangaa sana akili ndogo kuongoza akili kubwa, hajahitimu hata elimu ya kidato cha sita ila watu na phD zao wanachezeshwa rede.

Hakika leo ndio nimeamini alikuwa akiichukia sana ile nafasi ya umakamu, sio kwa mapambio haya niliyoshuhudia siku ya leo.
 
Back
Top Bottom